masasione_onlinetv

masasione_onlinetv business number
Call: 0715 507 823 / 0656 733 060
MTWARA || MASASI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Emmanuel Nchimbi, ametangaza uamuzi wa kustaafu siasa na utumish...
25/08/2026

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Emmanuel Nchimbi, ametangaza uamuzi wa kustaafu siasa na utumishi wa umma.

Nchimbi amesema leo, Agosti 25, 2026, amemuandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kumjulisha kuhusu uamuzi huo pamoja na nia yake ya kujiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais.

Amesema kujiuzulu kwake kutaanza rasmi tarehe 4 Septemba 2026, akieleza kuwa amefanya uamuzi huo kwa kuzingatia matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nchimbi ameeleza kuwa tarehe 27 Agosti 2025 alimuahidi Rais Samia kuwa angemsaidia yeye na taifa kwa uwezo wake wote na kwa uaminifu, huku akiahidi pia kuachia nafasi hiyo endapo Rais angeona anahitaji Makamu mwingine wa Rais.

“Nimejiridhisha pasipo shaka kuwa Mhe. Rais anatamani mabadiliko, hivyo nimeamua kutimiza ahadi yangu”, amesema Nchimbi.

Aidha, amemshukuru Rais Samia pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa imani waliyoonyesha kwake, huku akiwashukuru Watanzania kwa ushirikiano waliompa wakati wote aliokuwa katika utumishi wa umma.

Nchimbi amesisitiza kuwa pamoja na kustaafu siasa na utumishi wa umma, ataendelea kuwa raia mwema wa Tanzania.

Sponsored by mezanikwetu kaributujenge_hardware

Katika kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa kwake, Jeshi la Magereza limekabidhi msaada wa mashine ya kufulia nguo (was...
24/08/2026

Katika kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa kwake, Jeshi la Magereza limekabidhi msaada wa mashine ya kufulia nguo (washing machine) kwa Shule ya Msingi Jumuishi ya Masasi ikiwa ni sehemu ya kuendelea kuboresha huduma za kijamii.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkuu wa Magereza la Wilaya ya Masasi, SSP Selemani Ndivata alieleza kuwa Jeshi la Magereza linaendelea kushirikiana na jamii katika kuhakikisha utoaji wa huduma bora hususan kwa makundi yenye mahitaji maalumu.

“Maadhimisho ya Miaka 65 ya Jeshi la Magereza yanatoa fursa kutafakari mchango wetu kwa jamii na kutekeleza shughuli mbalimbali zenye manufaa kwa wananchi. Shule ya Msingi Jumuishi ya Masasi ina jukumu muhimu la kutoa elimu kwa watoto wenye mahitaji mbalimbali, hivyo msaada huu utasaidia kurahisisha shughuli za usafi na kuwawezesha walimu na watumishi wa shule kutumia muda mwingi katika majukumu ya msingi ya malezi na elimu”, alisema SSP Ndivata.

Kwa upande wake, Uongozi wa Shule ya Msingi Jumuishi ya Masasi ulitoa shukrani kwa Jeshi la Magereza kwa msaada huo, ukieleza kuwa mashine hiyo ya kufulia nguo itakuwa na manufaa makubwa katika kuboresha mazingira ya shule na kurahisisha shughuli za usafi wa mavazi na vifaa mbalimbali vinavyotumiwa na wanafunzi.

Aidha, Afisa Ustawi Halmashauri ya Mji Bi. Leila Kassugulu, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi, alilipongeza Jeshi la Magereza kwa kuendelea kuwa karibu na jamii na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha huduma za kijamii.

“Nitoe rai pia kwa taasisi zingine za umma na binafsi kuendelea kushirikiana nasi katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi hasa makundi maalum”, alisema Bi. Leila.

Jeshi la Magereza limeahidi kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika shughuli za maendeleo na kuhakikisha Maadhimisho ya Miaka 65 yanaacha alama chanya kwa jamii.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Jumamosi Agosti 22, 2026 amezindua rasmi Kituo ch...
22/08/2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Jumamosi Agosti 22, 2026 amezindua rasmi Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP), kilichopo Rufiji, Mkoa wa Pwani.

JNHPP ni mradi mkubwa wa kimkakati katika sekta ya nishati Nchini, wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 2,115 kupitia mitambo tisa, kila mmoja ukiwa na uwezo wa Megawati 235.

Mradi huo umegharimu takribani shilingi trilioni 7.452, fedha za ndani za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ujenzi wake ulianza Juni 2019 na kukamilika Machi 2025.

Sponsored by mezanikwetu kaributujenge_hardware

18/08/2026

DKT.AKWILAPO AMEPAMBANA SANA KUNUSURU MAISHA YA MWANANGU

Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb), amesisitiza umuhimu wa kuimarisha Ushirikiano kati Sekta ya Umma na Sekta Binafsi...
17/08/2026

Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb), amesisitiza umuhimu wa kuimarisha Ushirikiano kati Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) katika kuongeza uwekezaji na kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maji nchini.

Ameyasema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya Wizara ya Maji katika K**ati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira kuhusu mgawanyo wa fedha za Mfuko wa Taifa wa Maji kwa kipindi cha miaka mitatu, kuanzia mwaka 2024 hadi 2025.

Waziri Aweso amesema Serikali inaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha rasilimali zinatumika kwa ufanisi, sambamba na kushirikisha sekta binafsi na wadau mbalimbali katika kuongeza uwekezaji na kuboresha huduma za maji nchini.

Amesisitiza umuhimu wa kukamilisha miradi ya maji vijijini, kwasababu Serikali inalenga kumaliza uhaba wa maji katika vijiji 1,575 ambavyo bado havijafikiwa na miundombinu ya huduma ya maji.

