MWAI production

MWAI production Content creator and actor

17/09/2025

I accepted 1 fan badge from Gracious Dorcas.

Simulizi: NILIPEMDWA NA JINI BILA KUJUAMwandishi: Mwai ProductionSEHEMU YA TANONakumbuka k**a jana… Nilipokaa kitandani ...
14/09/2025

Simulizi: NILIPEMDWA NA JINI BILA KUJUA
Mwandishi: Mwai Production
SEHEMU YA TANO

Nakumbuka k**a jana… Nilipokaa kitandani nikisikia sauti ya Carolina ikiniamuru safari ya kwenda kwa wazazi wake imefika, nilihisi giza likinimeza. Nilihisi k**a roho yangu imetolewa mwilini. Nilipozinduka, nilikuwa nimesimama juu ya maji ya bahari—ndiyo, juu ya maji yenyewe, si mashua, si daraja—miguu yangu ikikanyaga bahari kana kwamba ni sakafu. Upepo mkali ulivuma, maji yakipiga makelele chini yangu, moyo wangu ukitaka kuruka nje.

Nikainua macho yangu… nikashangaa.

Katirkatika ya bahari kulikuwa na majengo ya kifahari: majumba makubwa, yakimetameta kwa mwanga wa ajabu, k**a almasi zikining’inia juu ya bahari. Niliona watu wakitembea juu ya maji kwa utulivu, kana kwamba hawana uzito. Wengine walicheka, wengine walikula, wengine walicheza. Nilihisi nimepelekwa kwenye dunia nyingine kabisa.

Carolina akaja kando yangu, akashika mkono wangu kwa upole:

“Mwai, karibia. Hapa ndipo kwetu. Huu ndiyo utajiri na fahari ya familia yangu.”

Tulipofika mlangoni mwa jumba kubwa la kifahari, tulipokelewa na wazazi wake. Walikuwa na maumbo ya kibinadamu wa kawaida kabisa, mavazi ya kifahari, tabasamu zao zikitupa ukarimu wa ajabu. Mama yake Carolina akanikumbatia, baba yake akaniambia kwa sauti ya nguvu:

“Karibu, Mwai, mwanangu. Hapa ndiyo nyumbani kwako sasa.”

Nikashangaa, nikawauliza kwa mshangao:

“Lakini… mnawezaje kuishi hapa katikati ya bahari?”

Baba yake Carolina akacheka kidogo, akaniangalia kwa macho ya siri:

“Sisi ni majini. Tunaishi popote tunapotaka—majini, misituni, majabali, hata makaburini. Lakini bahari ndiyo makao yetu salama zaidi. Hapa hakuna mwanadamu anaweza kufika bila ruhusa yetu. Wewe umepewa heshima ya kipekee.”

Nilihisi moyo wangu ukitetemeka. Maneno hayo yalinipa baridi ya mifupa.

Kisha Carolina akaniletea chakula. Meza kubwa ikaja mbele yangu, juu yake likiwa jibao la nyama mbichi, ikichemka damu. Sikutambua ni nyama ya mnyama gani—labda si wa duniani kabisa. Harufu yake ilichanganya mapafu yangu, nikataka kutapika.

Baba yake akaniangalia kwa ukali:

“Hicho ndicho chakula chetu cha kifamilia. Ukila, utaunganishwa nasi. Ukinywa damu hii, utakuwa mmoja wetu. Sasa kula, na kunywa.”

Carolina akaniwekea mbele kikombe kilichojaa damu, ikitikisika ndani yake kana kwamba bado inacheza pumzi ya uhai.

Nilipigwa na msh*tuko. Mikono yangu ikatetemeka. Jasho lilinitoka mwili mzima. Nilijiuliza: Je, nikikataa, watanifanya nini? Moyo wangu ulikuwa k**a unataka kupasuka.

Wakati huo, mbali na huko baharini, Jane alikuwa amefika nyumbani kwake. Chuo kiliona hali yake imezorota mno, kikamruhusu arudi. Wenzake walilia kwa huzuni, wengine wakasema:

“Ni bora akae na familia yake… huku hatuwezi kumsaidia.”

