NURU FM Iringa 88.9

NURU FM  Iringa  88.9 Karibu katika Ukurasa rasmi wa 88. 9 Nuru Fm. "mwangaza wa jamii"


(2)

Unasikiliza Nyambizi Mseto ukiwa wapi?cc:   📸
06/12/2025

Unasikiliza Nyambizi Mseto ukiwa wapi?

cc:


📸


Wazazi  Mjini Mafinga wametakiwa kuhakikisha Shule zitapofunguliwa mwakani Januari 13,2026 wanapeleka chakula cha mchana...
05/12/2025

Wazazi Mjini Mafinga wametakiwa kuhakikisha Shule zitapofunguliwa mwakani Januari 13,2026 wanapeleka chakula cha mchana kwa Viongozi wa k**ati ya Chakula Ili watoto waweze kupata Chakula shuleni.

Hayo yamezungumzwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa ya Ivambinungu katika Halmashauri ya Mji Mafinga Bw. Isaack Kilawa ambapo amekemea vikali tabia ya baadhi ya Wazazi kutopeleka chakula cha Watoto wao Shuleni.

Bw. Kilawa amesema tabia ya baadhi ya Wazazi kushindwa kushindwa kupeka chakula cha mchana shuleni ni jeuri isiyo na watawachukulia hatua Kali

"Naomba niwe mkweli nimekerwa sana sana mimi nakuja kwenye mkutano wa Wazazi halafu mnaniletea Dada wa kazi za ndani ilikusikiliza mkutano wangu? " Alihoji Bw. Kilawa.

Makamu mwenyekiti wa Wazazi Shule ya Msingi Mafinga Bw. Haruna Makombe, amewataka Wazazi kutobweteka na malezi ya Watoto wao.

"Wazazi tumejisahau sana na tunaona Watoto wameshakuwa Watu wazima na wanaweza kujitegemea huko ni kujidanganya" Alisema Bw. Makombe.

Naye Mwl. Joseph Kasanga ambaye ni Mkuu wa Shule ya Msingi Mafinga, alisema anashangazwa na tabia ya baadhi ya Wazazi kushindwa kuchangia chakula ambacho kinatumiwa na watoto wao na Kuelekea kukua kitaaluma.

05/12/2025

Miongoni mwa burudani zilizovutia hadhira ni mchezo wa kukimbiza vikombe, ambapo watoto walitakiwa kuvitoa vikombe vilivyokuwa upande A na kuvikimbiza hadi upande B kwa kasi. Mshindi alipaswa kuhamisha vikombe vyote kwa muda mfupi zaidi kuliko wengine,

Kila mtoto alionekana kuwa na lengo moja yaani kushinda, lakini pia kufurahia mchezo k**a sehemu ya ushindani chanya.

Burudani hii imejiri leo 5 Disemba 2025 katika Mahafali ya 26 ya Shule ya Awali na Msingi Moriah iliyopo Kata ya Nduli Manispaa ya Iringa.

📸✍



05/12/2025

Katika kilele cha mahafali ya 26 ya Shule ya Awali na Msingi Moriah, yaliyofanyika leo 5 Disemba 2025 Kigonzile, Kata ya Nduli Manispaa ya Iringa, moja ya mtoto na muhitimu wa darasa la Elimu ya Awali Hatua ya Tatu (KG3) alivuta hisia za wazazi na wageni waalikwa baada ya kuonesha miondoko ya kipekee wakati alipokuwa akicheza wimbo wa pamoja na

Kwa vibe na miondoko k**a hii, unadhani mtoto huyu anaweza kuwa kipaji kinachochipukia kwenye sanaa ?

📸✍



Tukutane baadae pale Savana Lounge & Night Club  kwenye Usiku wa Ally Choki  Mzee wa farasi.📸
05/12/2025

Tukutane baadae pale Savana Lounge & Night Club kwenye Usiku wa Ally Choki Mzee wa farasi.

📸


Mwaka huu 2025 umekuwa mzuri kwa muziki wa Nyanda za Juu Kusini! Tumeshuhudia ngoma kali, hits zinazopendwa sana, na vip...
05/12/2025

Mwaka huu 2025 umekuwa mzuri kwa muziki wa Nyanda za Juu Kusini! Tumeshuhudia ngoma kali, hits zinazopendwa sana, na vipaji vipya vikionekana kila kona.

Hawa ni baadhi ya wasanii waliotawala game mwaka huu, kwa mujibu wa Nyimbo ambazo watu waliomba kwenye Kipindi cha Kutoka Home na pia nyota zinazotarajiwa kuendelea kuang’ara mwaka 2026.

