Dira Digital Tanzania

Dira Digital Tanzania Official page of Dira TV

ARUSHA: Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda jana Alhamisi March 13, 2025, amekutana na kuongea na Balozi wa In...
14/03/2025

ARUSHA: Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda jana Alhamisi March 13, 2025, amekutana na kuongea na Balozi wa India nchini Tanzania Bishwadip Wey, wakikubaliana kukuza na kuimarisha mahusiano ya pande hizo mbili katika kuhakikisha kuwa Wananchi wa Arusha wananufaika na fursa mbalimbali kutoka nchini India.

Katika mazungumzo yao, Makonda na Balozi Wey wamejadiliana na Mkoa wa Arusha kupata fursa ya mambo matano ikiwemo, Kongamano kubwa litakalofanyika Mwezi Mei mwaka huu, ambapo atakuwepo Profesa mashuhuri kutoka nchini Marekani kutoa elimu kuhusu akili mnemba (Artificial Inteligence) kwa Vijana wa Arusha.

Viongozi hao pia katika mazungumzo yao wamekubaliana kuanzisha kilimo cha mitishamba inayotumika katika utengenezaji wa dawa za asili chini ya usimamizi wa Chuo kikuu cha Nelson Mandela, pia wamejadili kuhusu nchi ya India kutoa fursa za ufadhili wa masomo kwa Vijana takribani 1000 watakaokuwa na fursa za kusoma kozi mbalimbali sambamba na ufadhili wa Wapishi 50 watakaoenda kupata mafunzo ya upishi wa vyakula vyenye ladha ya kihindi ili kuvutia watalii kutoka nchini humo watakaokuja Tanzania.

Fursa nyingine iliyopatikana katika mazungumzo ya Makonda na Balozi huyo wa India nchini Tanzania ni pamoja na kuimarisha kilimo cha maembe mkoani Arusha kutokana na uhakika wa soko linalopatikana nchini India, ambapo raia wa nchi hiyo wamekuwa na uhitaji mkubwa wa unga unaotokana na tunda la embe kwaajili ya matumizi mbalimbali.

Mchezaji wa Bayern Munich, Joshua Kimmich amesaini mkataba mrefu wa hadi mwaka wa 2029.
14/03/2025

Mchezaji wa Bayern Munich, Joshua Kimmich amesaini mkataba mrefu wa hadi mwaka wa 2029.

Simba SC leo wanashuka dimbani dhidi ya Dodoma Jiji FC! Ushindi ni muhimu ili kupunguza pengo na Yanga SC, vinginevyo wa...
14/03/2025

Simba SC leo wanashuka dimbani dhidi ya Dodoma Jiji FC! Ushindi ni muhimu ili kupunguza pengo na Yanga SC, vinginevyo wanazidi kuweka mazingira mazuri kwa watani wao kutwaa ubingwa wa NBC Premier League! Je, Wekundu wa Msimbazi watawasha moto au Dodoma Jiji watawashangaza?

Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Othman Masoud Othman na Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu wanadaiwa kuzuiwa kuing...
13/03/2025

Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Othman Masoud Othman na Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu wanadaiwa kuzuiwa kuingia nchini Angola kushiriki mazungumzo ya Jukwaa la Demokrasia Afrika (PAD).

Othman, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwenye msafara wake ameambatana na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Dorothy Semu, Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk Nasra Nassor Omar na maofisa wengine wa chama hicho.

Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo-Zanzibar, Ismail Jussa ameliambia Mwananchi leo Alhamisi Machi 13, 2025 kuwa Othman na msafara wake wamezuiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Luanda jijini Angola.

Tayari ACT Wazalendo imetoa taarifa ya kulaani tukio hilo ililoliita la udhalilishaji wa kiongozi huyo huku k**ati yake ya uongozi ikikutana kwa dharura kujadili suala hilo, ambalo mamlaka za Angola hazijajitokeza kulizungumzia.

Wakati huohuo, Lissu ameandika kwenye ukurasa wake wa X kuwa mamlaka za uhamiaji za Angola zimewazuia na kukataa kuwaruhusu kuingia nchini humo, yeye pamoja na ujumbe wa zaidi ya viongozi wakuu 20 na wawakilishi wa vyama vya siasa kutoka Kusini mwa Afrika.

"Ambao tuliwasili Luanda mapema leo kwa ajili ya mkutano huo wa siku mbili, kundi hili linajumuisha Makamu wa Kwanza wa Rais wa sasa kutoka Tanzania (Othman), Rais wa zamani wa Botswana, Waziri Mkuu wa zamani wa Lesotho, pamoja na viongozi na wajumbe waandamizi kutoka Kenya, Sudan, Tanzania, Afrika Kusini, Namibia, Eswatini, Lesotho, Ujerumani, Marekani, Uganda, DRC, na Msumbiji," Lissu ameeleza katika andiko hilo.

"Waangola na Watanzania ni ndugu wa damu. Tanzania ilimkaribisha Dk Antonio Agostinho Neto na wapiganaji wa MPLA katika miaka ya mwanzo ya harakati zao za uhuru. Tuliisaidia Angola kwa hali na mali wakati wa uvamizi wa kikoloni wa utawala wa kibaguzi wa Afrika Kusini katika Kusini mwa Angola katika miaka ya 1970 na 1980,"ameandika Lissu

TABORA: WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amehimiza wananchi wa Nzega mkoani Tabora kuchangamkia fursa ya umeme kufika kwenye...
13/03/2025

TABORA: WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amehimiza wananchi wa Nzega mkoani Tabora kuchangamkia fursa ya umeme kufika kwenye vijiji na mitaa yote ya wilaya hiyo na kuachana na utumiaji wa kuni na mkaa katika kupikia vyakula.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Machi 13, 2025 wakati wa siku yake ya pili ya ziara mkoani Tabora, akisisitiza kuwa lengo la serikali kupeleka umeme kwenye vijiji vyote nchini ni kuhakikisha kuwa Mazingira yanatunzwa kwa wananchi kuachana na nishati chafu (mkaa na kuni) katika kupikia vyakula pamoja na kudumisha utunzaji wa mazingira kwani kuni na mkaa umekuwa ukiteketeza misitu nchini.

Kulingana na Majaliwa viwango vya bei ya kuunganishiwa umeme huenda ikabadilika, hivyo amewataka kuwa na kasi katika kuipata huduma hiyo ya nishati ya umeme kabla ya viwango hivyo kubadilika.

KAGERA: SERIKALI imetangaza hakuna ugonjwa wa Marburg tena nchini na kuwataka wananchi kuendelea kuwa huru.Waziri wa Afy...
13/03/2025

KAGERA: SERIKALI imetangaza hakuna ugonjwa wa Marburg tena nchini na kuwataka wananchi kuendelea kuwa huru.

Waziri wa Afya, Jenista Mhagama ametoa kauli hiyo leo Machi 13, 2025 wakati akihitimisha shughuli zote zilizohusu mlipuko wa ugonjwa huo ulioikumba Kata ya Ruziba, Wilaya ya Biharamulo Mkoa wa Kagera Januari 16 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu wawili.

Wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wamefanya hafla ya kujipongeza baada ya kutumia siku 54 kuhakikisha hakuna mgonjwa mpya wala vifo kwa kutoa elimu juu ya ugonjwa wa mlipuko na kuhakikisha wahisiwa wote wanaweka karantini Ili kuepusha madhara.

"Nachukua nafasi hii kuutangazia umma wa Watanzania wote na wageni kutoka nje ya nchi kuwa Tanzania ni salama na hakuna tena ugonjwa wa Marburg kwa sasa wananchi wawe huru kufanya shughuli zao bila wasiwasi nawasihi wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kwa kunawa mikono kwa kutumia maji safi na sabuni na vitakasa mikono ili kuendelea kuwa na afya njema na kujiepusha na magonjwa ya mlipuko,” amesema M

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maen...
13/03/2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ) Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC kwa njia ya Mtandao pamoja na viongozi mbalimbali, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 13 Machi, 2025. Mkutano huo pamoja na mambo mengine unajadili hali ya ulinzi na usalama Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

13/03/2025
ZANZIBAR: RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali vu Mwinyi amesema Serikali itaendelea Kui...
13/03/2025

ZANZIBAR: RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali vu Mwinyi amesema Serikali itaendelea Kuimarisha Miundombinu ya Sekta ya Elimu kwani ndio Kipaumbele cha kwanza cha Serikali anayoiongoza.

