Udaku news

Udaku news Kwa habari zimezo trendi katika michezo na music muda wotee

10/02/2022

Hellow sorie naomba radhi kwa kuto kupost kweenye kurass hii fans wote mniuie radhi kuna tatizo kidogo likitokea hope next weekii kila kitu kitakua sawa

24/12/2021

KMS Vs SIMBA
1. - 4
Full time

24/12/2021

Umoja wa Ulaya umeidhinisha chanjo yake ya tano dhidi ya ugonjwa wa Covid-19, wakati shirika la afya duniani likihimiza kuongezwa kasi katika kukabiliana na kirusi cha Omicron.

Jana Jumatatu, wakala wa dawa za Ulaya EMA iliidhinisha chanjo kutoka kwa kampuni ya dawa ya Marekani ya Novavax.

Novavax ni chanjo ya tano kuidhinishwa na Umoja wa Ulaya baada ya Pfizer, Moderna, AstraZeneca na Johnson & Johnson, tayari Umoja huo umetia saini mkataba wa kununua hadi dozi milioni 200 za chanjo hiyo ya Novavax.

Kampuni hiyo ya dawa imesema chanjo yake imeonesha ufanisi wa asilimia 90.4 dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 wakati wa majaribio yake.

24/12/2021

Mwili wa Mama Mzazi wa Msanii wa Bongofleva Lulu Diva umezikwa nyumbani kwao Muheza, Tanga leo mchana baada ya kufariki jana Jijini Dar es salaam, AyoTV na millardayo.com zinatoa pole kwa Lulu Diva, Ndugu Jamaa na Marafiki walioguswa na msiba huu. 🙏🏿

24/12/2021
24/12/2021

Polisi nchini Kenya wanamshikilia Dereva Bodaboda kwa tuhuma za mauaji ya Mwanafunzi wa Form Three katika Shule ya Sekondari Thaara ambaye walikutana nae Facebook.

Polisi wanasema wawili hao walikutana Facebook na kuanzisha urafiki na Mwanafunzi akasafiri kutoka Kijiji cha Kamahuha na akamfuata Mwanaume nyumbani kwake eneo la Gaturi ambako umauti umemkutia.

"Mwili utafanyiwa uchunguzi kujua kilichopelekea kifo cha Mwanafunzi huyo, na tayari tunaendelea kuwahoji Majirani ambao wamekiri kumuona Mwanafunzi akiingia ndani kwa Bodaboda huyo"

24/12/2021

Vilio na simanzi vimetawala wakati wa Ibada ya kumuaga Mwanafunzi ambaye amehitimu katika Chuo Cha SUA mkoani Morogoro, Magreth Mashuwe aliyeuawa na Watu wasiojulikana katika mashamba ya Chuo hicho hivi karibuni.

Ibada hiyo imefanyika katika viwanja wa Mochwari ya Hospitali ya Rufaa mkoa Morogoro na imehudhuriwa na Ndugu, Jamaa na Marafiki.

Dada wa marehemu, Liliani Mashuwe amesema mazishi yanatarajiwa kufanyika katika Kijiji cha Shimbikati kata ya Mkuu, Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro December 23, 2021 na kusisitiza kuwa wao k**a Familia wanaziachia mamlaka husika kufuatilia tukio hilo ili kuwabaini waliohusika.

24/12/2021

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dr. Dorothy Gwajima amesema mpaka sasa nchini Tanzania ni Watu 739 wamefariki tangu ugonjwa wa covid-19 uingie nchini huku idadi ya Wagonjwa waliopatwa na ugonjwa huo hadi sasa ikifikia 28218.

Dr. Gwajima ameyasema hayo leo December 22, 2021 mkoani Arusha akizindua kampeni harakishi na shirikishi kwa Jamii awamu ya pili ya mapambano dhidi ya covid-19 na kuhudhuriwa na Viongozi wa Serikali, Dini na Wananchi wa Arusha na Mikoa ya jirani.