Alipofika, wazazi wake walimkaribisha kwa machozi. Walimwona binti yao mrembo sasa akiwa dhaifu, akitetemeka, akishindwa hata kuzungumza vizuri. Mama yake alimuangalia kwa uchungu, moyo wake ukapasuka vipande vipande.

Usiku huo, mama yake Jane akaingia ndani ya chumba kidogo cha maombi. Akaweka Biblia juu ya meza, akapiga magoti, machozi yakimtiririka.

“Ee Mungu wa mbinguni… nimepoteza nguvu, nimepoteza maneno. Binti yangu anateswa na nguvu za giza. Nakuomba, kwa damu ya Yesu, muokoe Jane wangu. Usiache shetani akashinda!”

Akaanza kufunga, akilia kwa sauti, sauti ya mama ikivunja anga ya usiku.

Na mimi, pale baharini, nilikuwa nimezungukwa na maelfu ya macho ya majini wakinitazama nikishika kikombe cha damu. Walitaka nijisalimishe, niwe wao.

Nilihisi nimefungwa—sauti za Carolina na wazazi wake zikiniambia:

“Kula, kunywa, uwe wetu… au uteseke milele.”

Nikaelewa sasa maisha yangu yalikuwa mateka ya giza.
Sikuwa tena binadamu wa kawaida.

Simulizi: NILIPEMDWA NA JINI BILA KUJUAMwandishi: Mwai ProductionSEHEMU YA NNEJane alianza kudhoofika kila siku. Sasa ha...
13/09/2025

Simulizi: NILIPEMDWA NA JINI BILA KUJUA
Mwandishi: Mwai Production
SEHEMU YA NNE

Jane alianza kudhoofika kila siku. Sasa hakuwa tena yule binti mchangamfu niliyemjua—alikuwa kivuli cha nafsi yake. Wanafunzi chuoni walimwona akitembea kwa sura ya hofu, macho yamevimba kwa machozi, na mara kwa mara akishtuka ghafla na kupiga yowe:

“Carolinaaaa… nisameheeee! Tafadhali usiniueeee!”

Wenzake walipojaribu kumshika, alitetemeka, akijivuta chini akilia, mara nyingine akionekana k**a anaongea na mtu asiyeonekana. Wengine wakaanza kumsema vibaya:

“Jane kapagawa…”
“Amechanganyikiwa, kapotea akili…”

Mara nyingi Jane alikuwa akilia ovyo katikati ya darasa, akilia kwa uchungu, akirudia maneno yale yale:

“Carolina… nisamehe… usinipe adhabu…”

Polepole, kila mtu akamkimbia. Jane aligeuka k**a kichaa—mtu ambaye kila mwanafunzi alimtazama kwa hofu na dharau.

Niliposikia hali yake, moyo wangu uliungua kwa maumivu. Nilihisi lawama nzito: ni mimi niliyemsababisha mateso haya. Niliamua jambo moja—lazima nitafute msaada, hata k**a siamini kanisani. Nilijiambia: “Labda mchungaji atanisaidia. Labda Mungu atanionyesha njia.”

Nilitoka kuelekea kanisani. Barabara ilikuwa kimya, upepo wa usiku ukipuliza majani kwa sauti ya kutisha. Wakati natazama mbele, nilimuona mchungaji—ndiyo, uso wake nilimfahamu vyema, alikuwa yule mchungaji wa jirani aliyezikwa hivi karibuni, lakini sasa alikuwa hai akitembea kwangu.

Nilidondosha mifupa ya hofu, lakini nilijilazimisha kuamini: “Mungu asante, umemfufua mchungaji kwa ajili yangu!”

Nilimkaribia nikamwambia shida zangu zote, nikalia mbele yake k**a mtoto mdogo:

“Mchungaji, nimefungwa na kitu kisichokuwa cha kawaida… Carolina… ni jini. Ameniteka, ameniharibia maisha, anamuua Jane. Tafadhali nisaidie!”

