Monfm TZ

Monfm TZ Radio station that produces programs that educate and entertaining community

Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Joseph Sinde Warioba, amesema Serikali inapaswa kukubali makosa yaliyotokea Oktoba 29, ak...
23/12/2025

Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Joseph Sinde Warioba, amesema Serikali inapaswa kukubali makosa yaliyotokea Oktoba 29, akisisitiza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kulinda haki, amani na kuimarisha imani ya wananchi kwa Serikali.

Warioba ameyasema hayo alipofanya mazungumzo na moja ya chombo cha habari hapa nchini, ambapo amesema kuwa kukiri na kurekebisha makosa si dalili ya udhaifu, bali ni ishara ya uwajibikaji na uongozi unaojali maslahi ya Taifa kwa ujumla.

Aidha, amesisitiza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinapaswa kubaki huru, vikitekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, haki na usalama wa wananchi bila kuingiliwa na shinikizo la kisiasa.
100.5Kasulu


Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeongeza treni moja ya abiria kuelekea mikoa ya Kaskazini ili kupunguza msongamano wa w...
23/12/2025

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeongeza treni moja ya abiria kuelekea mikoa ya Kaskazini ili kupunguza msongamano wa wasafiri unaojitokeza kipindi cha sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

Hatua hiyo imechukuliwa kutokana na ongezeko kubwa la wasafiri kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya Kilimanjaro na Arusha, hali ambayo imekuwa ikisababisha baadhi ya abiria kukosa usafiri au kulazimika kulala vituoni kutokana na uhaba wa vyombo vya usafiri.

Akizungumza kuhusu maandalizi hayo, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa TRC, Fredy Mwanjala amesema treni za MGR kwenda Arusha na Moshi ambazo kawaida husafiri kila Jumatatu na Ijumaa, sasa zimeongezewa safari ya ziada itakayokuwa ikiondoka kila Jumamosi kuanzia sasa hadi Januari 2026.

Amesema lengo la kuongeza treni hiyo ni kuhakikisha TRC inawahudumia ipasavyo Watanzania wanaosafiri kusherehekea sikukuu, wakiwemo watumishi wa umma na wanafunzi wanaokwenda na kurejea kutoka likizo za mwisho wa mwaka.

Kwa upande wa mikoa ya kati, Mwanjala amesema TRC itaongeza mabehewa kutoka 16 hadi 20 katika safari za Dar es SalaamKigoma baada ya kukarabati mabehewa manne, hatua inayolenga kukidhi ongezeko la abiria kipindi cha Krismasi na Mwaka Mpya.

100.5kasulu


Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Hamad Masauni, amesema Muungano wa Tanzania unaendelea kukabiliwa na ch...
23/12/2025

Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Hamad Masauni, amesema Muungano wa Tanzania unaendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali, akionya kuwa iwapo vijana hawatapewa elimu sahihi kuhusu misingi ya Muungano huo, upo hatarini kuvunjika.

Akizungumza Leo Desemba 23,2025 wakati akifungua kikao na Wahariri wa Vyombo vya Habari, kikiwa na mada: 'Wajibu wa vyombo vya Habari katika Kulinda na Kuendeleza Muungano', Masauni amesema kuwa kumekuwepo na mitazamo potofu inayojengwa hasa miongoni mwa vijana, hali inayochochea mgawanyiko usio na msingi.

Tunakoelekea vijana hawa tusipowaeleza ukweli watatuzidi kimo. Imefikia mahala tunagawana kwa vitu wale wamepata hiki, wale kile. Wanashindwa kuelewa kuwa hatukuungana kwa vitu; Mzanzibari au Mtanzania Bara akipata fursa, tatizo ni nini? amesema Masauni.

Amesema Muungano umeendelea kuwa nguzo ya amani, mshik**ano na utulivu wa Taifa, licha ya kuwepo kwa baadhi ya watu wanaoubeza bila kuelewa madhara yake.

