Karatu Online TV

Karatu Online TV The Official
We shoot • We edit • We Publish • Documentary Karatu Tv

05/06/2026

KARATU, ARUSHA
Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo amewataka wananchi wa Wilaya ya Karatu kuthamini na kulinda amani na utulivu wa nchi, akisisitiza kuwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii hayawezi kupatikana bila kuwepo kwa mazingira ya amani.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Karatu, kiongozi huyo alisema kuwa utulivu ndio msingi wa shughuli mbalimbali za uzalishaji na utoaji huduma, akibainisha kuwa bila amani hakuna biashara, hakuna kilimo, hakuna utalii, wala shughuli za usafiri k**a bodaboda na bajaji zinazoweza kufanyika kwa ufanisi.
Aidha, aliwataka wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kudumisha umoja, mshik**ano na usalama wa maeneo yao ili kuwezesha maendeleo endelevu na ustawi wa jamii.
"Bila utulivu hakuna biashara, hakuna kulima, hakuna utalii, hakuna kuendesha bodaboda wala bajaji. Amani ni nguzo muhimu ya maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla," alisisitiza.
Mkutano huo ni sehemu ya ziara ya viongozi wa chama na Serikali ya kukutana na wananchi, kusikiliza kero zao na kueleza utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

29/05/2026

Mhe. Cecilia Paresso Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha, ameendelea kuwawakilisha wananchi wa Mkoa wa Arusha hasa wanawake na vijana kuhusu fursa ya Mkopo ya Shilingi Bilioni 200 iliyotolewa na Mheshimiwa Rais.

29 May 2026
Bungeni
Jijini Dodoma.

23/05/2026

_VIDEO HIGHLIGHT:_

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza na kutatua changamoto za wananchi wa Manispaa ya Iringa katika viwanja vya Kichangani mkoani Iringa leo Jumamosi, Mei 23, 2026.

POLISI WAREJESHA TABASAMU KWA WATOTO WA K**E WENYE UHITAJI KARATUMkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha, SSP Georgina Matagi am...
21/05/2026

POLISI WAREJESHA TABASAMU KWA WATOTO WA K**E WENYE UHITAJI KARATU
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha, SSP Georgina Matagi ameendelea kuonyesha moyo wa kujali jamii baada ya kutoa msaada wa taulo za k**e kwa wanafunzi wa k**e wanaoishi katika mazingira magumu kupitia shirika la Food for His Children lililopo wilayani Karatu.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Mei 19, 2026, SSP. Georgina Matagi amesema kuwa katika utekelezaji wa majukumu yake amekuwa akikutana na watoto wa k**e wanaokosa mahitaji muhimu ya kiafya, hususan taulo za k**e, hali inayosababisha baadhi yao kushindwa kuhudhuria masomo vizuri, kupoteza kujiamini na hata kuathirika kiafya.
Amesema changamoto hiyo ndiyo iliyomgusa na kumfanya aamue kushirikiana na shirika hilo ili kusaidia kurejesha matumaini kwa watoto hao na kuwapa nafasi ya kusoma katika mazingira salama na yenye heshima.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kimkakati wa Food for His Children, Honorina Honorati amemshukuru Mkuu huyo wa Polisi kwa moyo wake wa kujitolea na kuonyesha upendo kwa jamii, akieleza kuwa msaada huo utawezesha kuwafikia watoto wengi zaidi wenye uhitaji.
Ameongeza kuwa shirika hilo linaendelea na juhudi za kuwasaidia wasichana waliopo katika mazingira magumu ili kuhakikisha hawakosi haki yao ya elimu kutokana na changamoto za maisha.
Kwa sasa, lengo la kuwafikia wasichana 1,592 linaendelea ambapo hadi sasa wasichana 908 tayari wamepata msaada huo, huku juhudi zaidi za wadau na wasamaria wema zikiendelea kuhitajika ili kuwafikia waliobaki.
Shirika la Food for His Children linaendelea kujihusisha na shughuli mbalimbali za kuinua maisha ya familia zenye uhitaji pamoja na kusaidia watoto wa k**e kupata mahitaji muhimu kwa ajili ya afya, elimu na ustawi wao.

