Main FM Tanzania

Main FM Tanzania Main FM 91.7 Kigoma - Leading Commercial Radio :: Burudani :: Michezo :: Habari : +255 677 77 55 33

 : NBCPremier LeagueFT' Pamba Jiji 0 🆚 1 Simba Sc🏟️CCM Kirumba 🏆 ⚽Lionel Ateba
22/11/2024

: NBCPremier League

FT' Pamba Jiji 0 🆚 1 Simba Sc
🏟️CCM Kirumba
🏆

⚽Lionel Ateba



Leo hii Ijumaa katika   ya  tutakuwa nae Kocha Mkuu wa  Juma Ramadhan Mgunda.Pamoja na mengine mengi tutakayozungumza na...
22/11/2024

Leo hii Ijumaa katika ya tutakuwa nae Kocha Mkuu wa Juma Ramadhan Mgunda.

Pamoja na mengine mengi tutakayozungumza nae atazungumzia pia mchezo wa kesho kati ya Vs katika Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma.

Tutakuwa live kupitia 91.7 Mhz na online kupitia www.mainfm.co.tz


 : Kikosi cha Simba SC kinachoanza kwenye mchezo dhidi ya Pamba Jiji FC katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
22/11/2024

: Kikosi cha Simba SC kinachoanza kwenye mchezo dhidi ya Pamba Jiji FC katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.


 : Kikosi cha Pamba Jiji FC kinachoanza kwenye mchezo dhidi ya Simba SC katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
22/11/2024

: Kikosi cha Pamba Jiji FC kinachoanza kwenye mchezo dhidi ya Simba SC katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.


Kutoka mjengoni leo tunasherehekea siku ya kuzaliwa ya  mtangazaji na mchambuzi wa soka kutoka hapa mjengoni, ungana nas...
22/11/2024

Kutoka mjengoni leo tunasherehekea siku ya kuzaliwa ya mtangazaji na mchambuzi wa soka kutoka hapa mjengoni, ungana nasi kumtakia heri na baraka kwenye siku yake ya kuzaliwa.

Happy birthday Ismail Tano 🎂

  ya  ⚡ iko kwa hewa muda huu... Weekend yako unaianza ukiwa wapi muda huu na unaisikiliza  ⚡ kutokea wapi?Komenti yako ...
22/11/2024

ya ⚡ iko kwa hewa muda huu... Weekend yako unaianza ukiwa wapi muda huu na unaisikiliza ⚡ kutokea wapi?

Komenti yako tutapita nayo muda huu kupitia 91.7 Mhz Kigoma au www.mainfm.co.tz


 : Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 22, 2024 anamwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa konga...
22/11/2024

: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 22, 2024 anamwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa kongamano la tano ya Maendeleo ya Biashara na Uchumi linalofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hazina jijini Dodoma.

Kongamano hilo linatoa fursa kwa wanafunzi, taasisi za elimu, wataalamu wa sera, wajasiriamali, na wadau kutoka sekta ya umma na binafsi kujadili na kushauri kuhusu masuala yanayohusiana na mazingira ya biashara na uwekezaji.

Pia, Kongamano hilo linatoa fursa ya kutafuta suluhisho la changamoto za taaluma ya biashara na uchumi na kuongeza ufanisi katika mifumo ya biashara na uwekezaji ili kuongeza kasi ya maendeleo ya uchumi na ustawi wa jamii.


 : "Mimi ninaamini mpira utachezwa leo, na mkuu wa mkoa akitembelea sehemu ya mkoa wake iwe uwanjani au amekwenda hospit...
22/11/2024

: "Mimi ninaamini mpira utachezwa leo, na mkuu wa mkoa akitembelea sehemu ya mkoa wake iwe uwanjani au amekwenda hospitali haina maana kwamba ameenda kuwahujumu wagonjwa au wachezaji" - Said Mtanda, Mkuu wa mkoa wa Mwanza

"Mimi nikiwa ofisini kwangu jana nilipata taarifa kuna dalili za uvunjifu wa amani, baadhi ya makomandoo wa Simba Sc wamewahold viongozi wa Pamba Jiji Fc ambao walikuwa uwanjani wakifanya mazoezi kabla ya kuondoka, sasa wamefunga milango yote, wale vijana walipoona watashambuliwa wakaenda juu VIP wakafunga milango...."