Kuna nchi zilikuwa kwenye muungano lakini baada ya kuvunjika zilitumbukia kwenye machafuko. Mifano ipo hapa Afrika, ikiwemo Sudan na Sudan Kusini; walikuwa na amani lakini baada ya kutengana mambo yalibadilika,
amesema

.5Kasulu


Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars inashuka dimbani usiku wa leo Jumanne kutupa karata yake ya kwanza ya michuano ya ...
23/12/2025

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars inashuka dimbani usiku wa leo Jumanne kutupa karata yake ya kwanza ya michuano ya AFCON 2025 ikivaana na Nigeria.

Mechi hiyo itakapigwa kuanzia saa 2:30 usiku kwa saa za Tanzania kwenye Uwanja wa Fez uliopo Mji wa Fez, Morocco ikiwa mara ya pili kwa timu hizo kukutana katika AFCON baada ya kupita takribani miaka 45.

Mara ya kwanza timu hizo zilikutana AFCON 1980 iliyofanyika Nigeria, wenyeji walipofungua kampeni kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Tanzania mjini Lagos Machi 8, 1980 kabla ya timu hiyo kwenda kubeba ubingwa wao wa kwanza wa michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Kwa ujumla timu hizo zimekutana mara saba katika michuano tofauti, huku Nigeria ikiwa haijapoteza, ikishinda mechi nne na sare tatu, imefunga mabao 11 na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara tatu.

100.5kasulu


Mamlaka nchini Nigeria zimetangaza kufanikiwa kuwaokoa wanafunzi 130 waliotekwa nyara na watu wenye silaha kutoka shule ...
22/12/2025

Mamlaka nchini Nigeria zimetangaza kufanikiwa kuwaokoa wanafunzi 130 waliotekwa nyara na watu wenye silaha kutoka shule ya Kikatoliki ya St. Marys, iliyopo kaskazini mwa nchi hiyo, mwezi Novemba.

Taarifa hiyo imetolewa na msemaji wa Ikulu ya Nigeria kupitia ujumbe katika mtandao wa X, bila kueleza kwa kina namna operesheni ya kuwaachia wanafunzi hao ilivyotekelezwa.

Kwa mujibu wa afisa huyo, kuachiwa huru kwa wanafunzi hao kunahitimisha zoezi la kuwarejesha nyumbani wanafunzi wote waliotekwa nyara kutoka shule hiyo iliyopo katika jimbo la Niger, kaskazini mwa Nigeria.

Awali, iliripotiwa kuwa zaidi ya wanafunzi 300 walitekwa nyara katika tukio hilo, ambapo takribani wanafunzi 100 waliachiwa huru mapema mwezi huu kabla ya kuachiliwa kwa kundi la mwisho.

.5MHzKasulu


Habari ya Clement Mzize kuikosa Taifa Stars imepokelewa kwa hisia tofauti na wadau wa soka, wengi wakiiona k**a pigo kue...
22/12/2025

Habari ya Clement Mzize kuikosa Taifa Stars imepokelewa kwa hisia tofauti na wadau wa soka, wengi wakiiona k**a pigo kuelekea maandalizi ya fainali za AFCON 2025 kule Morocco.

Mzize, ambaye amekuwa mhimili wa mashambulizi chini ya kocha Miguel Gamondi klabuni Yanga, amejipatia sifa ya kuwa mshambuliaji mwenye kasi na uwezo mkubwa wa kuitanua safu ya ulinzi ya mpinzani, jambo ambalo Taifa Stars italikosa sana.

Kukosekana kwa mshambuliaji huyo chipukizi si tu kunapunguza machaguo ya Kocha Miguel Gamondi katika eneo la ushambuliaji, bali pia kunaondoa ile nguvu ya ziada na kasi inayohitajika katika michuano mikubwa k**a AFCON ambapo wapinzani wana nguvu na kasi.