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba akisalimiana na Rais wa Kenya Dkt. William Ruto wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano...
12/05/2026

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba akisalimiana na Rais wa Kenya Dkt. William Ruto wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Ushirikiano kati ya Afrika na Ufaransa (Africa Forward Summit: Africa-France Perternship for Innovation and Growth) unaofanyika jijini Nairobi Kenya, leo Mei 12, 2026.Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu amemuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo

07/05/2026

DC KARATU AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUTOA GARI MAALUMU LA WINCHI... Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Lameck Karanga, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa gari maalumu lenye winchi kwa ajili ya Shirika la Umeme Wilaya ya Karatu. Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Wilaya hiyo, Mhe. Karanga amesema ujio wa gari hilo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma za umeme, hususan katika shughuli za matengenezo ya miundombinu pamoja na uokoaji wa vifaa katika maeneo yenye changamoto. Ameeleza kuwa gari hilo litachangia kuongeza ufanisi wa kazi za shirika hilo, hivyo kupunguza muda wa kukatika kwa huduma ya umeme na kuboresha upatikanaji wake kwa wananchi pamoja na wafanyabiashara wa Karatu.
Aidha, Mhe. Karanga amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia inaendelea kuonyesha dhamira ya dhati katika kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi nchini. Pia ameahidi kuwa usimamizi wa rasilimali hiyo utafanyika kwa umakini ili iweze kuwanufaisha wananchi wa Karatu kwa muda mrefu.

Kila juhudi ina thamani 💪Heri ya Siku ya Wafanyakazi – endelea kung’ara katika kile unachofanya! ✨
01/05/2026

Kila juhudi ina thamani 💪
Heri ya Siku ya Wafanyakazi – endelea kung’ara katika kile unachofanya! ✨

29/04/2026

MHE. GIDO AIBANA WIZARA YA MAJI BUNGENI DODOMA

Leo tarehe 29 Aprili, 2026, Mhe. Marirta Gido Kivunge amesimama imara Bungeni Dodoma na kuibana Wizara ya Maji kuhusu kukamilika kwa miradi ya maji Wizara ya Maji kuhusu kukamilika kwa miradi ya maji iliyokwama mkoani Arusha.

Mhe. Marirta amehoji juu ya Utoaji wa fedha za dharura kwa miradi ya Sepeko, Meserani (Longido na Monduli) na mradi wa Maji ya Chai - Kikatiti (Arumeru). Pia Mpango wa kutoa mitambo ya kisasa ya kuchimba visima na mabwawa kwa Halmashauri za wilaya kame za Monduli, Longido, na Ngorongoro ili kutatua kero ya maji kwa wananchi na wafugaji.
Sisi ni sauti ya wananchi, hatulali mpaka kero ya maji iishe.

29/04/2026

Mhe Cecilia Paresso (Mb) na Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametaka kujua lini Serikali itachimba visima vya maji safi kwa Wananchi wa Vijiji vya Upper kitete na Slahhamo katika kata ya Mbulumbulu wilayani Karatu.

29/April 2026,
Bungeni,
Jijini Dodoma.

Kamati ya Fedha Uchumi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri na Diwani w...
23/04/2026

Kamati ya Fedha Uchumi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri na Diwani wa Kata ya Mbulumbulu Mhe. Englibert Qorro imetembelea na Kukagua Miradi ya maendeleo Katika Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.

Address

Karatu

Opening Hours

Monday 09:00 - 16:00
Tuesday 09:00 - 16:00
Wednesday 09:00 - 16:00
Thursday 09:00 - 16:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 12:00
Sunday 09:00 - 12:00

Telephone

+255673941419

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Karatu Online TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Karatu Online TV:

Share

Category