Waziri Aweso amesisitiza matumizi bora ya fedha za Mfuko wa Taifa wa Maji kwa kuzielekeza katika maeneo yenye mahitaji makubwa, na kutaka utekelezaji wa miradi uzingatie thamani ya fedha kwa kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa kwa manufaa ya wananchi.

Sponsored by mezanikwetu kaributujenge_hardware

Katika Kuazimisha Miaka 15 ya Uajiliwa na Kulitumikia Jeshi La Polisi Jumla Ya Askari 18 Wa Jeshi La Polisi Wilaya Masas...
15/08/2026

Katika Kuazimisha Miaka 15 ya Uajiliwa na Kulitumikia Jeshi La Polisi Jumla Ya Askari 18 Wa Jeshi La Polisi Wilaya Masasi Wanaotambuliwa K**a GH Tanzania kwa Waliohitimu na Kuajiliwa Miaka ya 2011-2012 Wamerejesha Katika Jamii kwa kuenda Kutoa Msaada kwa Wanafunzi Wenye Uhitaji Maalum wa Shule Ya Msingi Elimu Jumuishi Masasi

Kwaniaba Ya Jumla Ya Askari Polisi 18 Wa GH TANZANIA Wilaya Ya Masasi Mkaguzi Wa Jeshi La Polisi Raphael Mayala amesema kuwa Wametoa kidogo walichobarikiwa kwa kurudisha kwenye jamii k**a sehemu ya kuazimisha Miaka 15 ya Utumishi Wao

Vitu Walivyotoa ni Vinywaji Baridi, Mchele, Sabuni, Mafuta Ya Kupikia, Unga, Sukari na Maharage ili kuwafanya Watoto hao waendelee kujiona ni sehemu ya Jamii k**a Walivyo wengine ambao hawana Mahitaji Maalum

Sponsored by mezanikwetu kaributujenge_hardware

Mtoto Swaila amezikwa leo mjini Masasi, katika mazishi yaliyohudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini, Dkt. Leonard ...
15/08/2026

Mtoto Swaila amezikwa leo mjini Masasi, katika mazishi yaliyohudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini, Dkt. Leonard Douglas Akwilapo.

Swaila alifariki dunia nchini India Agosti 10, 2026, wakati akiendelea na matibabu baada ya kufanyiwa operesheni.

Mwili wake uliwasili Masasi kutoka nchini India, huku familia, ndugu, jamaa na wananchi wakijitokeza kwa wingi kushiriki katika mazishi na kutoa heshima za mwisho.

Mbunge Dkt. Leonard Akwilapo, ambaye alishiriki katika juhudi za kumpeleka Swaila nchini India kwa matibabu, naye alihudhuria mazishi hayo na kuungana na familia katika kipindi hiki cha majonzi.

Mungu ailaze roho ya Swaila mahali pema peponi.

Sponsored by mezanikwetu kaributujenge_hardware

Mwili wa mtoto Swaila, aliyefariki dunia nchini India wakati akipatiwa matibabu, umewasili mjini Masasi.Swaila alipelekw...
14/08/2026

Mwili wa mtoto Swaila, aliyefariki dunia nchini India wakati akipatiwa matibabu, umewasili mjini Masasi.

Swaila alipelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu kupitia juhudi za Mbunge wa Masasi Mjini, Dkt. Leonard Douglas Akwilapo.

Kifo chake kilitokea Agosti 10, 2026, baada ya kupata mshtuko wa moyo kufuatia changamoto za kiafya baada ya kufanyiwa operesheni.

Mazishi ya mtoto Swaila yanatarajiwa kufanyika kesho, Agosti 15, 2026, majira ya saa nne asubuhi.

Sponsored by mezanikwetu kaributujenge_hardware

13/08/2026

WABUNGE WA VITI MAALUM MTWARA WATOA VITI MWENDO KWA WENYE ULEMAVU, WAITAKA JAMII KULINDA KUNDI HILO

Mnadhimu Wa Jeshi la Polisi Kitengo Cha Usalama Barabarani Kamishina Msaidizi Mwandamizi Wa Polisi Butusyo Akim Mwambelo...
11/08/2026

Mnadhimu Wa Jeshi la Polisi Kitengo Cha Usalama Barabarani Kamishina Msaidizi Mwandamizi Wa Polisi Butusyo Akim Mwambelo amewataka Madereva Wa Vyombo Vya Moto Kutumia Vyuo Vilivyosajiliwa Ili Kupata Elimu ya Usalama Barabarani
itakayowawezesha Kupata Vyeti kisha Leseni Ya Udereva kwa Njia Ya Uhalali

Ameyasema hayo akiwa Ziarani Wilaya Ya Masasi Mkoani Mtwara akielezea kuwa amebaini na kuwak**ata Madereva 6 Wenye Leseni Zilizopatikana kwa Njia Isiyo Sahihi

Ziara hiyo imelenga Kukagua Utendaji Kazi Wa Askari Wa Usalama Barabarani, Kukagua Vyombo na Madereva, na Kutoa Elimu na Maadili ya Kazi kwa Watumiaji wa Barabara

Aidha K**anda Wa Polisi Kitengo Cha Usalama Barabarani Mkoa Wa Mtwara Kamishina Msaidizi wa Polisi Emilian Kamuhanda Ametaja Kuwa Mkoani Mwake Vipo Vyuo 5 vilivyosajiliwa Kutoa Elimu Hiyo na Kuwataka Madereva Waache Tabia Ya Kutembea na (Lost Report) bali hiyo iwasaidie tu Kupata Leseni Mpya.

Sponsored by mezanikwetu kaributujenge_hardware

Address

MASASI TOWN COUNCIL (MTC)
Masasi
MIGONGO

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when masasione_onlinetv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share