Mchungaji akaniangalia kwa upole, akasema kwa sauti tulivu:

“Usiogope mwanangu. Njoo twende nyumbani kwako nikakuombee, roho zote chafu zitakimbia.”

Nilifurahi. Nikamruhusu aje nyumbani kwangu. Tulipofika, aliniamuru:

“Piga magoti. Fumba macho. Hebu tuanze maombi.”

Nilitii. Niliinama, nikapiga magoti, nikafumba macho. Nilihisi mikono yake ikiweka juu ya kichwa changu. Akanza kuomba, sauti yake ikisomea maneno ya sala. Nilihisi mwanga fulani ukishuka, nikaanza kupata matumaini.

Lakini mara alipomaliza akasema:

“Ameeeniii…”

Nilishtuka, macho yangu yakafunguka kwa nguvu. Nilipoangalia mbele yangu, damu ilinikimbia usoni—haukua mchungaji!

Ilikuwa Carolina!

Uso wake ulikuwa umejaa hasira, macho yake yakiwaka k**a moto wa kuzimu. Akapiga kelele kwa sauti ya radi:

“Nilikuambia Mwai! Popote uendapo mimi nipo! Usithubutu kutafuta msaada—ukirudia tena nitakupa adhabu ambayo hata kaburini hautaisahau!”

Nilitetemeka, nilishindwa hata kupumua.

Wakati huo huo, Jane akiwa hosteli, aliingia bafuni kuoga akidhani pengine maji yangeondoa mawazo mabaya. Alipokuwa akimimina maji mwilini, ghafla akasikia “shhhhh…” k**a sauti ya nyoka. Alipotazama juu ya kuta—vichwa vya nyoka viliibuka pembezoni mwa bafu, vikipepesa ndimi zao zenye sumu.

Akajaribu kukimbia, lakini sakafu ilipasuka—kutoka chini, mikono ya wafu ikaanza kujitokeza, ikipapasa miguu yake, ikimvuta chini. Macho yake yakapanuka, akapiga kelele kubwa:

“Mwaaaaai! Nisaidie! Mwaaaaaai!”

Ndipo damu ikaanza kusambaa sakafuni, maji yakageuka kuwa mekundu. Sauti nzito kutoka kila upande ikasema:

“Unampenda Mwai? Unampenda? Huyo si wako!”

Jane akalia kwa uchungu, akipiga kelele mpaka sauti ikavunja ukimya wa hosteli. Wenzake walikimbia kuangalia nini kinatokea. Walipoingia bafuni—kila kitu kilikuwa kimetoweka. Hakukuwa na nyoka, wala damu, wala mikono ya wafu.

Jane alibaki amesimama, akitetemeka, akawaambia wenzake kwa hofu:

“Mlikuwa mnaona! Walikuwa humu ndani! Nyoka! Mikono ya wafu! Damu! Wote walikuwa humu ndani!”

Lakini wenzake walicheka, wakamwangalia kwa dharau:

“Wewe kichaa. Tulijua tu… akili yako imeharibika.”

Jane akaangua kilio, akashika kichwa chake kwa maumivu, akajua sasa hakuna atakayemwamini tena.

Na mimi… usiku ulipokaribia, nilikaa kitandani nikihisi usingizi unanikimbia. Ndipo sauti nzito ikaja, ikizunguka hewa ya chumba changu, sauti ya Carolina yenye ukali wa radi:

“Mwai… safari yako ya kwenda kwa wazazi wangu imefika. Utaona… hutakimbia.”

Mwili wangu ulitetemeka, na nikajua usiku huo haukuwa wa kawaida.
Ulikuwa mwanzo wa kitu kikubwa zaidi.

