01/09/2026
Mahak**a ya Wilaya ya Clark County, nchini Marekani imemkuta Duane “Keffe D” Davis na hatia ya kuhusika katika mauaji ya mwanamuziki maarufu wa rap, Tupac Shakur, aliyeuawa miaka 30 iliyopita katika shambulio la lililotokea kwenye gari huko Las Vegas.
Katika sh*taka hilo majaji walijadiliana kwa muda usiozidi saa tatu kabla ya kumkuta Davis, mwenye umri wa miaka 63, na hatia ya mauaji kwa kutumia silaha hatari, huku kosa hilo likihusishwa na nia ya kukuza, kuendeleza au kusaidia shughuli za genge la kihalifu.
Jaji wa Mahak**a ya Wilaya ya Clark County, Carli Kierny, ameweka tarehe Oktoba 13, 2026 kuwa siku ya Davis kusomewa adhabu yake rasmi na ikumbukwe kuwa Davis anakabiliwa na adhabu ya juu kabisa ya kifungo cha maisha jela.
Tupac Shakur aliuawa kwa kupigwa risasi katika shambulio la gari kwa gari huko Las Vegas mwaka 1996, na kifo chake kimeendelea kuwa miongoni mwa kesi zinazozungumziwa zaidi katika historia ya muziki wa hip-hop.
Chanzo ABC News
✍️: