22/07/2025
Nukta Fakti imefanya uchunguzi kwenye chapisho linalosambaa kwenye mitandao ya kijamii hususan Facebok linalosambaza taarifa zinazodai kuwa Mwenyekiti wa zamani wa Chadema, Freeman Mbowe amefutwa uwanachama wa chama hicho na kubaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
Uchunguzi umebaini kuwa chapisho hilo ni feki, halijachapishwa na ITV, halipo kwenye kurasa rasmi za chombo hicho cha habari. Aidha chapisho la Taarifa kwa Umma lililotumika k**a chanzo haijatolewa na Chadema na halipo kwenye kurasa rasmi za chama hicho. Pia aina ya mwandiko (font) uliotumika sio mwandiko unaotumiwa katika machapisho rasmi ya Chadema.
Na Nukta Fakti