Simulizi: NILIPEMDWA NA JINI BILA KUJUAMwandishi: Mwai ProductionSEHEMU YA TATUNakiri kabisa… kuanzia pale, akili yangu ...
12/09/2025

Simulizi: NILIPEMDWA NA JINI BILA KUJUA
Mwandishi: Mwai Production
SEHEMU YA TATU

Nakiri kabisa… kuanzia pale, akili yangu ilianza kuchanganyikiwa. Niliishi k**a mtu aliyekumbatia kifo. Usiku haukuwa tena usingizi, mchana haukuwa tena mwanga. Nilitembea nikiwa roho yangu nje ya mwili. Na usiku ule ndio ulioandika kumbukumbu ya hofu ambayo sitasahau hata kaburini.

Jane alilala chumbani kwake hosteli, lakini usingizi wake haukuwa wa kawaida. Saa za usiku wa manane alijikuta ghafla ameamka akiwa si kitandani kwake… bali makaburini!

Udongo wa baridi ulikuwa umemfunika, na alipoinua kichwa, akagundua yupo juu ya kaburi jipya. Alipopepesa macho kusoma msalaba uliokuwa kichwani pa kaburi lile, damu yake iliganda. Maneno yaliyoandikwa yalichoma moyo wake moja kwa moja:

“JANE HAULE”
Tarehe ya kuzaliwa yake ilikuwa pale, na baada yake, tarehe ya kufa iliandikwa na kufunikwa kwa mstari wa deshiii —

Ndiyo, kifo chake kilikuwa bado hakijaandikwa!

Jane alipiga kelele kali, sauti ikapita katikati ya makaburi, ikitikisa utulivu wa usiku. Aliamka haraka akakimbia, lakini hapo ndipo maajabu ya hofu yalipoanza. Mikono mingi ya wafu ikaanza kujitokeza kutoka makaburini yaliyomzunguka—mikono myeupe, yenye udongo, yenye kucha ndefu na nyufa. Mikono hiyo ikaanza kumshika miguu, ikimvuta chini, taratibu ikimzonga, kana kwamba makaburi yote yalikuwa yanataka kummeza.

Jane akapiga kelele:
“Mwaaaaai! Nisaidieee! Mwaiiii!”

Ndipo giza likatikisika ghafla, na Carolina akajitokeza juu ya jiwe la kaburi, macho yake yakiwa k**a mianga ya moto. Akanena kwa sauti nzito, ikitikisa hewa yote:

“Jane! Nilikuonya. Kaa mbali na Mwai. Huyu si wa kwako, ni wangu! Ukithubutu tena… kaburi hili halitakaa liwe tupu!”

Mikono yote ya wafu ikatoweka ghafla, kana kwamba haikuwahi kuwepo. Jane akajirusha na kukimbia bila hata kuangalia nyuma. Miguu yake ikawa haina mwelekeo, macho yake yakijaa machozi ya hofu, hatimaye akajikuta amerudi hosteli, mwili wake wote ukitetemeka.

Wakati huo, mimi nilikuwa nyumbani kwangu, nikiandaa kikombe cha chai cha maziwa, nikijaribu kutuliza akili. Nilikuwa najidanganya kuwa yote ni ndoto tu. Ghafla, mlango wangu ukafunguka taratibu bila kuguswa.

Carolina akaingia.

Lakini sasa hakuwa yule kiumbe wa nyoka… alikuwa Carolina yule mrembo nilivyomzoea pale chuoni. Akavaa tabasamu la upole, akaja taratibu, na kwa sauti nyororo akasema:

“Mwai… usiogope. Siko hapa kukudhuru. Nakupenda.”

Nilihisi miguu yangu ikikataa kutembea. Nilihisi moyo wangu ukidunda kwa kasi kana kwamba unataka kuruka nje ya kifua changu. Nilihisi k**a natamani kukimbia, lakini miguu yangu ilikuwa mizito kana kwamba imenasa kwenye udongo wa kaburi. Nilishindwa hata kusogea.

Carolina akaja karibu zaidi, macho yake yakibadilika ghafla kutoka kwenye macho ya binadamu hadi ya mnyama—macho mekundu yanayowaka moto. Nilipojaribu kufumba macho, nguvu zikanipotea ghafla, nikajikuta nikiishiwa kabisa na kulala kitandani.

