11/10/2025
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia Tatuzo Yohana Mzumbwe, mkazi wa Masoko mkoani humo kwa tuhuma za mauaji ya mama yake wa kambo, Mary Yohana (61), kwa kumkata na panga kichwani.
Polisi wamesema mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 6, 2025, majira ya saa 2:00 asubuhi katika Kijiji cha Mapinduzi, Kata ya Masoko, Tarafa ya Isangati.
"Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa kifamilia kuhusu mashamba ambapo mtuhumiwa alikuwa akimshinikiza Mary Yohana kugawa mashamba ya urithi yaliyoachwa baada ya baba yake kufariki," imesema taarifa.
Jeshi la Polisi limesema mtuhumiwa atafikishwa mahak**ani baada ya uchunguzi kukamilika.