19/04/2026
π° Somo la Pili la Arkad: Kuruhusu βWatoto wa Pesaβ Wafanye Kazi
Baada ya Arkad kuanza kuweka akiba tena na kufuata ushauri wa wataalamu, Algamish alirudi na kumuuliza: βJe, unafanya nini na faida inayotokana na akiba yako?β
Arkad alijibu kuwa alikuwa anaitumia kununua chakula kizuri na nguo za kifahari. Algamish alicheka na kumwambia:
βUnakula watoto wa dhahabu yako! Unategemeaje watazalisha wajukuu ambao watakufanyia kazi?β
Somo: Usile faida (interest/dividends) ya uwekezaji wako mapema mno. Iache iendelee kujizalisha mpaka ufikie hatua ambapo unaweza kula faida kidogo bila kugusa mzizi wa utajiri wako. Hii inaendana na nukuu ya Warren Buffett uliyopenda: kutengeneza pesa ukiwa umelala. ~ .madevu