Radio JOY 90.5 FM

Radio JOY 90.5 FM Radio JOY 90.5 FM - Kigoma Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutumia mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya...
24/10/2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutumia mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Sikukuu za Kitaifa Sura 35, ameidhinisha tarehe 29 Oktoba, 2025 kuwa siku ya mapumziko.

Uamuzi huo umefanyika kwa madhumuni ya kuwawezesha wananchi wenye sifa stahiki wakiwemo watumishi wa umma na wafanyakazi katika sekta binafsi kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura.

K**a inavyofahamika, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza siku ya Jumatano tarehe 29 Oktoba, 2025 kuwa siku ya kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2025.

24/10/2025

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema ajali ya treni ya SGR iliyotokea katika eneo la Ruvu Mkoani Pwani asubuhi ya leo...
23/10/2025

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema ajali ya treni ya SGR iliyotokea katika eneo la Ruvu Mkoani Pwani asubuhi ya leo Oktoba 23, 2025 wakati ikitokea Jijini Dar es salaam kuelekea Dodoma imesababishwa na hitilafu za kiuendeshaji ambazo zilipelekea mabehewa matatu (3) kuacha njia.

Ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 2:00 asubuhi na hakuna aliyejeruhiwa licha ya hofu iliyowapata abiria wachache kufuatia ajali hiyo.

Taarifa ya TRC imeeleza kuwa timu ya wataalamu ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Uchukuzi, Mkurugenzi Mkuu TRC na vyombo vya usalama na menejimenti ya TRC wanaendelea na uchunguzi wa kina sambamba na kuhakikisha huduma zinarejea kwa haraka.

23/10/2025

Treni ya Mwendokasi (SGR) imeripotiwa kuacha njia yake na kupata ajali katika eneo la Ruvu Mkoani Pwani asubuhi ya leo Oktoba 23, 2025 wakati ikitokea Jijini Dar es salaam kuelekea Dodoma.

Kwa mujibu wa abiria wawili wakati wakizungumza na chombo cha Habari cha Ayo TV wamesema hakuna aliyejeruhiwa licha ya hofu iliyowapata wachache kufuatia ajali hiyo.

“Haijafahamika chanzo ila treni imehama kwenye reli k**a inavyoonekana kwenye video na picha, hatujaambiwa chochote ila kuna Viongozi na Maaskari wameanza kufika hapa sio mbali na hapa Stesheni Ruvu” amesema mmoja wa abiria hao.

Msemaji wa Shirika la Reli (TRC) Fredy Mwanjala amethibitisha kupokea taarifa za ajali hiyo, “tumepokea hizo taarifa za Treni kupata ajali na kwa kuwa ndio kwanza tumezipata kwa sasa Mkurugenzi Mkuu na Katibu Mkuu wa Wizara wote tunaelekea eneo la tukio na tunatoa taarifa baadae baada ya kufanya tathmini ya kina na Wataalamu” amesema.

Kufuatia kifo Cha Mchezaji wa zamani wa Simba Alphonce Modest, klabu ya Simba imetoa salamu za rambirambi kumuenzi mchez...
22/10/2025

Kufuatia kifo Cha Mchezaji wa zamani wa Simba Alphonce Modest, klabu ya Simba imetoa salamu za rambirambi kumuenzi mchezaji huyo.

Taarifa ya klabu hiyo iliyotolewa katika kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii imeonyesha kusikitishwa na taarifa ya kifo hicho.

‎ ‎‎Taarifa ya klabu hiyo imeeleza kuwa

"Uongozi wa klabu ya Simba umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya msiba wa aliyekuwa nyota wetu wa zamani Alphonce Modest kilichotokea jana nyumbani kwao mkoani Kigoma.”

“Modest ambaye alikuwa mlinzi wa kushoto mahiri katika miaka ya 90.” ‎‎”Simba inaungana na Wanamichezo wote kuomboleza msiba huu mzito na tunawaombea kwa Mungu wafiwa kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu". ‎

”Modeste aliyekuwa mlinzi wa kushoto katika miaka ya 90 amefariki Jana mkoani kigoma.”

Taarifa ya klabu hiyo imeeleza. Licha ya kucheza katika klabu ya Simba, Modest pia aliwahi kucheza katika klabu Yanga mwaka 1998 na alikua sehemu ya kikosi kilichoingia hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika (CAFCL) kwa mara ya kwanza aliyejiunga na klabu hiyo akitokea Simba.

Pumzika kwa Amani

22/10/2025

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umetoa msaada wa viti mwendo 11 vyenye thamani ya shilingi milioni 4.5 kwa Shirika ...
22/10/2025

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umetoa msaada wa viti mwendo 11 vyenye thamani ya shilingi milioni 4.5 kwa Shirika la Sauti Yetu Foundation kwa ajili ya kuwagawia watu wenye mahitaji maalum katika Halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma.

Hafla ya ugawaji wa viti mwendo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari Bongwe iliyopo Mjini Kasulu na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali, wawakilishi wa taasisi pamoja na wanufaika wa msaada huo.

Akizungumza katika hafla hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Sauti Yetu Foundation kutoka jijini Dodoma BW. Raphael Mabula amesema msaada huo unalenga kuwawezesha watu wenye mahitaji maalum kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii na kiuchumi ikiwa ni sehemu ya juhudi za kujenga jamii jumuishi isiyomwacha mtu nyuma.

Kaimu Mkurugenzi wa Sauti Yetu Foundation kutoka jijini Dodoma BW. Raphael Mabula, Picha na Hagai Ruyagila

Kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mji Kasulu Mwl, Vumilia Simbeye ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika tukio hilo amelipongeza shirika hilo kwa moyo wao wa huruma na upendo kwa jamii hususan kwa watu wenye mahitaji maalum.

