25/10/2025
π : Mchungaji wa kanisa la Alfa na Omega raia wa Marekani mwenye asili ya DRCongo aaga dunia huko Indiana Polis
Ni Mchungaji Pascal wa kanisa la Alfa na Omega raia wa Marekani mwenye asili ya DRCongo aliyeaga dunia hiyo Ijumaa Oktoba 24, 2025 mjini Indiana Polis huko Marekani.
Chanzo chetu cha siri kuhusiana na habari hii kilichopo huko USA kimesema kuwa, Mchungaji Pascal aliyetokea kwenye kambi ya Malawi na anayetajwa kuwa wa asili ya Bashi wa Bukavu alipatwa na mauti njiani mapema asubuhi akitokea nyumbani kwake na kujielekeza kwenye kazi yake ya duka.
Yote yalianzia pale Mchungaji Pascal alipowa ndani ya gari na kuanza kusikia moyo kuwaka moto sana. Bila kuchelewa, akaamua kulisimamisha baada ya kushindwa kabisa kutembeza na kupiga simu kwa msaada wa dharura.
Dakika chache baadaye, polisi na wasamaria wema wengine wakawasili eneo alipokuwa amepaki gari; wakamkuta akiwa kwenye hali mbaya zaidi. Bila kuchelewa wakapigia gari la wagonjwa simu ambapo gari hilo liliwasili hapo Mchungaji akiwa tayari ameshakata roho.
Mpaka sasa, mpango wa mazishi ya Mchungaji Pascal ambaye ameacha mjane wa kabila la Wabembe na zaidi ya watoto 3 haujatangazwa.
Mchungaji Pascal atakumbukwa na wengi kwa ukarimu wake alipokuwa dukani kwake kuuzia wateja wake nguo, samaki na dagaa toka Ziwa Viktoria na Tanganyika pamoja na chakula cha asili ya Afrika.
Uongozi wa #"HNC" unatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa kumpoteza mpendwa wao, Mungu azidi kuwafariji na kumpumzisha marehemu kwa amani.