07/12/2025
IFAHAMU HISTORIA YA BARABARA YA UHURU ILIYOPO MANISPAA YA LINDI TUNAPOELEKEA KUADHIMISHA MIAKA 64 YA UHURU YA TANGANYIKA.
Kupitia durusu durusu za historia leo hii nakusogezea historia ya barabara ya uhuru tunapoelekea kuadhimisha miaka 64 ya uhuru wa Tanganyika tokea ijipatie uhuru Th 09 Decemba 1961. Hivyo tutaidurusu barabara maarufu hapa lindi inayofahamika k**a barabara ya uhuru.
Kabla ya Tanganyika kupata uhuru mwaka 1961, barabara hii haikuitwa Barabara ya Uhuru k**a tunavyoijua leo. Ilifahamika k**a Queen Elizabeth Avenue, jina lililoashiria ushawishi na mamlaka ya utawala wa kikoloni wa Uingereza katika maeneo ya Afrika Mashariki. Jina hilo liliwekwa kwa heshima ya Malkia Elizabeth wa Uingereza.
Katika mji wa Lindi, kuitwa kwa barabara hii jina la Malkia kulikuwa pia ishara ya kuunga mkono mfumo wa utawala wa Muingereza ndani ya nchi ya Tanganyika.
Barabara hii ilikuwa kitovu cha uchumi wa wakati huo. Ilizungukwa na nyumba za wafanyabiashara wakubwa — hasa wafanyabiashara wa Asia (Wahindi) pamoja na Watanganyika waliokuwa wakijihusisha na biashara.
Ni muhimu kueleza kwamba Waingereza hawakuhusika moja kwa moja na biashara katika eneo hili, badala yake walijikita katika masuala ya uongozi na utawala. Hawakukaa kwenye maeneo haya ya biashara; maeneo haya ndiyo yaliyokuwa makazi na vituo vya shughuli za Watanganyika na wafanyabiashara wa Kihindi.
Katika enzi hizo, Barabara ya Uhuru ndiyo ilikuwa lango kuu la shughuli za kibiashara. Hapa ndipo palikokua na maduka, maghala na misururu ya biashara iliyoleta ajira nyingi kwa Waafrika waliokuwa wakifanya kazi za mikono, usafirishaji na huduma mbalimbali.
Mpaka leo, barabara hii inaendelea kuwa na umuhimu wake. Kwa yeyote anayefika Lindi, Barabara ya Uhuru ndiyo njia kuu inayoelekea Stendi Kuu ya Mabasi. Unapoingia mji wa Lindi ukielekea stendi, au unapotoka kuelekea safari zako, ni lazima kupita katika Barabara hii ya kihistoria — lango la kuingia na kutoka katika mji wa Lindi.
Na kisha ikafika tarehe 09 Desemba 1961
Siku ambayo Tanganyika ilitangazwa kuwa nchi huru. Wakazi wa Lindi hawakusita kuonesha shukrani na furaha yao. Walikusanyika na kubadilisha kibao cha barabara hii, wakiondoa jina la kikolon