Ndipo jambo baya kabisa likatokea.
Nilijihisi nikibebwa na kiumbe huyo, nikilazwa kitandani, nikashindwa kupinga. Nilihisi mwili wangu ni mzito, akili yangu ikikimbia huku ikilia, lakini mwili wangu ulikuwa mateka. Carolina alinitawala.

Sijui kilidumu kwa muda gani… Lakini nilipozinduka, nilikuta nipo uchi, jasho limenilowesha mwili. Niliangaza pembeni yangu—na pale… kulikuwa na bonge kubwa la Chatu, likiwa limejikunja, macho yake yakinichungulia. Nilishindwa kupiga kelele, pumzi yangu ikakata. Nilipiga yowe kwa nguvu niliyobaki:

“Aaaaahhhhhh! Mungu wangu!”

Lakini mara moja yule Chatu akatoweka mbele ya macho yangu.

Niligeuka ukutani, na ndipo nilipoona kitu kilichonifanya nihisi roho yangu inanitoka—michirizi ya damu ikitiririka ukutani, ikichora mistari kana kwamba kuna mtu alikuwa akiandika maandiko ya laana kwa damu. Harufu ya damu ilijaa chumba kizima.

Nilivaa boxer haraka, nikajirusha kukimbia nje ya nyumba… lakini jambo la ajabu lilitokea. Kila nilipofungua mlango, nikajikuta nimerudi pale pale chumbani kwangu. Nilikimbia mara mbili, mara tatu, mara nne—lakini sikutoka nje. Nilizunguka humo humo, nikikimbia k**a mwendawazimu ndani ya mduara wa giza lisilo na mwisho.

Mwisho wa yote, nguvu zikanishia. Nikaanguka chini, nikakaa sakafuni, nikijishika kichwa huku nikilia. Hofu ya kifo na giza ikanivamia, nikajua sasa Carolina ameniteka kabisa.

Hapo ndipo nilipoelewa… mapenzi ya jini siyo zawadi—ni kifungo cha roho, ni kaburi kabla ya kifo.

Simulizi: NILIPEMDWA NA JINI BILA KUJUAMwandishi: Mwai ProductionSEHEMU YA PILIUsiku mmoja, nililala chumbani kwangu nik...
11/09/2025

Simulizi: NILIPEMDWA NA JINI BILA KUJUA
Mwandishi: Mwai Production
SEHEMU YA PILI

Usiku mmoja, nililala chumbani kwangu nikiwa nimechoka sana, lakini usingizi haukuja kirahisi. Nilijisikia k**a kuna macho fulani yananitazama gizani. Nilipokuwa nikipapasa simu yangu kuwasha mwanga, ghafla nilihisi kitu kizito kikining’inia juu ya kifua changu. Nilipoangalia kwa macho ya hofu—ndiyo nikamuona Carolina.

Lakini si Carolina niliyemfahamu chuoni—
Huyu alikuwa ni kiumbe mwingine.

Mwili wake ulikuwa mrefu na wenye kung’ara k**a ngozi ya nyoka. Nyoka mkubwa mweusi ulikuwa ukijikunja kitandani mwangu, na kichwa chake—ndiyo sura ya Carolina. Macho yake yalikuwa mekundu sana, k**a makaa yaliyowashwa moto, na ulimi wake ulikuwa ukitoa sauti ya kushushua “shhhh… shhhh…” huku ukinigusa shingoni.

Nilitetemeka, midomo yangu ikawa mizito kuzungumza. Nilitaka kupiga kelele lakini sauti ikakataa kutoka.

Kisha akasema kwa sauti nzito, ikisababisha hewa nzima ya chumba kutetemeka:

“Mwai… mimi si mwanadamu. Mimi ni jini. Nimevaa umbo la kibinadamu kukupenda. Popote ulipo, mimi nipo. Unapopumua, mimi nipo. Ukimwangalia Jane… mimi nipo. Ukinisaliti—nitakuonyesha hasira ambazo mwanadamu hawezi kuvumilia.”

