Globify

Globify Issa Halili,
Founder & CEO of GLOBLIFY
+255782621022

GLOBIFY is a global digital media network, marketplace and platform that provides dynamic solutions and digital services based on programs and contents which inform, engage and entertain the world.

Let Love Connect Us ❤️
31/05/2025

Let Love Connect Us ❤️

Sikukuu njema ya Eid al-Fitr kwa Waislamu na wanafamilia wote wa globify.
31/03/2025

Sikukuu njema ya Eid al-Fitr kwa Waislamu na wanafamilia wote wa globify.





Globify tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwenu wadau kwakuwa nasi mwaka 2024. Msaada wenu, ushirikiano, na juhudi ...
01/01/2025

Globify tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwenu wadau kwakuwa nasi mwaka 2024. Msaada wenu, ushirikiano, na juhudi zenu zimekuwa nguzo muhimu ya mafanikio yetu. Tumefanikiwa kwa pamoja, na tunathamini sana mchango wenu katika kila hatua. Tuna furaha kubwa kuwa na ninyi k**a wadau wetu na tunatarajia kuendelea kushirikiana katika mwaka mpya, tukielekea kwenye malengo mapya na mafanikio zaidI

Heri ya Mwaka Mpya 2025
Tunawatakia mwaka mpya wenye furaha, afya njema, na mafanikio. Asanteni kwa kuwa sehemu ya safari yetu, na tukiwa pamoja, tutavuka vikwazo na kufikia malengo makubwa zaidi

GLOBIFY

*GLOB8FY HISTORY**IJUE HISTORIA YA PICHA HII*Inawezekana umeiona hii picha mara nyingi, ila leo utaifahamu stori ya kusi...
26/12/2024

*GLOB8FY HISTORY*

*IJUE HISTORIA YA PICHA HII*

Inawezekana umeiona hii picha mara nyingi, ila leo utaifahamu stori ya kusikitisha iliyojificha nyuma ya hii picha, stori inaanzia karne ya 15 katika kijiji kidogo kilichopo pembeni ya jiji la Nuremberg, huko ujerumani.

Kulikua na familia yenye watoto kadhaa, ilikua ni familia maskini ili kupata mkate wao wa kila siku ilibidi Baba yao afanye kazi kwa zaidi ya masaa 18 kwenye machimbo ya makaa ya mawe na walikula chochote walichopata, ila kulikua na watoto wawili katika familia hiyo ambao walikua na ndoto ya kuwa wachoraji wakubwa.

Walifahamu Baba yao hana uwezo wa kuwapeleka chuo wakasomee fani hiyo ya uchoraji, ikawa kila siku usiku wanajadiliana vipi watafikia ndoto zao, siku moja baada ya majadiliano mengi ya usiku wa siku nyingi kupita hawa watoto wawili walikubaliana kuwa watarusha shilingi juu ili wapate mshindi na atakaeshindwa itabidi aende akafanye kazi kwenye machimbo ya makaa ya mawe kwaajili ya kutafuta pesa na kumlipia ada ya chuo atakaeshinda, na baada ya mshindi kumaliza masomo nae atamsomesha mwenzake aliebaki kwa kuuza kazi ya sanaa ya uchoraji atakayokua anaiuza.

Kulivyokucha walirusha shilingi juu mmoja anaeitwa Albrecht Dürer alishinda na akaenda kusoma jijini Nuremberg, Germany. Kaka yake akabaki kufanya kazi ya hatari kwenye machimbo ya makaa ya mawe kwa miaka 4 ili kulipa ada ya Albrecht, na bahati nzuri Albrecht alikua na uwezo mkubwa sana chuo na hadi anamaliza masomo yake alianza kupata pesa kutokana na kazi zake za sanaa.

Baada ya kumaliza masomo Albrecht Dürer alirudi kijijini kwao na akakuta familia imemuandalia sherehe ya heshima kwa mafanikio hayo, wakiwa wanasherehekea Albrecht alisimama mbele ya meza iliyoandaliwa kwa heshima yake na akamshukuru kaka yake kwa kujitoa ili amsomeshe na akasema pia yupo tayari kumlipia ada kaka yake ili nae akasome k**a ilivyokua makubaliano yao, lakini habari ya kusikitisha ni kuwa kaka yake alikataa

Albrecht Dürer akamuuliza kaka yake kwanini unakataa? Kaka yake akajibu " Hapana mdogo wangu mimi sitaenda Nuremberg kusomea sanaa ya uchoraji, nimeshachelewa sana, hii miaka minne niliyofanya kazi kwenye machimbo imeharibu mikono yangu, kila mfupa ulio kwenye vidole vyangu hakuna ambao haujawahi kuvunjika, vidole vya mkono wangu wa kulia kila siku vinazidi kukak**aa, hata kwenye sherehe yako nimepata shida kushika glass kugonga cheers na wewe".

"Siwezi kushika kalamu wala brash, ila nina furaha mikono yangu hii iliyojaa kasoro imeweza kusaidia wewe kufikia ndoto yako".

