15/12/2025
Timu ya Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imeendesha Mafunzo kwaajili ya uandaaji wa Mipango na Bajeti katika Mikoa na Maamlaka za Serikali za Mitaa katika Ukumbi mdogo wa Halmashauri ya Wilaya mapema hii leo 15/12/2025. Mafunzo haya yamefunguliwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Ndugu Juma Kilimba na kuendeshwa na Wataalamu wa Mipango na Bajeti ndugu Haygaru Karengi na Juma Lugwisha.
Aidha Mafunzo haya yamehudhuliwa na Wakuu wa Idara, Vitengo na Maafisa Bajeti yakilenga utengenezaji wa Bajeti inayolenga kujibu mahitaji ya jamii kuanzia ngazi ya Kijiji/Mtaa, Kata, Halmashauri, Wilaya, Mkoa, Wizara ya fedha hadi ngazi ya Bunge.
Pia Waendeshaji wa Mafunzo wamewataka Watalamu hawa kuzingatia Usimamizi bora wa rasilimali, Kipimo cha utendaji, Mwongozo wa utekelezaji wa maendeleo, uwajibikaji na uwazi, Kuchochea maendeleo ya kiuchumi, Kusaidia uratibu wa mahusiano na wadau wa Maendeleo na kuhakikisha usawa na mshikamano wa Kitaifa wakati wa uandaaji wa Mipango ya Bajeti.