EBONY Digital

EBONY Digital The best Swahili Radio Station from the Southern Highlands of Tanzania. Frequency; Iringa 88.1, Njombe 91.9, Mbeya & Songwe 94.5, Dar es Salaam 106.9

Frequency; Iringa 87.8, Mbeya 94.7, Dar 106.9, Njombe 88.2, Songea 102.2 MHz

Weka kwenye ratiba yako Jumamosi hiiiHaitakuwa ya kawaidaaa kabisaaa sio ya kukosa UREJESHO UTHAMANI WA MWANAMKE Sehemu ...
01/04/2025

Weka kwenye ratiba yako Jumamosi hiii
Haitakuwa ya kawaidaaa kabisaaa sio ya kukosa UREJESHO UTHAMANI WA MWANAMKE Sehemu Moja tu ni Katika Kanisa la

USIKOSEEE

 -Mkurugenzi wa vunja bei Group na mdhamini wa mashindano ya vunja bei cup-akiwa sambamba na k**ati ya mashindano ya Vun...
31/03/2025

-Mkurugenzi wa vunja bei Group na mdhamini wa mashindano ya vunja bei cup

-akiwa sambamba na k**ati ya mashindano ya Vunja bei cup Atazungumzia kuhusu maandalizi ya hatua ijayo ya mtoano 50 bora ya mashindano ya Vunja bei cup ambapo uzinduzi wake rasmi ni kesho Tarehe 1 April pale katika viwanja vya Kalenga





Aliyekuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema, amekosoa vikali taarifa iliyotolewa...
31/03/2025

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema, amekosoa vikali taarifa iliyotolewa na chama chake kuhusu tukio la shambulio dhidi ya kiongozi wa wanawake taifa wa CHADEMA (BAWACHA). Mrema alionesha masikitiko yake kwa chama kutolaani kitendo hicho cha kikatili na badala yake kudai kuwa ni taarifa zinazozungumziwa mitandaoni. Alieleza kuwa chama hakikuonyesha mshik**ano kwa kiongozi huyo, na hakutoa pole, jambo ambalo linathibitisha kutokuwepo kwa umoja ndani ya chama.

Mrema alilalamikia kauli ya chama inayodai kuwa kinachunguza tukio, wakati huo huo kikitoa vitisho kwa mhanga, jambo ambalo linaweza kuathiri uchunguzi wa tukio. Alikosoa kauli za chama akizilinganisha na za uongozi wa Rais Hayati John Magufuli kuhusu ukandamizaji wa haki za binadamu.

Katika tamko lake, Mrema alisisitiza kulaani vikali ukatili wa kijinsia dhidi ya kiongozi huyo na kusema kuwa matendo k**a haya yanapaswa kupingwa na kila mtu mstaarabu, na kuitaka jamii, pamoja na vyama vya siasa, kuungana kupinga ukatili dhidi ya wanawake.


Kapteni Ibrahim Traoré, Rais wa Serikali ya Mpito ya Burkina Faso, ametoa msamaha kwa wanajeshi 21 waliohusika katika ma...
31/03/2025

Kapteni Ibrahim Traoré, Rais wa Serikali ya Mpito ya Burkina Faso, ametoa msamaha kwa wanajeshi 21 waliohusika katika mapinduzi ya Septemba 2015. Amri hii, iliyosainiwa Machi 24 na kuwekwa hadharani Jumapili, inazingatia masharti ya msamaha yaliyopitishwa na bunge la mpito mnamo Desemba 2024. Wanajeshi hao, wakiwemo maafisa na maafisa wasio na kamisheni, walikuwa wamefungwa au kutiwa hatiani kwa matendo yao katika mapinduzi yaliyoshindwa ya 2015.

Sheria ya msamaha inatoa fursa kwa askari waliohusika na kesi hii, na wanaoonyesha kujitolea katika mapambano dhidi ya ugaidi, kupewa msamaha na kupandishwa cheo kazini.


Kanye West, mwanamuziki maarufu na mwenye utata, amekiri kwa mara ya kwanza kuwa anajuta kuwa na watoto na mke wake wa z...
31/03/2025

Kanye West, mwanamuziki maarufu na mwenye utata, amekiri kwa mara ya kwanza kuwa anajuta kuwa na watoto na mke wake wa zamani, Kim Kardashian, ambaye kwa sasa wametalakiana wakiwa na watoto wanne. Katika mahojiano na DJ Akademiks, Kanye (ambaye sasa anajulikana k**a "Ye") alisema kuwa kumpatia ujauzito Kim ilikuwa kosa kubwa alilowahi kufanya maishani mwake, akidai kuwa hakupaswa kuwa na watoto nae. Aliongeza kuwa hakupata haki ya umiliki wa watoto wao—North, Saint, Chicago, na Psalm—hata katika suala la kutoa matumizi kwa uwiano wa 50-50.

Ye na Kim walikuwa katika ndoa kwa miaka sita, kutoka 2014 hadi 2021. Baada ya talaka, Ye alioa Bianca Censori, na kuna uvumi kwamba yupo mbioni kupata mtoto kutoka kwake ili kuokoa ndoa yao, licha ya tetesi kuhusu uwezekano wa kutalakiana kwao.


