03/07/2025
NGUVU NA UWEZO HALISI WA MAREKANI NA ISRAEL KATIKA ULIMWENGU
Na:Abdull Najad Faiq
Mwanzoni tuliaminishwa kuwa Marekani ni taifa kubwa kijeshi na lenye nguvu duniani,hii inachagizwa na ukubwa wa bajet ya Ulinzi ya Marekani sambamba kuwa na teknolojia ya hali ya juu katika Ulimwengu
Ila licha ya yote hayo Marekani hutumia mbinu kadhaa ili kudumisha nguvu zake pamoja na ubabe wake
Kwanza Marekani pamoja na Israel ni mataifa ambayo hupigana vita katika ardhi za nchi pinzani ili kuepuka hasara katika nchi zao kwa raia pamoja na miundombinu na mali,ikiwa vitatokea vita ambavyo vitasababisha madhara ndani ya ardhi ya Marekani ama Israel basi ninakuhakikishia Umoja wa Mataifa lazima utachukua hatua za haraka sana ili kumaliza mgogoro huo
Pili,sio Israel wala Marekani ambae anapenda apambane na mpinzani mwenye nguvu za kweli mathalan vita vya Israel dhidi ya Iran,tulizoea falsafa ya Israel kwamba ukiwapiga kidogo wao watakupiga zaidi mara dufu ila hali ilikua ni tofauti kwa Iran hakika tulishuhudia madhara ya uharibifu ya mashambulizi ya Iran dhidi ya Israel yalikua ni makubwa zaid,kitendo cha Trump kuamua kuvimaliza vita ilhali mwanzo aliiambia Iran kuwa isipo jisalimisha ataiacha ipate madhara toka kwa Israel,licha ya usaidizi wote wa ulinzi wa anga wa Marekani,Uingereza na Ufaransa kwa Israel na kuamua kusitisha vita bila ya kutimiza lengo lao la msingi,kuliibua dhana kwamba Israel ilikumbana na mpinzani mkali sana kiasi kwamba ikabidi Wamagharib wasalimu amri
Ilikua ni rahisi kwa Marekani kuivamia kijeshi Iraq ya Sadam Hussein ila Marekani hii super power ilivimbiwa na Korea Kaskazini ya Kiduku,je!mnajua kwanini? Sababu Kiduku alikua na Nyuklia ya kweli ila Sadam hakua na silaha hatari zilikua ni propaganda zilizopikwa na Marekani ili kuhalalisha wake uvamizi
Tatu,kumdhibiti mpinzani pamoja na kumpiga vita vya kiuchumi,Kwa miaka mingi Marekani amekua akitumia mbinu za kuiwekea vikwazo vya kiuchumi nchi iliyo hasimu wake kabla ya kuivamia kijeshi,hili tumelishuhudia kule Iraq,Libya na hata dhidi ya Iran wanatumia mbinu ile ile kuidhoofisha kiuchumi Iran ili kuleta hali ngumu ya maisha ndani ya nchi mwisho kuibua uasi wa wananchi dhidi ya Serikali yao
Udhibiti wa mpinzani pia unafanywa na Marekani kwa kutoa takwa kwa Iran kuachana na mpango wake wa makombora ya masafa marefu ili Iran iweze kuondolewa vikwazo vya kiuchumi na Marekani,hili linafanyika sababu makombora ya masafa marefu ya Iran yanaweza kuleta madhara makubwa kwa mshirika wao Israel ama hata dhidi ya wao Marekani wenyewe,swali la kujiuliza je!ni vita gani hivi visivyo na mlingano? Mbona Marekani hakuna anae muingilia juu ya silaha zake?
Kwahiyo kinacho itwa nguvu kubwa ya Marekani ni uongo sababu k**a wangekua na nguvu zilizo halisi basi wasingekua wakihofia nchi ambazo wanahisi ni maadui zao ziwe na nguvu kijeshi na kiuchumi,lakini daima Marekani imekua ikitumia mbinu ya kuzizoofisha ama kuzilainisha kwanza nchi hizo ndipo wafanye uvamizi wao
Katika vita vyake vingi Marekani alivyo pigana k**a utachunguza basi utagundua kuwa haendi pekeyake bali huenda pamoja na NATO ili nchi zaidi ya 5 wakuchangie pamoja huku wakiwa wamekufunga kamba kwa vikwazo vya kiuchumi
Laiti k**a dunia ingekua ni sawa na yenye haki basi na tujiulize ni nani ambae anaeweza kumuekea masharti Marekani juu ya uzibiti wa silaha anazozalisha ikiwemo mabomu hatari yenye uzito wa tani nyingi ya kupasua miamba pamoja na ndege za kivita?
Je ni nani leo katika Ulimwengu huu anaweza kuiwekea vikwazo ama kuiwajibisha Israel pamoja na Marekani pindipo wakitenda makosa?
Hakika mwisho utagundua kila kitu ni feki katika dunia hii haki itazingatiwa kuwa ni haki kutokana na ni nani inayo mgusa