Kagawa

Kagawa Nawapenda nyote

09/11/2025

Unaweza kudhalilisha sifa ya mtu Na kupunguza heshima yake.
Lakini hauwezi kamwe kumpokonya Neema zake.

  KAMBI ya Wakimbizi Nduta inayohifadhi Wakimbizi wa Nchi ya Burundi, inatarajiwa kufungwa ifikapo March 31 mwaka 2026, ...
19/10/2025

KAMBI ya Wakimbizi Nduta inayohifadhi Wakimbizi wa Nchi ya Burundi, inatarajiwa kufungwa ifikapo March 31 mwaka 2026, ikiwa ni mkakati wa Serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani ya Nchi pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi UNHCR, kuchukua hatua za kuwarudisha Wakimbizi wa Burundi waliokimbia nchi yao kutokana na machafuko ya vita.

Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi Wizara ya mambo ya ndani ya Nchi Tanzania Sudi Mwakibasi amesema hayo wakati akihutubia Wakimbizi wa kambi ya Nduta iliyopo Wilayani Kibondo mkoani Kigoma, na kuwa licha ya kufunga kambi hiyo, kambi ya Nyarugusu itafungwa pia Mwezi wa sita mwaka 2026, akieleza ni kutokana na kuwa na wakimbizi wengine kutoka nchi ya DRC CONGO.

Amesema, wakati ukifika Wakimbizi wote watakao kaidi kurudi hawatakuwa na maeneo ya kuishi na nyumba zao zitavunjwa sambamba na kuwachukulia hatua kutokana na kukiuka kurudi kwao katika kipindi cha promosheni ya serikaili na UNHCR.

Hatahivyo Balozi mdogo wa Burundi Nchini Tanzania Kekenwa Jeremia amewaomba ndugu zake kurudi kwa hiari na kuwaeleza kuwa, nchi ya Burundi iko salama na hakuna machafuko yoyote hivyo hawana budi kuungana na ndugu zao kujenga nchi yao kwa pamoja.

Shirika la UNHCR linaendelea na Promosheni ya uandikishaji Wakimbizi wa Burundi, waliokimbia Nchi hiyo kwa machafuko ya vita kuhakikisha wanarudi kwao sambamba na kuwahakikisha usalama, pindi watakaporejea.

19/10/2025

Address

Kasulu
Mabibo

Telephone

+255752466342

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kagawa posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category