Kisha akacheka kwa sauti ya mchanganyiko wa mwanamke na nyoka, kicheko kilichopenya hadi kwenye mifupa yangu. Nilifumba macho kwa nguvu, nikifikiria ni ndoto… lakini nilipofumbua, alitoweka. Nilibaki nimesweat mwili mzima, kitanda kikiwa kimejaa vumbi la ajabu na harufu ya kiberiti.

Siku iliyofuata, Jane alinikimbilia akiwa na hofu. Macho yake yalikuwa mekundu kana kwamba hakulala usiku kucha. Akanishika mkono na kuniambia kwa sauti ya kunong’ona:

“Mwai… jana usiku… nilimuona Carolina. Alinitokea chumbani kwangu. Alikuwa na macho makali… akaniambia nikae mbali na wewe. Alinipa vitisho… alisema nikipigania mapenzi yetu nitakufa kabla ya kuona jua linachomoza mara tatu.”

Nilishtuka sana, miguu yangu ikatetemeka. Jane akalia, machozi yakitiririka usoni mwake. Nilimhisi amepoteza nguvu, nikamkumbatia huku na mimi nikihisi machozi yakinitiririka. Sikuwahi kuwa na hofu kubwa kiasi hiki maishani.

Kuanzia siku hiyo, maisha chuoni yalianza kuwa ya mateso. Nilikuwa naogopa kwenda lecture. Nilikuwa naogopa kukaa kwenye kivuli. Nilipokuwa darasani, mara nikihisi shingo yangu inapapasa kitu baridi, nikigeuka nyuma hakuna mtu. Mara nyingine nikisikiliza lecture, masikioni mwangu hunong’ona sauti ya Carolina:

“Nakutazama… naona kila unachofanya…”

Nilichanganyikiwa kabisa.

Hatimaye mimi na Jane tulikubaliana: tutakwenda kwa mganga wa kienyeji—tumuone mtu mwenye nguvu za jadi, labda atatusaidia. Tulipanga safari kwa siri, tusionekane na yeyote. Tulikubaliana tutakutana usiku, twende kijijini mbali kidogo chuoni, ambako mganga mmoja mashuhuri alipatikana.

Lakini kabla hata hatujafanikisha mipango… Carolina alinijia tena.

Nilikuwa nimekaa peke yangu, nikitafuta dawa za kienyeji mtandaoni kwa wasiwasi. Mara taa zikazimika ghafla, chumba chote kikaingia giza totoro. Baridi kali ikazunguka mwili wangu. Nilihisi pumzi baridi ikinigusa shingoni. Nilipoangalia kioo cha kabati—ndiyo, nikamuona nyuma yangu.

Uso wake ulikuwa umeharibika nusu: upande mmoja Carolina mrembo niliompenda, upande mwingine ulikuwa umejaa mabaka meusi na macho ya mnyama pori.

Akanitazama kupitia kioo, akasema kwa sauti kali:

“Mwai… unataka kwenda kwa mganga? Wewe na Jane? Msithubutu! Mnafikiri kuna nguvu zinazoweza kunitoa kwako? Mimi ndiye mapenzi yako, mimi ndiye pumzi yako, mimi ndiye mwili wako! Ukijaribu kuondoka… nitamchukua Jane mbele ya macho yako na wewe utaishi ukiwa kivuli cha maumivu.”

Nilianguka chini, miguu ikikataa kunibeba. Nilishika kichwa changu kwa mikono yote, nikilia kwa sauti ndogo k**a mtoto mdogo. Moyoni mwangu nilijua… tulikuwa tumekwishaingia kwenye vita ya mapenzi na giza.

Hapo ndipo nilielewa kuwa safari ya kwenda kwa mganga siyo tu ya kutafuta msaada—
Ilikuwa vita ya kuokota uhai wetu.

Na sasa, kila sekunde ilikuwa ni hatari.
Na kila pumzi yangu… Carolina alikuwa ananitazama.

