Jelwa255

Jelwa255 Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Jelwa255, Publisher, Kibaha.

Brother
01/01/2022

Brother

06/11/2019

LEO ANZA KUTUMIA KANUNI YA 40%
Umeshawahi kufika mahali ukasema “Hapo ndio uwezo wangu umefika mwisho kabisa?”-Yaani unajikubalisha kuwa umefanya kwa juhudi zote na kwa 100% na kila ukitafakari unaona hakuna kitu cha ziada unaweza kufanya?Ulishawahi kupitia hali fulani na ukahisi ndio mwisho wa kila kitu na ukakata tamaa lakini ulifanikiwa kuvuka salama?
Jesse Itzler’s kwenye kitabu chake cha “Living with a SEAL” ameeleza kuhusu kanuni ya 40%.Kanuni hii inasema “Pale unapojiona umefanya kila kitu na hakuna unachoweza kufanya zaidi basi ujue hapo umefanya kwa 40% tu”.
Mwaka 2008 ulifanyika utafiti wa kisayansi kuhusiana na kanuni hii na ikathibitika kuwa kila unapojihisi umechoka,umefika mwisho na hauwezi kuendelea tena;Basi kumbuka hapo ni asilimia arobaini tu ya uwezo wako,bado una uwezo 60% haujautumia.
Kuna watu wengi wanashindwa kufanya mambo makubwa kwa sababu huwa wanaishia kwenye hii asilimia arobaini.Leo jaribu kuangalia kila unachofanya;kila unachosema hauwezi kufanya zaidi,ujue bado una 60% za kufanya zaidi.Hii inamaanisha kila mtu ana nguvu za akiba (reserve tank) ambazo ukikata tamaa mapema utashindwa kuzitumia.
Je,leo ni katika eneo gani la maisha yako ambalo ulifikiria umefika kiwango cha juu/mwisho na unakusudia kufanya zaidi? FUNGUA RESERVE TANK LEO


HAYA NDIO MAAJABU YA WANAWAKE YALIYOWASHINDA HATA WANA FALSAFA KUELEWA(13)....Wanawake ni binadamu wa ajabu sana katika ...
02/11/2019

HAYA NDIO MAAJABU YA WANAWAKE YALIYOWASHINDA HATA WANA FALSAFA KUELEWA(13)....

Wanawake ni binadamu wa ajabu sana katika uso huu wa Dunia yaani hawa watu ni next level, kuwaelewa ni ishu iliyowashinda hata wana falsafa, Newton na uwezo wake wote linapokuja suala la wanawake lazima atoke kapa na (ndio maana haieleweki hata k**a akioa). Manabii na busara zao zote walishindwa kuwaelewa wakaishia kushauri ya kwamba tuishi nao kwa akili. Sasa najiuliza ni jambo gani unaweza fanya bila kutumia akili?, hapa ndipo napata ushahidi kwamba kumbe wanawake walishindikana tangu zama za mwanzo kabisa!. Wanasaikolojia wanasema kuwa k**a utamuoa/kuishi na mwanamke mwenye miaka 25 basi itakuchukua miaka 25 mingine kumuelewa huyo mwanamke angaalau kwa 90% maana hawa kila siku hubadilika na kuwa wapya kimatendo na kifikra.

1.Mwanamke unaweza mnunulia BMW X6 akatoka nayo kwenda kutembea, akiwa njiani akaombwa lift na kijana akampa akipitia sheli hela ya mafuta ikawa haitoshi, yule kijana akaamua kumuongeza ata elfu 20 basi mwanamke huweza kubadili mawazo na kumuona yule kijana ni bora kisa tu kachangia mafuta kuliko wewe uliyenunua BMW X6, mfano akitoka hapo akapitia supermarket kununua bidhaa labda akapungukiwa kiasi mfano anadaiwa elfu 20, na yule kijana akasema hiyo ntalipa mimi basi basi hapo atasahau zile zawadi zote huwa unambebea na hiyo elfu 20 inaweza kumfanya awaze kumtunuku yule kijana penzi.

2.Mwanamke unaweza mpa hela akanunue nyama kilo 5 buchani, mwenye bucha akimuongeza robo tu hilo litamfurahisha kiasi kwamba anaweza kumpa mwenye bucha penzi na akusahau wewe ulieyota hela ya nyama kilo 5.

3.Mwanamke unaweza kumnunulia nguo, weaving, mafuta, perfume na urembo mzuri akavutia ila akipita mtaani akasifiwa na mwanaume kuwa kapendeza inaweza kuwa chanzo cha kumtunuku penzi na akakusahu wewe uliyegharamika na kufanya asifiwe!.

4.Mwanamke unaweza kumpa mimba na ukamhudumia mwanzo mwisho na familia ukalea kwa juhudi zako zote ila siku mkikosana anakwambia niache na watoto wangu, apo ashasahau kuwa wewe ndiye uliyempa mimba na kumlea yeye na watoto!.

5.Mchukue rafiki yako mwende bar, wewe uwe na laki 5 na yeye awe na elfu 30 kisha mkae meza moja na muagize unywaji, wewe agiza soda na yeye aagize bia. halafu baada ya nusu saa iteni warembo utaona wewe na laki 5 yako unapitwa tu ila yeye mwenye slfu 30 anaibuka kidedea kisa kaweza kumudu gharama ya bia, Hao ndio wanawake ndugu!

6.Mwanamke ndiye kiumbe pekee anayeweza kukupenda bila sababu ama kukuchukia bila sababu tofauti na viumbe wengine.

