Kingsport news

Kingsport news believe in God
football for life
game to game
update sports in God believe

Life is the journey 💪💪
15/12/2025

Life is the journey 💪💪

CHAMA MCHEZAJI WA DARAJA LA JUU"Chama ana Dunia yake, sio mchezaji wa kumzungumzia kirahisirahisi tu. Chama hatakiwi kuw...
13/10/2022

CHAMA MCHEZAJI WA DARAJA LA JUU

"Chama ana Dunia yake, sio mchezaji wa kumzungumzia kirahisirahisi tu. Chama hatakiwi kuwekewa bato na mchezaji yoyote wa kwenye ligi yetu kwasababu ni mchezaji wa daraja la juu sana, mimi napenda sana style yake ya kucheza" Makame, Shabiki wa Yanga SC.

Ibenge, Klabu ya Simba Sc ni timu ambayo mnapokutana katika michuano ya CAF ni ngumu sana kuisoma mbinu zao kwakuwa mpir...
03/09/2022

Ibenge, Klabu ya Simba Sc ni timu ambayo mnapokutana katika michuano ya CAF ni ngumu sana kuisoma mbinu zao kwakuwa mpira inoucheza katika Ligi yao wanapokutana na mtani wao Yanga, Ni mpira tofauti na ule wanaoucheza katika michuano ya CAF

Makocha wengi huwa wakishindwa kuisoma Simba Sc katika michuano ya CAF kwakuwa huwa wakiitazama Simba ikicheza katika Ligi yao kumbe mpira inaoucheza katika Ligi yao ni robo ya mpira ambao watamchezea mpinzani huku katika michuano ya CAF

Kuisoma Simba Sc angalia mechi zao za CAF unaweza fanikiwa ila ukiaangalia akicheza na mtani wao Yanga ujuwe umefungwa,

ANAANDIKA ALLY KAMWE.Mambo 10 nilioyaona SIMBA vs KAGERA1: WOW. JUST WOW .. WHAT A MATCH🙌 TUMEENJOY SOKA. Siku zote, Mec...
20/08/2022

ANAANDIKA ALLY KAMWE.

Mambo 10 nilioyaona SIMBA vs KAGERA

1: WOW. JUST WOW .. WHAT A MATCH🙌 TUMEENJOY SOKA. Siku zote, Mechi ya wazi, Mechi isiyokuwa na mitego, Mechi isiyokuwa na mipango mingi ya kukaba.. Ni Burudani kwa watazamaji wa Soka

2: POINTI 6. Mabao 5. CLEAN SHEET 2 Mfululizo.. Kubwa zaidi ‘Lete Mzungu’, Dejan Georgijević Ameleta Burudani.. What A Moment.. Mashabiki wa Simba wapewe Ulinzi😀

3: Tactically, Kocha wa Simba, Zoran Maki ni sawa Kilema aliyejua mwendo upi sahihi kwake.. Hana kiungo mzuri mkabaji.. Nini unafanya? Wekeza nguvu kwenye kushambulia

4: Simba wana wachezaji wazuri sana kwenye 1v1 .. Babu Zoran amechagua kuanza na Kanoute chini, kisha kuweka watu watano mbele wenye akili ya kushambulia.. Hapa anatega mpinzani kulazimisha kufungua mchezo. Kivipi?

5: Ni rahisi kufika kwenye 18 ya mwisho. Ukienda mara moja, ukirudia mara mbili.. Ujumbe unaokwenda kwa koch wa timu pinzani ni kupunguza tahadhari na kutamani kushambulia zaidi.. Mechi ikiwa hivi, QUALITY HUAMUA✅

6: CHAMA NI SANAA YA SOKA! Anachoweza kufanya Rutto kwenye Jukwaa la Siasa, Chama anaweza kukifanya mara mbili yake uwanjani.. Ni mjuzi. Mtaalam. Anakupa usichokitarajia🤝 ASANTE CHAMA

