KISIWA cha HABARI

KISIWA cha HABARI Kwa habari za uhakika zenye kuelimisha, kuburudisha na kufurahisha, bila kusahau hadithi zote utazipata hapa kwenye page yako pendwa ya KISIWA cha HABARI.

06/01/2025

YANGA 3-1 TP MAZEMBE

03/01/2025

Kumbe Harmonize Mpaka Mpira Yuko Ona Hapa

22/10/2024

Shabiki Wa Simba Atoa Ya MoyonibSimba Kufungwa Kufungwa Na Yanga

TANZIANDUGU YETU,  RAFIKI YETU MWANAHABARI SELEMAN MKANGARA AMEFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA LEO OKTOBA  21, 2024 KATIKA...
21/10/2024

TANZIA

NDUGU YETU, RAFIKI YETU MWANAHABARI SELEMAN MKANGARA AMEFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA LEO OKTOBA 21, 2024 KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI MIPANGO YA MAZISHI INAFANYIKA NYUMBANI KWAO ENEO LA MIVINJENI UFUNDI, KILWA ROAD.

WIKI MBILI NYUMA HALI YAKE ILIKUWA MBAYA.

INNALILLAH WAYNAHLILLAH RAJIUN.

TANGULIA BROTHER Seleman Mkangara

TUMSHIKE MKONO SELE MKANGARA  Seleman Mkangara NI siku ya Jumanne  jioni Oktoba 8/2024 nimerudi nyumbani kwangu kutoka s...
08/10/2024

TUMSHIKE MKONO SELE MKANGARA Seleman Mkangara

NI siku ya Jumanne jioni Oktoba 8/2024 nimerudi nyumbani kwangu kutoka shamba kwenye shughuli zangu za Kilimo.

Mwili umechoka baada ya kupinda mgongo kutwa nzima kupalilia shamba langu la mihogo huku Kisiju/Mkuranga Mkoani Pwani.

Jambo la kwanza namuagiza mjukuu wangu Bakema aniletee simu janja yangu niliyoiacha kwenye chaji nyumba ya jirani.

Tayari simu imenifikia mkononi na Babu yenu Kionambali M.Kionambali (82) nazama mtandaoni kuangalia yaliyotokea duniani.

Ghafla nakutana na habari ya kushtua ikimuhusu mmoja ya wajukuu zangu wapendwa lakini pia ni rafiki yetu wengi.

Naambiwa Selemani Abasy Mkangara(Sele Mkangara) yupo hoi kitandani akipigania uhai wake.

Afya ya Sele Mkangara imetetereka kwa kiasi kikubwa kutokana na kupigwa na maradhi ya kupooza (stroke).

Mkangara shabiki na seneta wa muda mrefu wa bendi ya Msondo Ngoma 'Baba ya Muziki' yupo kitandani kwa miezi kadhaa sasa.

Mkangara mmoja ya wadau wakubwa wa muziki wa dansi na filamu akiwa pia ni Mwandishi wa Habari Nguli sasa anahitaji msaada wetu mkubwa kuliko nyakati zingine zozote za uhai wake.

Siye marafiki zake licha ya uchache wetu tunao wajibu mkubwa wa kumfanyia jambo ili kuokota uhai wake kwa uwezo wa ALLAH.

Tunaelezwa kuugua ni ibada.Mkangara yupo kwenye ibada nzito yenye kuhitaji msaada wa hali na mali.

Kila mmoja wetu aguswe na kuona namna ya kushirikiana na familia yake ili tuokoe uhai wake kutokana na maradhi ya kupooza yanayomsumbua.

Babu yenu Kionambali Ijumaa hii Inshallah nitakua sehemu ya watakaokwenda kumjulia hali iwe nyumbani kwao au Muhimbili nilipoelezwa kwamba amelazwa.

Naelezwa Mkangara anaugua lakini moja ya mambo anayoyamis ni pamoja na maonesho ya bendi yake pendwa Baba ya Muziki inayojiandaa na bethidei ya miaka 60.

Rafiki zangu maseneta wa Msondo nasi tusiache kumfanyia ibada ya kumjulia hali Mkangara na kumpa msaada kadiri Mungu atakavyoturuzuku.

Ugua Pole Mkangara.

Kionambali M.Kionambali

Kisiju/Mkuranga Mkoani Pwani.

08/10/2024
--------------------------------

Address

Kigamboni

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when KISIWA cha HABARI posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to KISIWA cha HABARI:

Share