Amewasihi pia wazazi na walezi kutowaficha watoto wao wenye ulemavu majumbani, bali wawape fursa ya kushiriki katika shughuli za kijamii na kupata haki sawa na watoto wengine.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mji Kasulu Mwl, Vumilia Simbeye, Picha na Hagai Ruyagila

Baadhi ya wazazi na walezi wa watoto waliopokea msaada huo akiwemo Amina Bakari wametoa shukrani zao za dhati kwa shirika hilo kuwa msaada huo umewapa matumaini mapya na kuongeza uwezo wa watoto wao kushiriki katika maisha ya kila siku.

Baadhi ya wazazi na walezi wa watoto wenye mahitaji maalum waliopewa viti mwendo wakiwa katika picha na Hagai Ruyagila

Shirika la Sauti Yetu Foundation linaendelea na juhudi zake za kuwasaidia watu wenye uhitaji katika maeneo mbalimbali nchini likilenga kuboresha maisha na kutoa fursa sawa kwa makundi yote ya jamii.

❤️

21/10/2025

Kwa mara ya kwanza, wanafunzi milioni 1.6 wa darasa la nne wanatarajiwa kuanza upimaji wa kitaifa Oktoba 22,23 mwaka huu kwa kuzingatia Sera ya Elimu ya Mwaka 2014 toleo 2023 na mtaala ulioboreshwa.

Wanafunzi hao watafanya mitihani ya masomo sita ambayo ni sayansi yenye hisabati, jiografia na mazingira na upande wa sanaa ni michezo, Kiswahili, Kiingereza na historia ya Tanzania na maadili.

Pia, kutakuwa na uchaguzi wa masomo matatu ambayo ni lugha ya Kichina, Kiarabu na Kifaransa.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktoba 21,2025 na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Profesa Said Mohamed wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Profesa Mohamed amesema katika takwimu hizo wanafunzi watakaofanya upimaji wa lugha ya Kiingereza ni 106,503 sawa na asilimia 6.7, lugha ya Kiswahili milioni 1.475.

Pia, amesema wanafunzi wenye mahitaji maalumu miongoni mwa wanafunzi hao ni 5,750 ambapo kati yao wenye uoni hafifu ni 1,164 na wasioona 111,wenye uziwi ni 1,161 na wenye ulemavu wa akili 1,641 na wenye ulemavu wa viungo 1,673. Profesa Mohamed amesema katika upimaji huo, masomo sita pekee ndiye yatatumika kufanyiwa upimaji baada ya kuchaguliwa na wataalamu.

Mwanaume mmoja aitwaye Nicolas Soares (34) amek**atwa nchini Kenya na kurejeshwa Miami, Marekani, zaidi ya miaka 15 baad...
21/10/2025

Mwanaume mmoja aitwaye Nicolas Soares (34) amek**atwa nchini Kenya na kurejeshwa Miami, Marekani, zaidi ya miaka 15 baada ya tuhuma za kumuua Herbert Caniza nje ya nyumba yake mnamo Septemba 7, 2010. Soares, ambaye wakati huo alikuwa na miaka 19, alidaiwa kwenda kumvamia Caniza kwa nia ya kumuibia pesa na bangi, lakini akampiga risasi kifuani.
Caniza alifariki baadaye hospitalini, Polisi wa Miami wamesema walishirikiana na mashirika ya shirikisho kufanikisha kuk**atwa kwa Soares jijini Nairobi na kumrejesha Florida kujibu mashtaka ya mauaji ya shahada ya pili na wizi wa kutumia silaha.

Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, anatarajiwa kuanza kifungo chake cha miaka mitano gerezani Jumanne, kufuati...
21/10/2025

Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, anatarajiwa kuanza kifungo chake cha miaka mitano gerezani Jumanne, kufuatia hukumu ya kula njama ya kupokea fedha haramu kutoka kwa Rais wa zamani wa Libya, Muammar Gaddafi, kwa ajili ya kampeni yake ya urais mwaka 2007.

Sarkozy, ambaye alikuwa kiongozi wa mrengo wa kulia nchini Ufaransa kati ya mwaka 2007 hadi 2012, alihukumiwa mwishoni mwa mwezi Septemba kwa kosa la kupanga kwa siri upangaji huo wa kifedha haramu. Hata hivyo, amekana makosa hayo na kusema kuwa amekuwa mhanga wa “ukosefu wa haki”, huku tayari akikata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa, Sarkozy atafungwa katika gereza la La Santé lililopo Paris, katika chumba cha upweke cha mita tisa za mraba, ili kumkinga dhidi ya mawasiliano na wafungwa wengine pamoja na uwezekano wa kupigwa picha kwa simu za mkononi zinazodaiwa kuingizwa gerezani kinyume cha sheria.

Katika mahojiano na gazeti la La Tribune Dimanche, Sarkozy alisema kuwa tayari ameshapanga mizigo yake na yuko mtulivu kuelekea kifungo hicho. Aliongeza kuwa anapanga kutumia muda huo kuandika kitabu.

Ijumaa iliyopita, Sarkozy alikutana kwa faragha na Rais Emmanuel Macron katika Ikulu ya Élysée, mkutano uliothibitishwa na chanzo kutoka serikali kuu na kuripotiwa kwa mara ya kwanza na gazeti la Le Figaro.

Sarkozy anakuwa rais wa kwanza wa Ufaransa kufungwa tangu Philippe Pétain, kiongozi wa serikali ya Vichy iliyoshirikiana na Wanazi wakati wa Vita ya Pili ya Dunia.

Address

KIBIRIZI
Kigoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Radio JOY 90.5 FM posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Radio JOY 90.5 FM:

Share