Namba 1.
Namba 2.
Namba 3.
Namba 4.
Namba 5.
Namba 6.
Namba 7.
Namba 8.
Namba 9.
Namba 10.
Namba 11.
Namba 12.
Namba 13.
Namba 14.
Namba 15.
Namba 16.
Namba 17.
Namba 18.
Namba 19.
Namba 20.

Kati ya hawa, nani kakukosha zaidi mwaka huu 2025 tukiwa tumebakiza siku 26 kumaliza mwaka?

cc:

🎨


05/12/2025

Mahak**a Kuu Kanda ya Iringa imeanza maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwake, ikiweka msisitizo katika kutoa elimu kwa umma kuhusu historia, mafanikio na maboresho ya utoaji haki kwa kipindi cha miongo miwili. Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni “Safari ya Miaka 20 ya Mahak**a Kuu.”

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jaji Mfawidhi, Mhe. Dustan Ndunguru, amesema maadhimisho hayo yamelenga kuelimisha wananchi na kujitathmini ili kuboresha zaidi mifumo ya utoaji haki, hasa kupitia matumizi ya TEHAMA. Amevitaka vyombo vya habari kuendeleza ushirikiano na Mahak**a ili jamii ipate taarifa sahihi kuhusu shughuli za kimahak**a.

Kabla ya kilele cha maadhimisho tarehe 15 Desemba 2025, kutafanyika shughuli mbalimbali ikiwemo Wiki ya Sheria (8–12 Desemba) ambako elimu itatolewa kupitia redio na televisheni kuhusu mada k**a huduma za mahak**a, mirathi, wasia, uasili, migogoro ya ardhi, ukatili wa kijinsia, mashauri ya ndoa, matumizi ya TEHAMA na haki za mtoto.

Tarehe 12 Desemba kutafanyika mdahalo wa kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Katoliki Ruaha (RUCU), ukifuatiwa na matembezi ya maadhimisho tarehe 13 Desemba.

Kilele cha maadhimisho hayo kitapangwa kufanyika 15 Desemba 2025.

cc:
📸✍



Wazazi na Walezi Halmashauri ya Mji wa Mafinga Mkoani Iringa wametakiwa kuwalinda Watoto wao kipindi cha likizo ya mwish...
05/12/2025

Wazazi na Walezi Halmashauri ya Mji wa Mafinga Mkoani Iringa wametakiwa kuwalinda Watoto wao kipindi cha likizo ya mwisho wa mwaka 2025 baada ya Shule kufungwa ili kuwakinga na matukio ya ukatili. 

Hayo yamezungumzwa katika  mkutano wa Wazazi wa Wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Msingi Mafinga na Afisa wa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Mji Mafinga Nuru Kwayi, na kuongeza kuwa Wazazi wanatakiwa kuweka Ulinzi na Usalama kwa Watoto wao kipindi chote cha mapumziko. 

Aidha amewataka wazazi kuanza kufanya maandalizi ya kuwanunulia watoto wao mahitaji mazuri ya shule ili na wao wawe katika saikolojia nzuri sambamba kuzingatia lishe bora dhidi yaio.

Aidha amewataka Wazazi kuacha tabia ya kuwaruhusu Watoto kuangalia televisheni au kuachiwa simu zao za mkononi ili kuwaepusha na matumizi mabaya ya mtandaoni.

"Lakini Wazazi ugomvi wenu na Lugha zisizo za staha msizionyeshe kwa mbele ya Watoto mnawafundisha tabia za hovyo" Alisema Kwayi.

Kwa Upande wake Afisa wa Dawati la Jinsia na Watoto wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Mufindi Bi. Mary Kailo, amewataka Wazazi kuhakikisha Watoto wao wanapata nafasi ya kucheza na siyo kuwafungia ndani kwani hupelekea kuwehuka pale wanapopata nafasi ya kucheza na wenzao.
 
Awali Mwenyekiti wa Wazazi wa Shule ya Msingi  Mafinga Bi. Sifa Gerana amesema tabia ya baadhi ya Wazazi kutopeleka chakula Shuleni ili hali wao wanaishi na kula vizuri na kushiriki shughuli za Sherehe za Harusi na zinginezo ni ukiukwaji wa haki za Watoto.


Sisi tupo tayari😎je wewe upo tayari.
05/12/2025

Sisi tupo tayari😎
je wewe upo tayari.




Savana lounge & Night club wanakuletea usiku wa ally choki na iringa music band siku ya ijumaa kuanzia 4 usiku mpka asub...
05/12/2025

Savana lounge & Night club wanakuletea usiku wa ally choki na iringa music band siku ya ijumaa kuanzia 4 usiku mpka asubuhi hakuna kiingilio.


Address

Benbelastreet Gangilonga
Iringa
255

Telephone

+255717667442

Website

https://www.youtube.com/@NURUTV-gz6ou

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when NURU FM Iringa 88.9 posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to NURU FM Iringa 88.9:

Share

Category