Simulizi: NILIPEMDWA NA JINI BILA KUJUAMwandishi: Mwai ProductionSEHEMU YA KWANZANaitwa Mwai.Leo nakusimulia jambo ambal...
11/09/2025

Simulizi: NILIPEMDWA NA JINI BILA KUJUA
Mwandishi: Mwai Production
SEHEMU YA KWANZA

Naitwa Mwai.
Leo nakusimulia jambo ambalo mpaka leo nikilikumbuka damu yangu husimama, moyo hunidunda kwa kasi, na ngozi yangu husimama vizingiti k**a vile ipo mbele ya upepo wa mauti. Huu siyo mzaha, siyo ndoto—ni kisa cha kweli ambacho kimebadilisha maisha yangu milele.

Nilikuwa kijana wa kawaida tu, nikiwa na ndoto za maisha bora na mapenzi ya dhati. Nilimfahamu Carolina pale chuoni—binti mrembo kupita maelezo. Uso wake ulikuwa ni k**a jua la asubuhi, macho yake yalikuwa na mvuto wa ajabu, na kila aliponitazama nilihisi k**a ulimwengu mzima umesimama ili kutazama sisi wawili. Alizungumza kwa sauti nyororo yenye utulivu wa kuvuta pumzi ya mwisho kabla ya kulala.

Tulianza k**a marafiki wa kawaida, lakini mambo yakabadilika haraka. Carolina akanionyesha upendo ambao sikuwahi kufikiri ningepata. Alinitunza, alinipa maneno ya faraja nilipokuwa dhaifu, na kila mara nilihisi k**a ndiye aliyekuwa rafiki wa roho yangu. Nilihisi nimetua bandari ya salama kwenye bahari ya maisha yenye dhoruba.

Lakini sasa nikikuambia ukweli... nilikuwa nimependelewa na jini bila kujua.

Siku moja, nilikuwa nimetoka library nikikutana na Jane—msichana wa kibinadamu, tofauti na Carolina. Jane hakuwa na sura ya ajabu ajabu k**a Carolina, bali alikuwa wa kawaida lakini mwenye tabasamu la kuvunja ukuta wa giza. Kwa mara ya kwanza, moyo wangu ulinong’oneza kitu kipya—mapenzi halisi, yenye heshima na joto la mwanadamu.

Nilianza kumkaribia Jane, nikizungumza naye mara kwa mara, tukicheka k**a watoto wadogo, na taratibu nikahisi moyo wangu ukichagua upande wake. Lakini sikujua nilikuwa nimefungua mlango wa laana.

Usiku wa kwanza baada ya kuongea na Jane kwa karibu, ndoto mbaya zilianza kunisumbua. Nilimwona Carolina akiwa amevaa gauni jeupe, macho yake yakiwa mekundu k**a makaa ya moto. Akanong’ona kwa sauti nzito isiyo ya kibinadamu:

“Mwai… mimi ndiye nakupenda, na wewe ni wangu. Ukinisaliti… utajua maana ya hasira za jini.”

Nilipoamka, nilijikuta jasho limenilowesha mwili mzima. Nilidhani labda ni mawazo tu… lakini siyo.

Kesho yake, nilipokutana na Jane tena, upepo mkali usio wa kawaida ulivuma ghafla na karatasi tulizokuwa nazo zikarushwa kila pande. Jane akashika kichwa chake akisema anasikia kizunguzungu. Nilimsaidia akakaa, lakini ndani yangu nilijua… huu ulikuwa ujumbe wa Carolina.

Siku zikapita, nikaanza kuona tabia za ajabu. Nikiingia kwa Carolina, mara nikikumbatia mwili wake nilihisi baridi kali kana kwamba nakumbatia barafu. Mara nyingine macho yake yalibadilika ghafla kuwa ya paka mweusi kisha kurudi kawaida, na kila nilipojaribu kuuliza, alinitabasamu tu akisema:

“Usijali, mapenzi yangu ni ya kweli.”

Lakini moyoni mwangu nilijua, huyu si mwanadamu.

Hapo ndipo maisha yangu yakaanza kuwa vita ya mapenzi na uchawi.
Nilijikuta nimefungwa kati ya Carolina jini mwenye wivu wa mauti na Jane mwanadamu niliyempenda kwa dhati.