7.Mwanamke ndiye mwigizaji mkubwa ulimwenguni, anaweza kulia kwa furaha na akacheka kwa huzuni, bado hujawajua tu wanawake!

8.Mwanamke akisema ndio humaanisha hapana, na akisema hapana humaanisha ndio, pia anaweza kucheka bila kujua sababu lakini pia anaweza kulia pasipo sababu ya msingi ya kumfanya alie, hivyo chunga sana usijejichanganya!.

9.Mwanamke hupendi vutu vigumu na vyenye hatari mfano wanaume wenye nguvu, mlevi, muhuni (pl***oy), jambazi, mgomvi anayeogopwa hata na wanaume wenzie ila ukimuuliza anakuambia mie napenda kuwa na mwanaume mpole mwenye hofu ya Mungu tifauti na sisi wanaume tunavyopenda vitu vipole na vinyenyekevu na vyenye ukarimu, sasa wewe jifanye kumuamini mwanamke!

10.Jinsi unavyozidi kumpenda na kumthibutishia upendo wa dhati ndivyo unavyozidi kujiweka mbali nayeye, mwanamke hupenda migogoro isiyo na maana, ukijua hili ndoa haitokusumbua. Mwanamke hupendi utulivu kamwe!, usipomchokoa atakuchokoa tuu na usipomuendesha lazima akuendeshe yeye, Hawa viumbe hawana hiyana aisee!.

11.Mwanamke hupendi vitu vikubwa wala vidogo, kiufupi hana chaguo maalumu. Ukimnunulia gari sio garantii ya yeye kutulia nawewe bali anaweza kukusaliti hata na muosha gari wako. Ukimjengea nyumba nzuri na kumuwekea kila kitu sio njia ya kumteka kimahaba kwani anaweza kumtunuku penzi ata mtunza bustani wa nyumba yako.

12.Mwanamke hapendi ukweli, Ukimpa ukweli akija mwenye uongo basi we andika maumivu. Unaweza kuwa na elfu 50 ukamueleza ukweli kuwa "mke wangu leo hali mbaya chukua hii elfu 30,"... akatokea jamaa akamuongopea kuwa "Chukua hii elfu 15 ngoja nimesahau ATM card yangu nyumbani ikifuka saa 10 jioni ntakutumia laki 2 kwenye simu", Usishangae mkeo akakusaliti hata kabla ya hiyo saa 10 na iyo laki 2 asiione katu!.

13.Unamuoa hana ishu akiwa kwao amekaa tu, unaamua kumfungulia biashara hata ya duka unamjazia kila kitu. anatokea mshikaji mmoja kumuunga pale dukani kila siku na kumuachia soda tu na hicho kinakuwa kigezo tosha cha kuona mshikaji anamjali kwa kumuachia ya soda kila siku kuliko wewe uliyemfungulia duka zima na kinachofuata ni usaliti tu.

Yapo mengi mno kuliko hayo ila kwa leo naishia hapo... ukiweza shea kwenye groups zingine.
😂🙌🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽
Wamekuwa viumbe walioshindikana kwa Maana nyingine
😅👀 *Mniache tuu*🏃🏽‍♂

SHARE....

Editor:Jelwa255

https://www.facebook.com/684951608200854/posts/2981303125232346/?app=fbl
30/10/2019

https://www.facebook.com/684951608200854/posts/2981303125232346/?app=fbl

Mtu mmoja aliwahi kusema “No matter how badly someone treats you,Never drop down to their level.Remain calm and stay strong”(Bila kujali mtu atakufanyia kitu cha hovyo cha namna gani usiwalipize kwa kufanya cha hovyo.Uwe mtulivu na endelea kuwa imara).
Uwezo wako wa kukabiliana na MANENO na WATU wanaojaribu KUKUKASIRISHA ni kitu muhimu sana ili kujihakikishia unatimiza malengo yako.
Kila siku kuna watu huja kwako k**a WAJUMBE wa shetani -Kazi yao kubwa ni kukuandamana na maneno ya kuudhi,kukusemea uongo ama kukuchokoza tu kwa kila namna.
Wengi wa watu wa namna huwa na nia kubwa TATU:
Moja ni kukuletea madhara kupitia ulimi wako.Wengi wao wameshazoeleka kusema maneno ya hovyo ila wewe watu hawajazoea kukusikia ukisema maneno ya hovyo.Nia yao kubwa ni USEME na UFANYE k**a wao ili wote muwe kwenye kundi la kudharaulika na upoteze HESHIMA na KUAMINIKA kwako.
Mbili wanataka kukutoa NJE ya mstari wa kufanya mambo muhimu.Wanajitahidi kila wanavyoweza kuhakikisha unatumia muda wao KUWAJIBU zaidi unavyotumia muda wako kufanya mambo ya muhimu.Be Smart!
Tatu wanataka uwe mtu ambaye unaishi kwa KUJITETEA siku zote.Wanataka wakufanye MTUMWA wa kutoa maelezo kila siku ya KUJISAFISHA na KUKANUSHA.Kwa kufanya hivi ina maana nguvu zako nyingi zitaishia kwenye kudeal nao badala ya kufukuzia malengo yako.Be focused!
Kumbuka watu wa namna hii hawataisha kwenye maisha yako.Fanya maamuzi ya kuwa imara na kusonga mbele bila kujali wako wangapi.
Hawa wajumbe umeshawahi kukutana nao?
See You At The Top

Address

Kibaha

Telephone

+255676545707

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jelwa255 posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category