Dr. Gwajima amewasisiza Watanzania kujitokeza kwenda kuchanjwa na kuongeza kuwa katika Wagonjwa 10 waliolazwa Hospitali kutokana na covid- 9, Wagonjwa 8 kati yao hawajapata chanjo na kwamba Wagonjwa wawili waliochanja wakipata ugonjwa hupata nafuu mapema ikilinganishwa na ambao hawajachanja.

24/12/2021

FT: Liverpool 3-3 Leicester City (Chamberlain 19’ Jota 68’ Minamino 90+5’) (Vardy 9’ 13’ Maddison 33’)

Liverpool wanafuzu nusu fainali ya Carabao Cup kwa ushindi wa penati 5-4

24/12/2021

Mama mzazi wa Bondia, Hassan Mwakinyo anayejulikana kwa jina la Fatuma Hassan Siri amefariki Dunia leo Sinza Jijini Dar es Salaam baada ya kuumwa na kulazwa Muhimbili kwa siku sita kutokana na kuwa na uvimbe tumboni.

AyoTV na millardayo.com zinatoa pole kwa Hassan Mwakinyo, Ndugu Jamaa na Marafiki walioguswa na msiba huu. 🙏🏿

24/12/2021

FT: Tottenham 2-1 West Ham (Bergwijn 29’ Moura 35’) (Bowen 32’)

24/12/2021

Mwanafunzi wa darasa la nane katika Shule ya Msingi Sikura katika Kaunti ya Busia nchini Kenya amefariki baada ya kupaliwa na kushindwa kupumua vizuri wakati akishiriki shindano la kula lililoandaliwa Shuleni hapo.

Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 16 amefariki baada ya kipande cha mkate kuingia kwenye koo la hewa na kumfanya ashindwe kupumua na akapelekwa Hospitali ya Bulwani ambako umauti ulimfika.

Mtoto huyo alikuwa ni miongoni mwa Watoto waliokua wanashindana kula mkate na soda na aliyekuwa wa kwanza kumaliza akiahidiwa zawadi, Polisi wamesema wanachunguza tukio hilo kwa undani.

24/12/2021

Watu ambao wapo kwenye hatari ya kupata HIV wataanza kuchomwa sindano ya kujikinga na virusi hivyo (Prep) hivi karibuni, hatua hiyo inakuja baada ya Marekani kuidhinisha sindano hiyo.

Sindano hiyo ambayo imepewa jina la Apretude ni sindano ya kwanza ambayo Watu wenye uwezekano mkubwa wa kupata HIV wataitumia na itatumiwa na ambao hawana HIV ili kuwakinga wasipate virusi hivyo.

Kabla ya sindano hiyo kuidhinishwa Watu walio hatarini kupata HIV k**a Wahudumu wa afya na Waathirika wa dawa za kulevya walikuwa wanameza dawa za vidonge.

24/12/2021

Mtandao unaomilikiwa na Kampuni ya China wa Tiktok umefanikiwa kushika Namba 1 kwa kutumiwa zaidi Duniani kwa mwaka 2021 huku uwepo wa Covid 19 ukiupaisha zaidi mtandao huo ambao unatajwa kutumiwa zaidi na Watu wakati wa Lockdown.

Kwa mujibu wa Cloudfare, Tiktok ambayo kwa sasa ina Watumiaji zaidi ya Bilioni 1 kote Duniani imefanikiwa kuwa juu na kuifunika hadi Google ambayo mwaka jana ilishika Namba 1.

Mwaka jana Tiktok ilikuwa Domain Namba 7 kwa kutumiwa zaidi ikizidiwa na Facebook, Microsoft, Apple, Netflix, Amazon na Google ambayo ilikuwa namba moja.

24/12/2021

PICHA: Msaidizi wa Rais (Mnikulu), Said Ali Juma akikabidhi Mbuzi, mafuta ya kupikia pamoja na mchele leo kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwenye Kituo cha Nyumba ya Amani na Furaha kilichopo Mburahati, DSM kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya.

Address

Mbeya

Telephone

+255623541107

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Udaku news posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share