Albrecht Dürer alilia sana kwaajili ya kaka yake, kaka aliejitoa kuvunjika vidole ili amsomeshe yeye na mwisho hakuhitaji malipo yoyote.

Ni zaid ya miaka 450 sasa imepita tangu siku ya tukio hilo, Albrecht Dürer alichora picha nyingi zilizojaa kwenye makumbusho ila siku moja aliamua achore picha ya mikono ya kaka yake ikiwa imekutana pamoja na inaelekea mbinguni k**a ishara ya kushukuru, na picha yenyewe ndo hii ambayo imekua maarufu hata kwa wasiojua historia yake.

*GLOBIFY*

Heri ya Siku ya Uhuru wa Tanzania!🇹🇿Tunaposherehekea miaka 63 Tuendelee kudumisha umoja, amani na upendo.GLOBIFY
09/12/2024

Heri ya Siku ya Uhuru wa Tanzania!🇹🇿

Tunaposherehekea miaka 63 Tuendelee kudumisha umoja, amani na upendo.

GLOBIFY

GLOBIFY CHARITY ZANZIBAR 08 DEC 2024Watoto Yatima Wana Ndoto, Hebu Tuzisaidie Ziwe Halisi Kupitia Upendo Na Ukarimu Wetu...
22/11/2024

GLOBIFY CHARITY ZANZIBAR 08 DEC 2024

Watoto Yatima Wana Ndoto, Hebu Tuzisaidie Ziwe Halisi Kupitia Upendo Na Ukarimu Wetu.

Watoto Ni Baraka, Lakini Wanahitaji Walezi Na Moyo Wako Wa Ukarimu Ili Kuinuka.

Jiunge Na Globify Charity Ili Kugusa Maisha Yao Moja Kwa Moja Kupitia- https://chat.whatsapp.com/BiYVpSHVGt34tTA2eMQA3z

GLOBIFY CHARITY - LET LOVE CONNECT US

Globify Charity Yatoa Msaada kwa Watoto Yatima Katika Kituo Cha Islamic Yatima FoundationWadau wa Globify Charity, kwa m...
14/10/2024

Globify Charity Yatoa Msaada kwa Watoto Yatima Katika Kituo Cha Islamic Yatima Foundation

Wadau wa Globify Charity, kwa moyo wa upendo na mshik**ano, wametembelea kituo cha watoto yatima cha Islamic Yatima Foundation kilichopo Ilemela, Mwanza. Katika ziara hiyo, walikabidhi mahitaji muhimu kwa watoto hao, yakiwemo magodoro, vyandarua, vifaa vya shule, mahitaji ya vyakula na nguo.

Baada ya kutoa msaada, wadau walipata nafasi ya kutembelea Saanane National Park na kujionea vivutio mbalimbali vya kipekee vinavyopatikana katika hifadhi hiyo ya kitalii.

Uongozi wa Globify Charity unatoa shukrani za dhati kwa wadau wote waliowezesha mafanikio ya tukio hili kupitia michango ya fedha, vifaa, uhamasishaji, na ushiriki wa moja kwa moja katika safari hii ya matendo ya huruma na upendo kwa jamii. Pia, uongozi unatoa shukrani za dhati kwa uongozi wa kituo kwa mapokezi na ushirikiano mzuri. Uongozi unawakaribisha wadau wengine kuungana na Globify ili kupata fursa za uelimishaji na ushiriki katika matukio ya kijamii.

Jiunge nasi kupitia https://chat.whatsapp.com/BiYVpSHVGt34tTA2eMQA3z

Let Love Connect Us.

Ulisoma na mtu gani maarufu!?
08/10/2024

Ulisoma na mtu gani maarufu!?




SHERIA 6 ZA KUFANIKIWA MAISHANI: 1. Tambua mshindani wako ni yule uliyekuwa jana2. Tengeneza pesa na wekeza kabla ya kul...
01/10/2024

SHERIA 6 ZA KUFANIKIWA MAISHANI:

1. Tambua mshindani wako ni yule uliyekuwa jana

2. Tengeneza pesa na wekeza kabla ya kula bata

3. Kwepa watu hasi, maisha ni mafupi

4. K**a usiposaka kile unachokitaka, hutakipata.

5. Ona kufeli k**a mwanzo tu, sio mwisho.

6. Tabia zetu ndizo huamua maisha yetu ya baadae.

GLOBIFY

"Haijalishi ni kiasi gani tunachotoa bali ni upendo kiasi gani tunaowekeza katika kutoa"Kila tendo jema ni sadaka . Toa,...
29/09/2024

"Haijalishi ni kiasi gani tunachotoa bali ni upendo kiasi gani tunaowekeza katika kutoa"

Kila tendo jema ni sadaka . Toa,penda,rudia,tenda wema,tabasamu na uonyeshe utofauti katika kutoa kwako

Jiunge nasi tukawape tabasamu watoto wenye uhitaji
https://whatsapp.com/channel/0029VaER90OEgGfVZhNXv00o/1336

GLOBIFY

Address

Masaki

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Globify posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Globify:

Share