Huku kukiwa na tegemeo kwa washambuliaji wakongwe k**a Mbwana Samatta na Simon Msuva, pengo la Mzize linaacha pengo la kiuchezaji ambalo linahitaji mbinu mbadala ili kuhakikisha Stars haipotezi makali yake ya kutikisa nyavu.

Kwa wadau wengi, kukosekana kwa Mzize ni mtihani kwa benchi la ufundi la Stars kuonyesha kuwa wanaweza kutengeneza mfumo mshindani utakaobeba matumaini ya Watanzania kule Morocco bila kutegemea kipaji kimoja cha kipekee.

.5MHzKasulu


Dakika 15 kabla ya kipenga cha mwisho, mchezaji aliyetoka benchi Ayoub El Kaabi alifunga bao la kuvutia, akiihakikishia ...
22/12/2025

Dakika 15 kabla ya kipenga cha mwisho, mchezaji aliyetoka benchi Ayoub El Kaabi alifunga bao la kuvutia, akiihakikishia ushindi wa Morocco na kutimiza matarajio ya kabla ya mechi kwa kikosi cha kocha Walid Regragui.

Comoro walilinda goli lao kwa nidhamu kubwa na kuwafanya wenyeji wapate ugumu hadi dakika ya 55, pale Diaz alipoachwa bila ulinzi karibu na eneo la penati na kufunga kwa utulivu akipokea pasi ya chini kutoka kwa Noussair Mazraoui.

Morocco walipata ushindi huo bila kuwa na nahodha wao Achraf Hakimi, ambaye anauguza majeraha ya kifundo cha mguu alipoumia akiichezea Paris St-Germain kwenye Ligi ya Mabingwa mapema Novemba. Pia walimpoteza beki wa kati Romain Saiss, aliyeumia mapema katika mchezo huo.

Alama tatu hizo zinamaanisha Morocco imeongeza rekodi yake ya ushindi wa michezo 19 mfululizo, ingawa mtihani mgumu zaidi unawasubiri watakapokutana na Mali Ijumaa hii.

Leo Jumatatu kuna michezo mitatu inapigwa, ambapo Zambia itakutana na Mali katika mechi ya pili ya Kundi A, huku Misri na Afrika Kusini zikianza kampeni zao katika Kundi B.

100.5MHzkKasulu


Mahak**a Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imeamuru Kampuni ya UDA Rapid Transport Ltd kumlipa fidia ya Sh. milioni...
22/12/2025

Mahak**a Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imeamuru Kampuni ya UDA Rapid Transport Ltd kumlipa fidia ya Sh. milioni 88.8 Frank Zebaza, baada ya kugongwa na basi la mwendokasi, ambapo pia imebainika kuwa Dereva Hafidhi Ally alikuwa akiendesha basi hilo kwa mwendo hatarishi ambaye pia Mahak**a imemuamuru kumlipa Frank fidia ya shilingi Milioni kumi.

Hukumu hiyo ilitolewa Desemba 19, 2025 na Jaji Griffin Mwakapeje, kufuatia kesi ya madai namba 28992 ya mwaka 2024 iliyofunguliwa na Zebaza dhidi ya UDA Rapid Transport Ltd, dereva Hafidhi Ally, Shirika la Taifa la Bima (NIC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), akidai fidia ya jumla ya Sh. milioni 600 kwa madhara aliyopata.

Katika madai yake, Zebaza aliomba alipwe Sh. milioni 350 k**a fidia maalumu kwa gharama za matibabu na matumizi mengine yanayohusiana na ajali hiyo, Sh. milioni 150 k**a fidia ya jumla kwa maumivu na mateso pamoja na Sh. milioni 100 k**a fidia ya adhabu.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Mwakapeje alisema ushahidi uliowasilishwa mahak**ani unaonesha wazi kuwa mlalamikaji alipata majeraha makubwa yaliyomlazimu kufanyiwa upasuaji mkubwa na hadi sasa anaendelea kukumbwa na athari za kudumu katika mfumo wa fahamu na hisia, hali iliyosababisha kupungua kwa uwezo wake wa kufanya kazi.

