03/10/2025
Mgombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama Cha mapinduzi CCM Dokta Samia Suluhu Hassan amesema serikali inaendeleaje na mazungumzo na serikali ya India katika kuhakikisha Bei ya mbaazi inapanda Ili wakulima wa mbaazi wanufaike na zao Hilo.
Dokta Samia amesema hayo Leo wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Hanang mkoani Manyara baada ya kuanza kampeini zake rasmi katika mkoa wa Manyara, amewataka wananchi waendelee kuwa watulivu wakati serikali ikiendelea na mazungumzo.
Kwa upande wake mgombea ubunge wa Jimbo la Hanang Asia halamgha, amemshukuru Dokta Samia Kwa kuleta maendeleo katika wilaya ya Hanang katika sekta ya maji,umeme,barabara pamoja na elimu na kuwaomba wananchi kumchagua Kiongozi huyo.
Aidha, Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye amesema wananchi wa Hanang wamejupanga kumpigia kura Kiongozi huyo kutokana na kazi kubwa ya maendeleo aliyoifanya katikati kipindi chote Cha uongozi wake.
Dokta Samia Suluhu Hassan kesho October 4 atazungumza na wananchi wa mkoa wa Manyara katika viwanja vya stendi ya zamani na kunadi sera zake.