10/06/2025
Kamwe Ang'aka Baada ya taarifa hii ya Simba.
KUTOKA KWA AFISA HABARI WA YANGA •
Makolo katika hili ni bora mngekaa kimya tu. Jamii ya watu wenye Maarifa na Akili timamu, imeshajua UNAFKI wenu.
Mwanzo mlitangaza hamtashiriki Ligi tena mpaka mtakapopewa ripoti ya uchunguzi wa kilichokwamisha Derby, Ila baada ya mchongo wenu mlioset kujibu, mnatoka mbele eti mnataka tena mechi.
Wanafki wakubwa nyie.
Kilichobadilika ni nini? Ni mtu tofauti aliyeandika mwanzo akidai hamchezi Tena mpaka Ripoti itoke na huyu aliyeandika upuuzi wenu Leo?
Au kwa kuwa ile ya mwanzo iliandikwa Usiku sana tuamini mwandishi alishavesha Konyagi za kutosha kichwani akajiandikia msioweza kuyasimamia?
Niwaambie, katika hili la kudai HAKI NA RIPOTI hatuhitaji sapoti yenu. Sisi Tunajimudu na Tunaweza kuyapambania maslahi yetu bila UNAFKI WENU
Nyie tulizeni mshono, ikifika Tarehe mliyoambiwa, pelekeni Timu kachukueni pointi 3 na tangazeni ubingwa.. Mchecheto wa nini kwani? Mnaacha maswali mengi kwa watu kuonyesha mna wasiwasi na Hamjiamini
Sisi Tunasimamia Maslahi ya mpira, Haki itendeke halafu ndio Mechi halali ipangwe. Tunawatamani sana na mnalijua hilo.
Na ni vyema mkajua, mapambano yetu sio kwa ajili ya kubeba Ubingwa mezani. Sisi hatutakuwa Tayari kubeba Ubingwa Mezani bila kumalizana na nyie Uwanjani
Haki ikishatendeka, Tutawatafuta kivyovyote vile ili TUMALIZANE na Tukomeshe Kimdomo chenu
Kwa sasa Tuacheni kidogo tumalize Jambo kubwa lililo mezani.