100.5MHzKasulu

2025

Timu ya Simba SC imemtambulisha kocha wake mpya Steve Barker atakayenoa kikosi Cha wanamsimbazi kuanzia sasa.Kocha huyo ...
19/12/2025

Timu ya Simba SC imemtambulisha kocha wake mpya Steve Barker atakayenoa kikosi Cha wanamsimbazi kuanzia sasa.

Kocha huyo ametambulishwa jioni ya Leo December 19,2025 kurithi mikoba iliyoachwa na kocha aliyekuwa akiinoa clabu hiyo Pantev kabla ya mkataba wake kuvunjika na kuondoka.

.5MHzKasulu

🎄🎁🎅

Wanamgambo wa kikosi cha RSF ambao wamekuwa vitani na jeshi la serikali kwa muda wa miaka miwili na nusu, walisababisha ...
19/12/2025

Wanamgambo wa kikosi cha RSF ambao wamekuwa vitani na jeshi la serikali kwa muda wa miaka miwili na nusu, walisababisha vifo vya zaidi ya watu 1,000 wakati wa mashambulizi ya siku tatu waliyoyafanya mwezi Aprili.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu OHCHR imeeleza katika ripoti yake kwamba "ilirekodi mauaji ya raia 1,013 wakati wa mashambulizi ya RSF kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya Zamzam kati ya Aprili 11 na 13."
Ripoti hiyo imeongeza kuwa zaidi ya wakimbizi 400,000 waliokuweko kwenye kambi hiyo walilazimika kukimbia wakati wa mashambulizi hayo ya siku tatu.
Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, mapigano kati ya jeshi la serikali na wanamgambo wa RSF yamesababisha takriban watu milioni 12 kuyahama makaazi yao nchini Sudan huku maelfu ya wengine wakikabiliwa na kitisho cha njaa.

.5MHzkasulu

🎄🎁🎅

Mkazi wa Arusha, Arafa Yusuph Matoke mwenye umri wa miaka 74 amepata mafunzo ya Sanaa ya Upishi katika Chuo cha Ufundi S...
19/12/2025

Mkazi wa Arusha, Arafa Yusuph Matoke mwenye umri wa miaka 74 amepata mafunzo ya Sanaa ya Upishi katika Chuo cha Ufundi Stadi (Veta) cha Hoteli na Utalii kwa kipindi cha miezi mitatu.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Hussein Mohamed Omar, amemkabidhi Afara cheti cha kuwa mwanafunzi bora katika mahafali ya 13 ya chuo hicho, yaliyofanyika jana Alhamisi, Desemba 18, 2025.

Arafa ni miongoni mwa wahitimu waliopata ujuzi kupitia mpango maalumu wa kuwajengea ujuzi na maarifa kwenye vyuo vya ufundi vya Veta unaojulikana k**a mwanamke na samia, ambao umewahusisha zaidi ya wanawake 16,000 kote nchini.

Mwanzoni nilisita kujiunga na mafunzo ya muda mfupi kwa sababu nilijua sitaweza kulingana na umri wangu, lakini baada ya kuanza na wenzagu 60 walimu walinitia moyo darasani tulitumia mwezi mmoja na muda uliobaki mafunzo kwa vitendo jikoni ambako nilifanya vizuri, sasa ninaomba kazi za upishi kwenye shughuli mbalimbali, alisema Arafa.

Katika hotuba yake Dk Omar alimpongeza Bi. Arafa kwa ujasiri wake licha ya umri wake kuwa chachu kwa wengine kutumia fursa hiyo kupata ujuzi na maarifa yatakayoweza kufungua milango ya ajira na kujiajiri.

.5MHzKasulu


Address

Murusi Street
Kasulu

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Monfm TZ posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category