22/12/2025
Mimi ni kijana umri wangu ni miaka 36, ila sijajua k**a huo umri bado ni kijana, nimeoa na tayari nina watoto watatu.
Dada Mimi ni mfanya Biashara, tuna duka Moja ambalo anakaa mke wangu na wafanyakazi wawili, Mimi mara nyingi ni mtu wa kusafiri kufanya Biashara zingine mikoani.
Alhamisi nilipigiwa simu na wateja wakiuniuliza mbona duka limefungwa, hiyo ilikuwa mida ya saa nne asubuhi, nikampigia simu mke wangu Ili nimuulize vipi inakuaje mpaka muda huo hawajafungua, ila simu ikawa haipatikani, nikampigia kijana ambaye ni mfanyakazi wa pale dukani ambaye huwa anasaidiana na mke wangu, kijana akaniambia kuwa mke wangu aliwaambia kuanzia alhamisi mpaka ijumamosi hawafungui, wata fungua jumatatu, kikawaida jumapili huwa duka Langu hatufungui, nilivyo ambiwa hivyo nikashangaa, ikabidi nimpigie mdada wa kazi hapa nyumbani ndo akaniambia mke wangu ameaga anaenda kwenye mkesha atarudi jumamosi, niliishiwa nguvu nikakosa Cha kufanya.
Ilibidi nifanye haraka haraka nirudi dar, ijumaa usiku nikawa nimefika nyumbani sikumkuta mke wangu, nikatulia tu nikawa nimemsubiri Kwa hamu sana aniambie ni kwanini afunge Biashara siku tatu wakati tuna mzigo ambao tume uleta Kwa ajili ya sikukuu hizi,
Dada huwezi amini mke wangu alivyo rudi nyumbani jumamosi mida ya saa tatu asubuhi alifika tu na kufungua geti alivyo niona tu nimekaa kibarazani akaniambia Kwa sauti ya juu anataka talaka tuachane Kwa madai eti MUNGU kamuonyesha Mimi ndo sababu ya yeye kutokufanikiwa, nikamwuliza mafanikio gani anataka? K**a ni gari anatembelea mbili ni yeye aamue atumie lipi, nikashangaa kaingia ndani kachukua begi akaondoka.
Toka jana jumamosi mke wangu kaondoka nyumbani, taarifa za chini naambiwa kaenda kupanga, kaniachia watoto hapa mpaka simuelewi, mtoto huyu mdogo ana mwaka mmoja na miezi miwili na yeye kamuacha.
Najiuliza Nini kimemkuta mke wangu hata sielewi, hatukuwahi hata kukwazana kiasi Cha kufikia kuachana, na kabla ya kwenda mkoani alinishauri yeye mwenyewe tununue kiwanja tujenge kiwanda Cha kufyatua matofali tena akawa ananisisitiza sana kuhusu hicho kitu halafu leo ananiambia Mimi ndo kikwazo kwenye maisha yake.
Nilimpa uhuru wa kutumia pesa ndiyo mana hata gari zote za kutembelea alikuwa anatumia yeye, Mimi siyo mpenzi wa kutembelea gari nikiwa mjini, napendelea pikipiki ila kitu Cha ajabu Leo nakuja Kuambiwa Mimi ndo chanzo Cha yeye kutokufanikiwa, najiuliza ni mafanikio gani anataka!!