14/12/2025
Project ya Chelsea ni project tofauti kuliko project zote mlizowai kuziona kwenye soka....ni k**a project ya Ajax sema hii ina malengo makubwa zaidi ya kuuza wachezaji!
Arsene Wenger alikuwa na project k**a hii ila yeye aliifanya kwa shida sababu timu haikuwa na pesa mara baada ya kuhama kutoka Highbury na kwenda Emirates. Na kipindi kile k**a mnakumbuka vizuri waandishi walianza kumuibulia maneno kwamba anatumika na taifa la kwao Ufaransa kuwakuza wachezaji wa kifaransa tu.
Ili uielewe project ya Chelsea usiifananishe na timu yeyote, isome, uielewe, kisha uchague wewe ukubaliane nayo au uikatae ila usiifananishe au kuilinganisha na timu yeyote coz ni project mpya ndiyo maana Uingereza huko wanaumiza kichwa kupingana na mbinu wanazozitumia matajiri wa Chelsea haswa kwa kutoa mikataba ya mpaka miaka 9 jambo ambalo halikuwai kutokea huko nyuma.