Na kila siku, kivuli cha Carolina kilinizunguka—nikilala, nikiamka, nikiwa na Jane, au hata nikiwa peke yangu. Upendo wake ulianza kugeuka kuwa kizuizi, kuwa kifungo cha roho, kuwa mtego wa mauti.

Sikuamini macho yangu pale nilipomwona Jane akianza kupoteza afya taratibu. Kila tulipoonana, macho yake yalionekana kuchoka, mwili wake kudhoofu… nilijua Carolina alishaanza kumfuata.

Huu ndio mwanzo wa kisa hiki cha kusisimu
mapenzi ya mwanadamu na jini, upendo uliojaa wivu, roho mbaya, na usaliti unaobeba kivuli cha uchawi.

Naapa, yote haya yalinitokea mimi mwenyewe.
Na sasa nakwambia—nilipendwa na jini bila kujua.

09/09/2025
09/09/2025
Simulizi: NILIPEMDWA NA JINI BILA KUJUAMwandishi: Mwai ProductionSEHEMU YA KWANZANaitwa Mwai.Leo nakusimulia jambo ambal...
09/09/2025

Simulizi: NILIPEMDWA NA JINI BILA KUJUA
Mwandishi: Mwai Production
SEHEMU YA KWANZA

Naitwa Mwai.
Leo nakusimulia jambo ambalo mpaka leo nikilikumbuka damu yangu husimama, moyo hunidunda kwa kasi, na ngozi yangu husimama vizingiti k**a vile ipo mbele ya upepo wa mauti. Huu siyo mzaha, siyo ndoto—ni kisa cha kweli ambacho kimebadilisha maisha yangu milele.

Nilikuwa kijana wa kawaida tu, nikiwa na ndoto za maisha bora na mapenzi ya dhati. Nilimfahamu Carolina pale chuoni—binti mrembo kupita maelezo. Uso wake ulikuwa ni k**a jua la asubuhi, macho yake yalikuwa na mvuto wa ajabu, na kila aliponitazama nilihisi k**a ulimwengu mzima umesimama ili kutazama sisi wawili. Alizungumza kwa sauti nyororo yenye utulivu wa kuvuta pumzi ya mwisho kabla ya kulala.

Tulianza k**a marafiki wa kawaida, lakini mambo yakabadilika haraka. Carolina akanionyesha upendo ambao sikuwahi kufikiri ningepata. Alinitunza, alinipa maneno ya faraja nilipokuwa dhaifu, na kila mara nilihisi k**a ndiye aliyekuwa rafiki wa roho yangu. Nilihisi nimetua bandari ya salama kwenye bahari ya maisha yenye dhoruba.

Lakini sasa nikikuambia ukweli... nilikuwa nimependelewa na jini bila kujua.

Siku moja, nilikuwa nimetoka library nikikutana na Jane—msichana wa kibinadamu, tofauti na Carolina. Jane hakuwa na sura ya ajabu ajabu k**a Carolina, bali alikuwa wa kawaida lakini mwenye tabasamu la kuvunja ukuta wa giza. Kwa mara ya kwanza, moyo wangu ulinong’oneza kitu kipya—mapenzi halisi, yenye heshima na joto la mwanadamu.

Nilianza kumkaribia Jane, nikizungumza naye mara kwa mara, tukicheka k**a watoto wadogo, na taratibu nikahisi moyo wangu ukichagua upande wake. Lakini sikujua nilikuwa nimefungua mlango wa laana.

Usiku wa kwanza baada ya kuongea na Jane kwa karibu, ndoto mbaya zilianza kunisumbua. Nilimwona Carolina akiwa amevaa gauni jeupe, macho yake yakiwa mekundu k**a makaa ya moto. Akanong’ona kwa sauti nzito isiyo ya kibinadamu:

“Mwai… mimi ndiye nakupenda, na wewe ni wangu. Ukinisaliti… utajua maana y

07/09/2025

�����

07/09/2025

Address

Kyela

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when MWAI production posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share