19/12/2025
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amekerwa na hali ya kusuasua kwa Ujenzi na Ukamilishaji wa Kituo cha Afya katika Kijiji na Kata ya Mahuninga Tarafa ya Idodi halmashauri ya Wilaya ya Iringa, ambapo ametoa Maelekezo huku akiagiza wak**atwe wale Wazabuni wanaokwamisha mradi huo uliotakiwa kukamilika na kuanza kutoa huduma za Afya miezi mitano iliyopita lakini mpaka Sasa umekwama katika hatua ya umaliziaji.
RC Kheri James ametoa Maelekezo na maagizo hiyo Desemba 18, 2025, katika Ziara yake ya Ukaguzi wa hali na hatua iliyofikiwa katika Ujenzi wa mradi wa Kituo hicho cha Afya.
Aidha, katika Ziara hiyo, RC Kheri James, amepata fursa ya kufanya Mkutano wa hadhara wa kuzungumza na Wananchi wa Kata ya Mahuninga pamoja na kusikiliza na kutatua kero na Changamoto zao zinazokwamisha shughuli zao na kuchelewesha Maendeleo.