16/09/2025
HADITHI: 𝐌𝐋𝐀𝐍𝐆𝐎 𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐅𝐎
MTUNZI: 𝐆𝐄𝐎𝐅𝐑𝐄𝐘 𝐃𝐈𝐒𝐌𝐀𝐒
SEHEMU: 04
𝑰𝑳𝑰𝑷𝑶𝑰𝑺𝑯𝑰𝑨......
"Mauaji mengine. Daktari mwingine wa kiwanda cha dawa. Mji wa Malampaka. Walakini hakuna dalili za uhalifu wa kawaida. Ni mtaalamu mwingine wa sumu.”
Subira alimtazama Kamanda wake kwa mshangao, “Sir… they’re striking again.”
“Two attacks within 12 hours. This is coordinated.”
Kamanda Nasoro alibana meno, kisha akasema kwa sauti ya amri:
“Cancel Dar. Tuelekee moja kwa moja Arusha. Tuwahishe Simiyu timu ya pili. This is no longer a local murder case. We’re dealing with a serial killer, or worse… an organization.”
𝑺𝑨𝑺𝑨 𝑬𝑵𝑫𝑬𝑳𝑬𝑨.............
ARUSHA – NJIRO – SAA 10:15 JIONI
Walipofika eneo la tukio, walikuta Inspector Mary akiwa ameweka kambi. Alikuwa ameshaweka mkanda wa Kamandaa usalama (crime scene tape) kuzunguka eneo lote. Maiti za Daudi na Dk. Rehema tayari zilikuwa zimeondolewa, lakini damu iliyo kwenye sakafu na athari za sindano kwenye mkono wa Rehema zilikuwa bado freshi.
Subira alichuchumaa karibu na sakafu, “Injection mark is clean. Straight to the vein. Whoever did this, alijua anachofanya.”
Kamanda Nasoro alichukua picha ya bastola ya Daudi aliyokuwa ameshikilia mpaka mwisho wa maisha yake, “Hii bastola ilikuwa loaded?”
“Ndiyo. Risasi zote 12 bado zipo. Hakuweza hata kupiga moja.”
Nasoro alitazama kamera za CCTV zilizozimwa kwa EMP.
“This is tactical. They planned this for weeks. Kila hatua imepangwa. They don’t just want these scientists dead, wanataka kazi zao zipotee kabisa.”
FILE LA KESI – “PROJECT SALAAM”
Baada ya uchunguzi wa awali, Subira alipata nyaraka zilizoonesha kuwa Dk. Rehema alikuwa sehemu ya mradi wa siri wa serikali unaoitwa “Project Salaam”. Mradi huo ulikuwa unahusu utafiti wa dawa zinazoweza kudhibiti silaha za kemikali, hasa kwa ajili ya ulinzi wa taifa dhidi ya mashambulizi ya kigaidi.
Kitu cha kushangaza zaidi? Dk. Rehema alikuwa akishirikiana na Dk. Hamza Rajabu, yule aliyekufa Simiyu.
Kamanda Nasoro alinyamaza kwa muda, macho yake yakitazama faili hilo, “This is bigger than I thought… Hawa watu hawauwi tu, wanazima utafiti mzima. Lazima kuna mtu mkubwa anawashika mkono.”
Kamanda Nasoro akajiapiza moyoni, “Sitapumzika hadi niwak**ate. Nikiwa hai au mfu.”
Lakini hakuwa anajua, mauaji haya yalikuwa tu mwanzo. Na mtego tayari ulikuwa umewekwa kwa ajili yake.
KIFO KIMYA – SIMIYU
Simiyu –Malampaka – Saa 6:42 usiku
Usiku ulikuwa mzito. Anga la kijiji cha Malampaka lilikuwa limetandwa na mawingu meusi, yasiyo na nuru hata ya mwezi. Barabara ya vumbi iliyopitia mbele ya nyumba ya Daktari Hamza Rajabu, mtaalamu wa utafiti wa molekuli katika kiwanda cha dawa cha Biogene Africa Ltd, ilikuwa kimya – si kawaida kwa maeneo haya ambayo watoto hupiga kelele hadi saa tatu usiku.
Ndani ya nyumba hiyo ya vyumba vitatu, kulikuwepo na uhai wa hatari. Saa 6:27 usiku, mtu asiyejulikana alivunja usalama wa milango ya elektroniki kwa kutumia kifaa cha kuvuruga security signal kinachojulikana k**a CodeJammer X90 – kifaa kinachotumika na maajenti wa kijasusi kudukua mifumo ya usalama ya majengo.
Mhalifu huyo aliingia kwa utulivu, akiwa amevalia sare ya kawaida ya kiwanda – madoadoa ya bluu na beji bandia ya kiwanda hicho. Bastola yake ilikuwa ya kimya, aina ya Walther PPK, maarufu kwa matumizi ya kijasusi tangu enzi za Vita Baridi.