7: ‘Finishing’ nzuri kwa Dejan.. Mwili wake ulimfanya dhambi ya uongo kwa golikipa. Alidesh kulia akageuka kushoto.. Kamba nzuri na mguu wa kushoto.. Hii itampa kujiamini zaidi

8: Bado Simba inawadai zaidi BANDA na SAKHO.. Wana kasi, skills nzuri za kuvamia eneo la mwisho Lakini Maamuzi yao bado sio sahihi kwenye kuamua mchezo

9: Well Done kipa wa Kagera👏 Licha ya kosa la mawasiliano kati yake na mabeki, alikuwa na mechi bora sana kwenye Saves. Utulivu mkubwa sana kwenye Timing zake kuhesabu hatua za mastraika

10: Asante Outtara! BEKI WA SOKA. Asante Kanoute.. Well Play Makame.. Asante pia Beki Laurent.. Kagera wana Timu nzuri sema wamepata ratiba ngumu mwanzoni

Nb: Mzungu ahesabiwa kwenye SENSA 😀

Mpaka sasa sijaona kiungo bora No 10 zaidi ya Clatous Chama TZ. Kuna wachezaji wenye vipaji lakini ni marufuku kumweka m...
17/08/2022

Mpaka sasa sijaona kiungo bora No 10 zaidi ya Clatous Chama TZ. Kuna wachezaji wenye vipaji lakini ni marufuku kumweka mchezaji yoyote kwa sasa kwenye daraja la Chama. Nipo tayari kwenda mahak**ani kumfungulia mashtaka yeyote yule atakayekiuka maagizo Haya.

🔍 𝗣𝗿𝗶𝘃𝗮𝗹𝗱𝗶𝗻𝗵𝗼

𝗠𝗔𝗠𝗕𝗢 10 𝗔𝗡𝗜𝗟𝗜𝗢𝗬𝗔𝗢𝗡𝗔 𝗦𝗜𝗠𝗕𝗔 𝘃𝘀 𝗚𝗘𝗜𝗧𝗔1: POINTI 3. MABAO 3 .. CLEAN SHEET ✅ SIMBA ARE BAAACK🦁 Ushindi wenye Faida kubwa kwe...
17/08/2022

𝗠𝗔𝗠𝗕𝗢 10 𝗔𝗡𝗜𝗟𝗜𝗢𝗬𝗔𝗢𝗡𝗔 𝗦𝗜𝗠𝗕𝗔 𝘃𝘀 𝗚𝗘𝗜𝗧𝗔

1: POINTI 3. MABAO 3 .. CLEAN SHEET ✅ SIMBA ARE BAAACK🦁 Ushindi wenye Faida kubwa kwenye kujenga hali ya kujiamini kwenye kikosi..👍

2: ZORAN ni k**a alisubiri kuiona Geita mpya inavyofanana. Alivyowaona, akawasha Taa Nyekundu. ‘SUB’ iliyobadili mchezo ni ile ya Mkude kuingia OKRAH.. Kwanini?

3: Geita walikuwa na mpango wa kuzuia kwenye Mid Block wakiwa kwenye umbo la 4-4-2 .. Lakini baadae wakabadili kwenda kwenye Low Block [Kukabia chini] .. Hapa ndipo Zoran aliporusha karata yake kwa kuleta mtu anayeweza kutembea na mpira na sio kupiga pasi

4: OKRAH ana uwezo mkubwa wa kuficha mpira akikimbia. Kasi yake ilikuwa silaha ya kuivunja Line ya 2 ya ulinzi ya Geita kuvamia eneo la Tatu la mwisho la uwanja.. Mkude & Chama Simba ilipiga pasi.. OKRAH AKALETA KASI 🙌

5: Sub ya Okrah ni k**a ilipeleka ujumbe kwa Minziro kuwa sasa mchezo uko wazi. Simba katikati wana kiungo mmoja tu mwenye uwezo wa kukaba.. Kanoute pekee. Nini alifanya Minziro?