"Makomandoo wa Simba sc wakaanza kuvunja vioo vya VIP ya CCM Kirumba, lakini baadae wakaanza kuvunja milango, kwa hiyo wakanipigia mimi, nikampigia Mkurugenzi wa jiji, lakini nikawapigia jeshi la polisi, na nikafikiri ni busara kusogea eneo hilo ili baadae mambo yasije kutangazwa ambayo sio sahihi.... lakini pia kuhakikisha jeshi la polisi linafanya kazi yake kwa weledi"

"Sikuingia uwanjani na wala sikuwa na nia ya kuona mazoezi ya Simba Sc, kwa sababu mimi ndio mgeni rasmi, nina haraka gani ya kuwaona Simba Sc wakati leo nilikuwa na uwezo wa kuiona Simba Sc kwa utulivu kwa dakika 90?" - Said Mtanda, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

"Ahmed Ally amenichafua, na mimi k**a kiongozi siwezi kumchukulia hatua ya kisheria yeyote yule ambaye atanichafua, Hivyo Ahmed Ally nimemsamehe baada ya yote" - Said Mtanda, Mkuu wa mkoa wa Mwanza



"Tumeamka Salama, na tuko salama jicho na fikra zetu ni katika mchezo wa leo kuhakikisha tunachukua alama tatu Insha All...
22/11/2024

"Tumeamka Salama, na tuko salama jicho na fikra zetu ni katika mchezo wa leo kuhakikisha tunachukua alama tatu Insha Allah"

"Wana Simba Mwanza na Kanda ya ziwa, Karibuni sana Kirumba tuipe nguvu Simba yetu"- Ahmed Ally, Afisa Habari Simba SC.


Wakati huu wagombea mbalimbali ngazi za uongozi wa Serikali za mitaa wakiendelea na kampeni kuelekea Uchaguzi wa Serikal...
22/11/2024

Wakati huu wagombea mbalimbali ngazi za uongozi wa Serikali za mitaa wakiendelea na kampeni kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika 27/11/2024, kupitia muda huu tuko na Wasaidizi wa Kisheria kutoka Kituo cha msaada wa Kisheria Mandela Paralegal Organization, Deckas Ezekiel Kirondo na Betrida Buhaga wakitoa Elimu ya Mpiga Kura.

Tusikilize kupitia 91.7 Mhz Kigoma au www.mainfm.co.tz



Magazeti ya leo Novemba 22, 2024.
22/11/2024

Magazeti ya leo Novemba 22, 2024.


 : Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Makongoro Nyerere amewataka Watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muunga...
21/11/2024

: Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Makongoro Nyerere amewataka Watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha na kuchochea ajenda ya nishati safi ya kupikia nchini.

Hayo yamebainishwa leo Novemba 21, 2024 na Mhe. Nyerere mara baada ya uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya REA iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala, Mha. Advera Mwijage.

Amesema, Rais Samia anaendelea kuipeleka ajenda ya nishati safi kimataifa ili kuhakikisha watu wanapika katika mazingira salama kiafya na kimazingira.

Mhe. Nyerere ameongeza kuwa, suala la Nishati Safi ya Kupikia sasa ni ajenda ya kimataifa na wataibeba katika kuelimisha umma kuhusu matumizi salama ya nishati hiyo kwa upana.

Kwa upande wake, Mha. Mwijage amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anapika katika mazingira salama na kwamba hatua hiyo itawezekana kwa kupatikana kwa nishati safi ya kupikia iliyo nafuu inayopatikana na kutumika kwa urahisi.

Ameongeza kuwa, mtoa huduma kampuni ya Taifa Gas Limited atahudumia wilaya zilizopo ndani ya Mkoa wa Rukwa kwa kusambaza mitungi 9,765 kwa bei ya ruzuku mitungi ya gesi ya kilo sita pamoja na vifaa vyake katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji.

Amezitaja wilaya zitakazonufaika kuwa ni pamoja na Wilaya ya Kalambo, Sumbawanga na Nkasi.


Address

Kigoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Main FM Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Main FM Tanzania:

Share

Category