Rais wa Marekani, Donald Trump, ameibua mjadala mkali baada ya kusema kuwa kuna uwezekano wa yeye kuwania muhula wa tatu...
31/03/2025

Rais wa Marekani, Donald Trump, ameibua mjadala mkali baada ya kusema kuwa kuna uwezekano wa yeye kuwania muhula wa tatu, licha ya Katiba ya Marekani kupiga marufuku jambo hili kupitia Marekebisho ya 22. Katika mahojiano na NBC News, Trump alisisitiza kuwa kuna njia za kufanya iwezekane, na hakutaka kufuta uwezekano wa kugombea tena urais. Kauli yake imezua hofu miongoni mwa wachambuzi wa siasa na wanaharakati wa demokrasia.

Kwa mujibu wa Katiba ya Marekani, rais hawezi kutawala zaidi ya mihula miwili ya miaka minne, na Marekebisho ya 22 yalipitishwa baada ya Franklin D. Roosevelt kutawala kwa zaidi ya mihula miwili. Hata hivyo, kauli ya Trump imeibua maswali kuhusu mbinu zinazoweza kutumika ili kuwania muhula wa tatu, ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya kisheria au mchakato mgumu wa kubadili Katiba.

Wafuasi wa Trump wanaunga mkono wazo lake, wakisema anastahili kuendelea kuongoza, lakini wakosoaji wanasema hili linaweza kutishia demokrasia ya Marekani na kuanzisha uongozi wa kiimla.


Ebony Fm Inakutakia wewe na Familia Yako Eid Mubarak.
31/03/2025

Ebony Fm Inakutakia wewe na Familia Yako Eid Mubarak.


Uchaguzi wa chama cha soka mkoa wa Iringa umekamilika ambapo wajumbe wa mkutano mkuu wamewachagua viongozi wapya wa chak...
29/03/2025

Uchaguzi wa chama cha soka mkoa wa Iringa umekamilika ambapo wajumbe wa mkutano mkuu wamewachagua viongozi wapya wa chaka hicho (IRFA) watakaokua madarakani kwa miaka minne ya kiutawala.

VIONGOZI WALIOCHAGULIWA NI K**A IFUATAVYO

Crypian Kuyava - Mwenyekiti
Joel Musiba - Makamu mwenyekiti
Abousufian Silia - Mjumbe wa mkutano mkuu

⛳️Wajumbe wa k**ati ya utendaji.

1. Victoria Mwenda
2. ⁠Davis Wapalila
3. ⁠Rehema Mhehe

Baada ya kupitishwa kwa makamu mwenyekiti na mkutano mkuu, kinasubiriwa kikao cha k**ati ya utendaji ambacho kitampitisha katibu atakayeteuliwa na mwenyekiti.


Muimbaji Sean Kingston na mama yake Janice Turner wamekutwa na hatia ya ulaghai na wizi. Wamekabiliwa na mashtaka ya kul...
29/03/2025

Muimbaji Sean Kingston na mama yake Janice Turner wamekutwa na hatia ya ulaghai na wizi. Wamekabiliwa na mashtaka ya kula njama ya kugushi nyaraka na utapeli wa vitu vyenye thamani ya $1 milioni (sawa na TSH Bilioni 2.68). Mashtaka yanayowakabili ni pamoja na ulaghai wa vito vya thamani ya $500,000, zaidi ya $200,000 kutoka Benki ya America, $160,000 kutoka kwa muuzaji wa magari ya kifahari, na kiasi kingine kutoka kwa benki na wauzaji wa vitanda. Hukumu yao itatolewa Julai 2025.


Balozi Juma Volter Mwapachu, mwanasiasa mkongwe na mwanadiplomasia mashuhuri, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82 ...
29/03/2025

Balozi Juma Volter Mwapachu, mwanasiasa mkongwe na mwanadiplomasia mashuhuri, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kifo chake kilithibitishwa Machi 28, 2025. Alizaliwa Septemba 27, 1942, jijini Mwanza, na alisomea sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na India. Alikuwa kiongozi muhimu katika siasa, diplomasia, na maendeleo ya kikanda, na mwanachama wa muda mrefu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Hata hivyo, alijiondoa CCM mwaka 2015, akieleza kwamba chama hicho kilikuwa kimepoteza dira.


Taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeuruhusu uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kutumika kw...
28/03/2025

Taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeuruhusu uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kutumika kwa michezo ya robo fainali na nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL) na Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC) 2024/2025.

Uwanja huo umeruhusiwa baada ya Ukaguzi uliofanywa na Wakaguzi wa CAF hivi karibuni. CAF inaendelea kufuatilia kwa karibu maboresho yanayoendelea kwenye uwanja huo.


Embeyte Medhin Hagos, mwanamke wa Ethiopia mwenye umri wa miaka 76, amejifungua mtoto wake wa kwanza baada ya miaka ming...
28/03/2025

Embeyte Medhin Hagos, mwanamke wa Ethiopia mwenye umri wa miaka 76, amejifungua mtoto wake wa kwanza baada ya miaka mingi ya kujaribu kushika mimba.

Ujauzito wake uliwezekana kwa njia ya IVF, na alijifungua mtoto wake huko Mekelle, Ethiopia, akiashiria hatua muhimu ya matibabu na hadithi ya ustahimilivu.


Address

Uhindini
Iringa
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when EBONY Digital posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to EBONY Digital:

Share

Category