6: Akadandia mtumbwi wa vibwengo! Akamtoa Okoyo na kumleta Chikola. Geita nao wakaufungua mchezo! QUALITY IKATAKIWA KUAMUA MCHEZO! Faida ikawa kwa Simba hapa

7: CHAMA.. WHAT A PLAYER🙌 Ile ni Sanaa ya Soka. Mpira uko kichwani mwake, mguuni ni maamuzi✅ Kwenye nusu nafasi bado anaweza kunusa hatari kwa mpinzani.. ASISTI YA KWANZA MSIMU HUU🤝

8: GEORGE MPOLE & LYANGA walipoteza ‘Link’ yao! Walicheza kwa presha kubwa na kushindwa kutumia Faida ya Edmund John uwanjani.. Henock alipovutika upande wa kushoto, Mpole na Lyanga walitakiwa kuiona hio k**a faida kwa kutengeneza movements nyuma yake

9: PETER BANDA anajua boli. Nimependa pia jituhada za Sakho.. Rudi tena litazame bao la Phiri.. Utaona rahisi namna alivyofunga Lakini ile Movement aliyoifanya inakupa jibu ni mtu hatari kiasi gani

10: Kelvin Nashon 👏 Kipa wa Geita anatakiwa kuongeza umakini zaidi.. Mechi kubwa huwa zinaamuliwa na details ndogondogo sana!

Nb: Chama mmoja ni sawa na ……😀

TUJIFUNZE KUUKUBALI UKWELII💥💥💥Moja ya jambo gumu sana kwetu waafrika ni kuukubalii ukweliii ila sio kazi.....Wanasimba t...
14/08/2022

TUJIFUNZE KUUKUBALI UKWELII💥💥💥

Moja ya jambo gumu sana kwetu waafrika ni kuukubalii ukweliii ila sio kazi.....

Wanasimba tukubali jambo tuna timu bora sana ila siku ya jana haikuwa nzurii hasa kwa upande wetu....
Pongezi kwa Wananchiiiiii wamefanya kitu kizurii sana... Kocha wa Simba kuna kitu amekiongeza sana kweny timu ya Simba...

Nabi ni Master plan yeye ndio alikuwa game changer.. ✔️

Nimeondoka na jina na Aziz Ki
Pale Simba nimeondoka na Jina Outarra

Mayele na Sakho hao hawahitaji maneno kuwaelezea🖐️

Kuna namna hizi timu msimu huu zitasumbua sana kiukwelii hawa mapacha msimu huu watashindikanika😁

Nb.. Taratibu tunatoka kwenye uchawi, hujuma na ushirikina tunaenda kwenye ubora na watu wanaufata na kuuelewa...

💥Kinachomhukumu Dejan Georgijevic ni rangi yake nasio uwezo wake.Kinachomhukumu zaidi ni ushamba wetu na sio kipaji chak...
14/08/2022

💥Kinachomhukumu Dejan Georgijevic ni rangi yake nasio uwezo wake.

Kinachomhukumu zaidi ni ushamba wetu na sio kipaji chake!

Unaweza usinielewe na sio lazima unielewe...

Wengi wanapoona rangi yake wanategemea makubwa kutokana na waafrika kutawaliwa kifikra na wazungu...wengi tunaamini wazungu ni daraja la kwanza!

Watu wanategemea akiingia uwanjani akipata mpira atapiga chenga wachezaji wote mpaka afunge bao.
Yees... ushamba wetu uko hapo!!

Watu wanasahau Mohamed Salah na Heung-Min Son wametwaa Golden Boot mbele ya wazungu wengi tu pale kwenye ardhi ya Malkia.

Wanasahau Samuel Eto'o na Didier Drogba walifunga mabao mengi mbele ya mabeki wa Kizungu.

Ukitaka kuamini ushamba wetu ulipo zaidi...wanaosema Dejan hamna lolote hawakuambii kapata nafasi ngapi akashindwa kufunga.
Hawasemi kapewa pasi ngapi kashindwa kuzitendea haki.

Mashabiki wanataka kwakuwa Dejan ni Mzungu basi huyo huyo adake,azuie,apige kros na huyo huyo akafunge sio?

