19/03/2023
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe, Juma Zuberi Homera amesema mkoa wa kimadini Chunya unafanya vizuri sana katika sekta ya madini jambo linalopelekea uzalishaji wa madini kuongezeka kutoka kilograma 20 mpaka kufikia kilogramu 330 kwa mwezi ambapo zaidi ya Bilioni thelathini hupatikana kupitia sekta hiyo ya madini
Homera amesema hayo Mapema jana wakati akifunga maonesho ya kwanza ya Teknolojia ya Madini yalitofanyika kuanzia tarehe 14/03/2023 katika viwanja vya Chunya kati vilivyopo halmashauri ya wilaya ya Chunya ambayo hutambulika k**a mkoa wa kimadini Chunya
“Kwakweli Chunya mnafanya vizuri sana katika sekta ya madini kuanzia wachimbaji wakubwa na wachimbaji wadogo hakika kwakweli tunastahili kuwapongeza sana sana wanachunya wote kwa kazi kubwa mnayoifanya”
Homera amesema maelekezo aliyoyatoa Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ya kulegeza mashariti katika sekta ya uchimbaji ndiyo yanayopelekea kuwa na wawekezaji wengi wilayani chunya Huku wawekezaji wazawa kuongezeka katika sekta ya Madini
“Tumeshuhudia wawekezaji wengine wamewekeza kwenye sekta ya madini hapa wilayani Chunya, tumejionea makampuni makubwa k**a vile Ramani Investment, kina Achimwene, Kindai Investment, Sunshine, Msigwa na mengine mengi, Yote haya ni kutokana na maelekezo aliyoyatoa Mhe. Rais ya kulegeza mashariti ya kuingiza vifaa vya uchimbaji hivyo ni lazima tumpongeze sana Mweshimiwa Rais kwa kuamua kuwekeza kwenye sekta ya Madini”
Kwakukumbuka kifo cha Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. Dkt John Joseph Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya amewaongoza wananchi waliojitokeza katika maonesho hayo kutulia kwa dakika moja ikiwa ni ishara ya kumkumbuka, kuenzi na kumwombea kheri apumzike kwa amani huko aliko