Dk Mwinyi amesema hayo wakati wa Ufunguzi wa Skuli tatu mpya za Msingi za ghorofa za Chumbuni, Kidichi na Skuli ya Msingi ya Abeid Amani Karume iliyopo Mwera.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Machi 12, 2025 ameweka jiwe la msingi la Mradi wa Upanuzi wa Mtandao wa Majisafi ya Ziwa...
12/03/2025

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Machi 12, 2025 ameweka jiwe la msingi la Mradi wa Upanuzi wa Mtandao wa Majisafi ya Ziwa Victoria kutoka Makomero - Mgongoro, uliopo kijiji cha Mwamayoka, Igunga mkoani Tabora ambao umegharimu shilingi milioni 840.8

Akizungumza baada ya kuzindua mradi huo, ambao unatarajia kuhudumia wananchi 5,402, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali
Inaendelea kusimamia utoaji wa huduma za maji safi na salama nchini ili kuhakikisha hali ya upatikanaji wa maji inawafikia wananchi kwa asilimia 100

“Ndugu zangu wananchi, mradi huu ni matokeo ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi, kuweni na uhakika kwamba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kiongozi anayewajali, anawapenda na anasikiliza changamoto zenu, endeleeni kutekeleza majukumu yenu ipasavyo kwasababu tunaye kiongozi madhubiti”

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa ameiagiza RUWASA kuongeza na kusogeza vituo vya kuchotea maji karibu na wananchi “RUWASA hakikisheni miradi hii inatoa maji wakati wote”

Mradi huo ambao umefi

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasili nchini Barbados kushiriki Mkutano wa Kimataifa k...
12/03/2025

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasili nchini Barbados kushiriki Mkutano wa Kimataifa kuhusu matumizi ya Nishati endelevu utakaofanyika katika jiji la Bridgetown kuanzia tarehe 12 hadi 14 Machi, 2025.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Grantley Adams nchini humo, Dkt. Biteko amepokelewa na Waziri wa Nishati wa Nchi hiyo Mhe. Lisa Cummins pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Cuba na mwakilishi katika eneo la Caribean, Mhe. Humphrey Polepole

Aidha, Dkt. Biteko atashiriki katika majadiliano mbalimbali kuhusu matumizi ya Nishati endelevu kimataifa ikiwemo Nishati safi ya kupikia ambayo ni ajenda muhimu kwa ajili ya kuwakomboa wananchi dhidi ya matumizi ya nishati isiyokuwa safi.

Dkt. Biteko ameongozana na Mshauri wa Rais masuala ya Wanawake, Mhe. Angellah Kairuki, Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar, Mhe. Shaib Hassan Kaduara na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mha. Felichesmi Mramba.

SONGWE Mtu mmoja ameripotiwa kufariki dunia na wengine 33 wamejeruhiwa baada ya gari la abiria aina ya Toyota Coaster le...
12/03/2025

SONGWE Mtu mmoja ameripotiwa kufariki dunia na wengine 33 wamejeruhiwa baada ya gari la abiria aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili T 691 DSM kugongana na Tingatinga (maarufu k**a ‘Kijiko’) lisilokuwa na namba za usajili katika eneo la Nandanga, Halmashauri ya Mji Tunduma, Wilaya ya Momba, barabara Kuu ya Ileje Mpemba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Augustino Senga, amesema ajali hiyo ilitokea Machi 10, 2025, majira ya saa 12:00 mchana, baada ya dereva wa Tingatinga hilo kuendesha kwa kuyumba barabarani hali iliyosababisha kugongana na gari hilo la abiria, mali ya Bobu Mwampashi, ambalo lilikuwa likiendeshwa na Juma Mwafyabo (47).

Kwa mujibu wa Kamanda Senga, marehemu ni Sara Mzopola (37), aliyefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mji wa Tunduma, iliyopo eneo la Mpemba.

“Tunaendelea kumsaka dereva wa Tingatinga ambaye alikimbia baada ya kusababisha ajali hii ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake,” alisema Kamanda Senga.

Alisema awali majeruhi wote 33 wa ajali hiyo walikimbizwa katika Hospitali ya Halmashauru ya Mji Tunduma, ambapo 11 walilazimika kupewa rufaa kwenda Hospitali ya rufaa ya Mkoa kutokana na hali zao kuwa mbaya, huku majeruhi 14 wakiruhusiwa kurejea nyumbani baada ya matibabu.

Aliongeza kuwa, majeruhi wengine nane wanaendelea kupata matibabu katika Hospitali hiyo ya Halmasgaurina kwamba hali zao zinaendelea vizuri.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa (TMO) wa Tunduma, Dkt. Sebastia Siwale, amekiri hospitali hiyo kupokea majeruhi wote 33 na kwamba hivi sasa inaendelea kuwahudumia majeruhi nane tuu.

Address

Kinondoni

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dira Digital Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share