Lindi Press Media

Lindi Press Media Lindi Press Media is fully owned by LINDI REGIONAL PRESS CLUB, Our office is in Lindi Town.

The mission is to ensure the content promotes moral values to the public and offer them with issues.

NA BASHIRU KAUCHUMBE, RUANGWAUamuzi wa Wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi wa kupeleka Ofisi za Ardhi kila Mko...
19/09/2020

NA BASHIRU KAUCHUMBE, RUANGWA

Uamuzi wa Wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi wa kupeleka Ofisi za Ardhi kila Mkoa badala ya kuwa na Ofisi za Kanda, umeonesha mafanikio makubwa ya kurahisisha upatikanaji wa hati za kumiliki ardhi kwa haraka.



Hali hiyo imedhiirishwa kwa wakazi wa wilaya ya Ruangwa wapatao 69 ambao wamepatiwa hati za kumiliki Ardhi katika Hafla fupi ya kukabidhiwa hati iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa.

Akikabidhi hati hizo kwa wanachi hao Msajili wa Hati wa Mkoa wa Lindi Bwana Godfrey Faramagoa amesema dhima ya kufanya hivyo ni kurasimisha na kuhamsisha wananchi ambao wanaviwanja ambavyo wamevipata kwa kufuata utaratibu wa kisheria kujenga utamaduni wa kupatiwa Hati za kumiliki Ardhi.



Amezitaja faida za kuwa na hati za kumiliki hati za Ardhi ni pamoja na kuongeza thamani ya Ardhi/Kiwanja na Mashamba,Hati inaweza kutumika kwa dhamana kwa mwananchi pindi wanaposhikiliwa na jeshi la Polisi au kufikishwa mahak**ani ,pamoja na kutumika k**a dhamana ya Mikopo katika taasisi za Kifedha au Mikopo ya kilimo .

Kwa upande wake Afisa Ardhi wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Bwana Peter Hanjay amesema kuwa upatikanaji wa Hati za kumiliki Ardhi itakuwa rahisi kutokana na Wizara kusogeza huduma karibu katika ngazi ya Mikoa tofauti na awali Hati zilikuwa zinatolewa na Ofisi za Kanda kitu ambacho kilichangia wananchi wengi kushindwa kuzifuata hati hizo kwa kushindwa kumudu gharama za usafiri na malazi ,Lakini kwa sasa Mwananchi akishakamilisha Taratibu zote anapatiwa hati yale ndani ya siku saba

Hanjay amewasisitiza wakazi wa Ruangwa kuchangamkia fursa hii kwa kuanza michakato ya kupata hati za Kuliliki Ardhi ,amesema Ofisi yake ipo wazi na ipo tayari kutoa huduma hizo.

Bi Maimuna Pendeka ni Miomngoni mwa Wananchi waliopata hati hizo ,Ameishukuru wizara kwa kufungua Ofisi ngazi Ya Mkoa kwani yeye alishakamilisha mchakato wa kupata Hati Toka mwaka 2016 lakini alishindwa kuifuata Mtwara Mtwara kutokana na kushindwa gharama za Nauli na pesa za kujikimu.Pia amesema kuwa Hati hizo zitamsadia kupata Mikopo kutoka taasisi za kifedha na kuendeleza shughuli zake za kinishara.



Akijibu hoja za wananchi katika Hafla hiyo fupi kuhusu makazi yasiyo rasimi ambayo yamejengwa pasipo kuzingatia mipango miji,Afisa Mipango miji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Bwaba Isihaka Panja amewashauri wananachi wanaohitaji mpango miji katika eneo lao au kurasiisha mashamba ni wakati wao sasa kujiunganisha pamoja kwa kushirikiana na Mamlaka za Vijiji au Mitaa kwa kushirikiana na Idara ya Ardhi ili kuweza kuandaa mchakato wa kurasimisha maeneo hayo.

Jumla ya Hati 193 zimetolewa kwa Mkoa wa Lindi mbapo Wilaya Liwale zimetolewa Hati 40,Nachingwea Hati 24 na Ruangwa Hati 69.

Mkuu wa Jeshi la kujenga taifa Tanzania (JKT) Brigedia Jenerali Charles Mbuge kupitia muwakilishi wake Kanali Philipo Ma...
19/09/2020

Mkuu wa Jeshi la kujenga taifa Tanzania (JKT) Brigedia Jenerali Charles Mbuge kupitia muwakilishi wake Kanali Philipo Mahende, amewataka wahitimu 987 wa mafunzo ya awali ya kijeshi na uzalishaji mali kwa mujibu wa sheria uparesheni uchumi wa kati 2020 kikosi cha 843KJ Nachingwea Lindi kufanya kazi kwa vitendo ili kujikwamua na umasikini na kutazama fursa zitakazoweza kuwasaidia na sio kuilalamikia serikali muda wote.
https://youtu.be/doY-9RQW3WQ

Mkuu wa Jeshi la kujenga taifa Tanzania (JKT) Brigedia Jenerali Charles Mbuge kupitia muwakilishi wake Kanali Philipo Mahende, amewataka wahitimu 987 wa mafu...

19/09/2020
19/09/2020
19/09/2020
19/09/2020

Address

Lindi
Lindi
0000

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Lindi Press Media posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Lindi Press Media:

Share