Ninachojua mimi... Ni mapema mno kumhukumu Dejan kwamba hajui.

Tulivyoweka akiba ya maneno kwa Aziz Ki kwenye mechi dhidi ya Vipers tuendelee kumsubiri Dejan.

Anaweza kuthibitisha ubora wake k**a alivyofanya Aziz Ki jana ama akawa Danny Sserunkuma... Nyakati zitaamua!

✍️credit by Sospeter Ilagila.

Ameandika  Welcome Back NBC PL Yanga SC wanashinda mechi ya pili mfululizo ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba SC huku Fisto...
13/08/2022

Ameandika

Welcome Back NBC PL

Yanga SC wanashinda mechi ya pili mfululizo ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba SC huku Fiston Mayele akifunga magoli yote ya Yanga ya ushindi katika hizo mechi

Simba SC walianza mechi vizuri sana, pressing , sharp , maamuzi sahihi kwa wakati sahihi na kuwaweka Yanga kwenye presha kubwa sana . Hasa matumizi ya utatu kwenye kiungo . How ??

1: Mkude na Kanoute hawakuwa katika mstari mmoja wa katikati bali Mkude alikuwa chini sana karibu na mabeki wawili wa kati akitengeneza pembe tatu

2: Kanoute alikuwa anafanya movement za kwenda mbele zaidi ( forward runs ) sababu kuu ni kuvunja mstari wa viungo wawili Sureboy na Aucho ili kutengeneza space kwa Chama Jr kupokea mpira akiwa huru na kutengeneza nafasi

3: Kilichoiangusha Simba ni movement za Kyombo hazikuwa sahihi kwa wakati sahihi kiasi kwamba kuna muda walikuwa wanachelewasha pasi ya mwisho

Kazi kubwa ya Nabi kuona tatizo na kufanya maamuzi wakati wa mapumziko . Tunasema mchezeshe mchezaji wako bora katika nafasi sahihi ambayo atakuwa mfanisi ... Nani na kivipi ?

1: Kumrudisha Feisal kwenye kiungo cha kati akiwa na Aucho na kumpeleka Aziz Ki katika kwenye namba 10 ... why Ki kwenye namba 10 ?

2: Kwasababu mstari wa kiungo wa Simba unapenda kuzuia mtu badala ya kuzuia space iliyowazi , na Aziz Ki anajua sana kuiona nafasi na kuitumia nafasi , na hatari yake ni kwamba hatumii muda mrefu kwenye mpira anaiona picha nzima ya kila kitu kinachoendelea

Nafikiri k**a Yanga watajua nini anaweza , na nini hatari yake Aziz Ki , basi ni muda wa viungo wake wengine kuachia pasi haraka na mbele yake anahitaji movement zaidi kwenye shape ya 4-2-3-1 ambayo Nabi anaipenda

NOTE

1: Inonga ana bahati sana kumaliza mechi, alikuwa anafikiri nini ? Hata sijui .

2: Tatizo la Simba la kutokuwa na namba 6 halisi , limeonekana tena dhidi ya namba 10 halisi

3: Pasi nzuri ya Chama Jr , na umaliziaji mzuri wa Sakho 🔥

4: Fiston Mayele kasi na movement zake ni hatari sana k**a atakuwa analishwa mapema ... 🔥 angeweza kupiga Hat trick leo

5: STEPHANE AZIZ KI .... hakukuwa na majibu dhidi yake ... BEST PLAYER ON THE PITCH BAR NONE 🔥

Full Time : Yanga SC 2-1 Simba SC

ANAANDIKA ALLY KAMWE.Mambo 10 nilioyaona YANGA vs SIMBA1: DAR ES SALAAM IS GREEN & YELLOW ✅ BEAUTY BEAUTY…  YANGA BINGWA...
13/08/2022

ANAANDIKA ALLY KAMWE.