Dkt. Hamza: Damu ya Mwanasayansi
Dk. Hamza alikuwa ameketi sebuleni akipitia faili la kidigitali lililokuwa limefungwa kwa password encryption. Alikuwa anachunguza taarifa za vifo vya wenzake wawili: Dk. Rehema Yusuf wa Arusha, na mtaalamu wa maabara wa Dar es Salaam aliyepotea wiki mbili zilizopita. Moyo wake haukuwa na amani.
Alishtuka kwa sauti ya kitu kilichoanguka jikoni. Kabla hajainuka, alisikia mlio mdogo k**a upepo – phhhh!
Risasi ya kwanza ilimgonga begani. Hakuweza kupiga kelele. Alijaribu kutambaa kuelekea mlango wa mbele, lakini mhalifu alimsogelea haraka na kumpiga sindano moja ya sumu ya sodium thiopental, ambayo humfanya mtu kupoteza fahamu ndani ya sekunde 15. Kisha akampiga sindano ya pili ya potassium chloride, iliyosababisha moyo wake kusimama kabisa.
Kabla hajaondoka, mhalifu huyo alichukua USB flash iliyokuwa mezani, ndicho kilichokuwa kinatafutwa.
Uchunguzi Wa Polisi – Usiku Uleule
Kufuatia taarifa ya majirani waliomsikia Hamza akigugumia, SP (Superintendent of Police) Samwel Kibwana, Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Bariadi, aliwasili na timu yake saa 8:02 usiku. Aliongozana na ASP (Assistant Superintendent of Police) Khadija Musa, mtaalamu wa uchunguzi wa kisayansi wa vituo vya uhalifu (forensics).
ASP Khadija alipiga picha mwili wa Dk. Hamza, akatazama alama ya sindano mkononi.
“This is precision work. No signs of struggle, no broken locks. They knew him, or knew how to get in,” alisema huku akipiga picha kwa simu yake yenye app ya ballistic evidence capture.
SP Kibwana alichungulia chini ya meza na kuona casing moja ya risasi – .32 ACP, risasi maarufu kwa bastola za kijasusi, “Walther PPK. Bastola ndogo, kimya, deadly,” alisema.
Taarifa Kufika TISS – Mwanza
Saa mbili baadaye, tukio hilo liliripotiwa kwa Afisa Usalama wa Taifa Mkoa wa Simiyu, Senior Intelligence Officer (SIO) Abbas Kimario, aliyekuwa akifuatilia shughuli za kiwanda hicho kwa miezi miwili. Aliwasiliana na Makao Makuu ya Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) jijini Dodoma, na kutoa taarifa ya hatari, "Wataalamu wa viwanda vya dawa wanauawa kwa utaratibu unaoonyesha involvement ya majeshi au maajenti waliopitia mafunzo maalum ya ‘Black Ops’. Kuna uwezekano wa uvujaji wa siri za kitaifa."
Mpango wa Kitaifa Wa Kuzuia Mauaji Zaidi
Kutoka Arusha, ACP (Assistant Commissioner of Police) Nasoro Mtei alipokea taarifa hizo akiwa bado eneo la mauaji ya Rehema. Alisimama kimya kwa dakika moja kabla hajageuka kwa Detective Subira Hassan, aliyekuwa akipanga picha za CCTV zilizokuwa corrupted, “Prepare a report to IG’s office. Tuweke suala hili chini ya ‘Operation Mauti Kimya’ – a joint task force between TISS, CID na JWTZ,” alisema Nasoro, “Yes, sir,” Subira alijibu kwa ukaidi wa kazi.
Silaha, Mbinu na Njama
Taarifa kutoka kwa SIO Abbas zilionyesha kwamba mtu aliyemuua Dk. Hamza alitumia mbinu za kijeshi k**a vile, “Room Clearing” – kusafisha chumba kwa utaratibu wa haraka bila kugusa vitu.
“Needle kill” – mbinu ya kutumia sindano kimya kwa kudunga mishipa mikuu.
“EMP Jammer” kuvuruga CCTV na mitandao ya ndani.
Taarifa hizo zilipelekea kuamini kuwa huu haukuwa mhalifu wa kawaida bali mtu aliyepitia mafunzo ya kijasusi, au labda ni afisa wa zamani wa vikosi maalum.
****
Kufikia saa kumi alfajiri, vifo vitatu vya wanasayansi waliojikita katika utafiti wa dawa vilikuwa vimegusa mikoa mitatu tofauti ndani ya masaa 24: Arusha, Simiyu na Mwanza.
Kamanda Nasoro alitazama ramani ya Tanzania, akawasha red marker. Alichora mstari kutoka Arusha hadi Mwanza, kupitia Simiyu, akasema, “They’re moving in a pattern. Naona wanalenga sehemu fulani. But what’s the next target? Dodoma? Dar?”
Subira alitazama faili la “Project Salaam,” macho yake yakiwa hayapepesi.
“Sir… If the pattern holds, the next victim is in Dodoma. And he’s still alive.”
𝑰𝑻𝑨𝑬𝑵𝑫𝑬𝑳𝑬𝑨.......