
27/08/2025
Kisukari cha Mimba ni nini?
Ni aina ya kisukari kinachotokea kwa wanawake wakati wa ujauzito, hata k**a kabla hawakuwa na kisukari. Hutokea kwa sababu homoni za ujauzito huathiri namna mwili unavyotumia insulini na kufanya sukari kubaki nyingi kwenye damu.
Mara nyingi hakuna dalili wazi, lakini wakati mwingine mama mjamzito anaweza kupata:
*Kiu ya mara kwa mara
*Kukojoa mara nyingi zaidi ya kawaida
*Uchovu mwingi
*Kiwango cha sukari kubainika juu kwenye vipimo
Madhara yanayoweza kutokea kwa kwa mama Mjamzito mwenye kisukari na mtoto wake Tumboni ni k**a ifiatavyoπ
Mama: shinikizo la juu la damu, kujifungua kwa upasuaji (C-section), hatari ya kupata kisukari baadaye.
Mtoto: kuzaliwa mkubwa kupita kiasi, matatizo ya kupumua, sukari kushuka mara tu baada ya kuzaliwa
Namna ya kudhibiti
Kula chakula chenye uwiano mzuri (epuka sukari nyingi na vyakula vya mafuta kupita kiasi).
Fanya mazoezi mepesi ya mara kwa mara (k**a kutembea).
Kufanya vipimo vya sukari mara kwa mara k**a daktari alivyoshauri.
kwa maswali yeyote tufate DM tutakujibu haraka sana