Mambo 10 nilioyaona YANGA vs SIMBA

1: DAR ES SALAAM IS GREEN & YELLOW ✅ BEAUTY BEAUTY… YANGA BINGWA TENA🏆 Kuna Raha kubeba Ubingwa, Halafu Kuna Raha ya Kubeba Ubingwa kwa kumfunga Mtani. WANANCHIIIII…🗣🗣

2: YANGA WAMESHINDA KIKUBWA mbele ya SIMBA. MAYELE AMESHINDA MECHI YAKE KIBABE MBELE YA INONGA✊ What A Player. What A Moment. KING MAYELE AMEIAMUA TENA NGAO YA JAMII🙌

3: TACTICALLY, NABI alikosea Dakika 45 za kwanza. Akapatia Dakika 45 za pili. Kivipi? Role ya Aziz Ki sio wa kucheza pembeni.. He is The Best kwenye Zone ya 14. Kwenye 4-2-3-1, Aziz kuwa pembeni kuliifanya Yanga ikose Balance walipokosa mpira huku Sure Boy na Aucho wakivutika kwa pamoja Simba walipokuwa wakifanya Build Up. Ikawa rahisi kwa CHAMA kupokea mpira nyuma ya mgongo wao.

4: Dakika 45 za pili, AZIZ KI alirudi k**a namba 10. Fei akashuka chini. Morrison na Moloko wakaja kuwapa Yanga uhai kwenye mapana ya Uwanja. Tactically hapa Nabi akauridisha mchezo kwenye mkono wake, huku ZORAN akifanya makosa mawili kwa upande wake. Yapi?

5: Sub ya Chama. Labda k**a kuna shida ya Fitness lakini sio OKWA wala OKRAH anayefikia uelewa wa Mbinu wa Chama. Usahihi wa pasi na Utulivu kwenye boksi la mpinzani. Bado Okwa na Okrah hawajapata ‘Link’ nzuri kati yao

6: Kosa la pili ni ile Sub ya Kanoute. Kwanini? Kanoute alikuwa sharp na alireact haraka kunasa pasi za hatari za Yanga. Viungo wa Yanga walisumbuka sana kuona njia ya kujenga shambulizi Kanoute alipokuwa katikati

7: AZiZ KI ANAJUA BOLI.. Ana maamuzi sahihi kwa wakati sahihi. K**a akielewana zaidi na Mayele pale juu, yale maelekezo yote aliyokuwa anayatoa kabla ya kupiga pasi, yatageuka kuwa mabao

8: Kwa mujibu wa Sheria namba 12 [Fouls and Misconduct] Henock hakustahili kuzimaliza Dakika 90. It was a serious Foul play iliyohatarisha usalama wa mchezaji mwenzake. ILISTAHILI KUWA KADI NYEKUNDU

9: Ouattara ni kitasa cha maana. Changamoto ni Henock kukubali kuwa namba 4. Lazima kuwe na kiongozi kati yao. Kuna makosa kiasi ya mawasiliano kwenye safu ya ulinzi

10: Well Done Kanoute👏 Well Done Dickson Job. Nafikiri Bangala ana faida zaidi kiufundi akicheza kati kuliko beki wa kati

Nb: Yule Mzungu ni ‘Mandonga Mweupe’😀

Nelson Okwa rasmi atambulishwa Simba 🔥🔥🔥🔥
03/08/2022

Nelson Okwa rasmi atambulishwa Simba 🔥🔥🔥🔥

🇳🇬 Nelson Okwa (28) is on his way to Tanzania. ✈️🇹🇿Okwa is currently in Ethiopia 🇪🇹 He will arrive at 03:10. 🚨In Swahili...
02/08/2022

🇳🇬 Nelson Okwa (28) is on his way to Tanzania. ✈️🇹🇿

Okwa is currently in Ethiopia 🇪🇹

He will arrive at 03:10. 🚨

In Swahili:

nelson Okwa (28) yuko njiani kuelekea Tanzania.

Kwa sasa Okwa yuko Ethiopia

Atafika saa 03:10.

I

Credit Mick JnR

Address

Mbeya

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kingsport news posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share