MAWIO TZ

MAWIO TZ Karibu katika ukurasa huu maalumu wa MAWIO TZ, unaokuhabarisha Taarifa/Habari na Makala mbalimbali ndani na nje ya Tanzania ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

Wananchi 412 wapata huduma ya vipimo vya afya bure St.Joseph Ikelu, Makambako NJOMBE, Serikali yaombwa kupunguza Kodi Se...
04/05/2025

Wananchi 412 wapata huduma ya vipimo vya afya bure St.Joseph Ikelu, Makambako NJOMBE, Serikali yaombwa kupunguza Kodi

Serikali imeombwa kuzipunguzia kodi hospitali zinazo milikiwa na taasisi za dini ili kurahisisha uendeshaji kwa kuwa hazijaanzishwa kwa lengo la kufanya biashara zaidi ya kutoa huduma kwa wananchi kutimiza takwa la kanisa kutoa huduma ya kimwili na kiroho.

Wito huo umetolewa na Pandre Inocent Chaula ambaye ni katibu wa afya na katibu wa Mhashamu Askofu Ausebius Kyando Jimbo Katoliki la Njombe wakati wa maadhimisho ya Jubilei kuu ya Ukristo 2025 iliyofanyika katika hospitali ya St.Joseph Ikelu iliyopo halmashauri ya mji wa Makambako.

"Hospitali imeletwa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi na sio biashara tuombe tusaidiane katika huduma hizi,tunapata changamoto ya katika uendeshaji michango mingi,kodi nyingi sasa tuwaombe viongozi wa serikali mliopo mtusemee k**a kituo cha huduma na sio biashara"amesema Padre Chaula

Amesema "Kanisa linamuhudumia mtu kimwili na kiroho kwa miaka hii ya karibuni sisi sekta binafsi hasa za makanisa tunaonja ukali huo hivyo basi tuiombe serikali iwe inatufikiria katika jambo hilo na pia ugumu katika mambo ya bima kwasababu vifurushi vya bima vilivyoletwa kidogo vinakandamiza mtoa huduma"

Amewataka wahudumu wa afya kuwa chachu ya matumaini kwa wagonjwa ambapo pia amepongeza hospitali kwa kutoa huduma za uchunguzi wa afya bure kwa wananchi 412 huduma iliyotolewa siku mbili hospitalini hapo.

Awali akisoma taarifa ya wafanyakazi wa hospitali hiyo Dkt.Policap Nyengela amesema licha kazi kubwa ya utoaji wa huduma inayofanywa ikiwemo za kibingwa lakini wanakabiliwa na changamoto za ukosefu wa vipimo vikubwa hususani MRI vipimo ambavyo vingeweza kusaidia kupunguza safari za kusafirisha wagonjwa sehemu nyingine kufuata kipimo hicho.

Nao baadhi ya wananchi akiwemo Hanipher Malekela na Osmond Mkungilwa waliofika kwa ajili ya kufuata huduma katika hospitali hiyo wameshukuru kwa huduma zinazotolewa huku wakiomba watumishi kuto vunjika moyo kwenye utumishi wao.

"Kazi hii ni wito kwa hiyo wawe na moyo huo wa kujitolea wala wasivunjike mioyo kutokana na Changamoto hasa za wagonjwa kwa kuwa mgonjwa anafika hospitali akiwa na matarajio yake"

Kwa mujibu wa katibu wa afya na katibu wa Mhashamu Askofu Ausebius Kyando amesema kuwa Askofu amepokea changamoto na yuko tayari kushughulikia zilizopo katika mamlaka yake na kwenda kuzisemea nyingine katika mamlaka za ngazi ya juu.

Baadhi ya Jumbe Katika Maadhimisho ya Siku ya WAFANYAKAZI DUNIANI 2025 (MEIMOSI) Ambayo Kitaifa yamefanyika SINGIDA na k...
01/05/2025

Baadhi ya Jumbe Katika Maadhimisho ya Siku ya WAFANYAKAZI DUNIANI 2025 (MEIMOSI) Ambayo Kitaifa yamefanyika SINGIDA na kuhudhulia na Viongozi wengi wa Serikali wakiongozwa na Rais Samia Suluhu
:
Endelea Kufuatilia Mawio Tz na Usisahau Ku-subscribe Kwenye Channel yetu ya YouTube MAWIO TZ tukujuze kwa Undani zaidi

Leo 1 May 2025, (MEI MOSI) katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi, Walimu wa Mkoa wa SINGIDA wamejitokeza wakiwa wame...
01/05/2025

Leo 1 May 2025, (MEI MOSI) katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi, Walimu wa Mkoa wa SINGIDA wamejitokeza wakiwa wamebeba Mabango yenye Ujumbe Muhimu wa Pongezi kwa MKUU WA MKOA wao.

Endelea Kufuatilia Mawio Tz na Usisahau Ku-subscribe Kwenye Channel yetu ya YouTube MAWIO TZ kwa Habari na Makala Kemkem

Kilio cha walimu Manga kutembea KM 24 kuifuata shule kufika mwisho,TASAF wajenga nyumba ya kisasaKufuatia changamoto ya ...
01/05/2025

Kilio cha walimu Manga kutembea KM 24 kuifuata shule kufika mwisho,TASAF wajenga nyumba ya kisasa

Kufuatia changamoto ya kukaa umbali wa takribani KM 24 wanayokumbana nayo walimu wa shule ya msingi Deo Sanga iliyopo katika kijiji cha Manga halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe.

Hatimaye Changamoto hiyo inaelekea kupunguzwa kwa kiasi kikubwa mara baada ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa kushirikiana na wakazi wa kijiji hicho kukamilisha nyumba pacha yenye thamani ya Tshs 92,410,714.29

Akitoa taarifa ya ujenzi wa Nyumba hiyo mbele ya Mwenyekiti wa k**ati ya uongozi ya Taifa ya TASAF Peter Ilomo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi,Liston Ngimilanga ambaye ni afisa Mtendaji wa kijiji cha Manga amesema ujenzi wa nyumba hiyo umefikia hatua ya umaliziaji ambapo mradi huo mpaka sasa umegharimu Shilingi 91,360,714.29

"Katika kuhakikisha huduma bora zinatolewa kwa wananchi wa kijiji cha Manga,kijiji kilipokea fedha hizo kutoka serikali kuu kupitia TASAF kwa ajili ya ujenzi wa nyumba pacha na hii ni baada ya wananchi kuibua na kuthibitisha mradi"amesema Ngimilanga

Awali Mwalimu Naboti Ilongo kutoka shule hiyo amesema mpaka sasa shule hiyo ina nyumba nne lakini mahitaji yao ni nyumba saba hivyo mara baada ya ujenzi wa nyumba hiyo kutakuwa na mahitaji ya nyumba moja kwa walikuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya walimu kutoka mjini Makambako wakifanya kazi katika shule hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa k**ati ya uongozi ya Taifa ya TASAF Peter Ilomo amesema serikali imetoa kiasi hicho ili kuunga mkono juhudi za wananchi wa Manga na kupongeza kwa usimimizi wa mradi huo.

"Jengo ni zuri na hata umaliziaji wake umefanyika kwa umahili mkubwa,na kwa kweli niwashukuru CMC kwa kusimamia hii kazi na nina imani mwezi ujao mtakuwa mmemaliza hii kazi"amesema Ilomo

Ahsanteni sana Wapenzi Watazamaji Mnaotufuatilia Kwenye Channel yetu ya YouTube ( MAWIO TZ) na Mitandao ya Kijamii ๐Ÿ™๐Ÿ’“๐Ÿซ‚Fa...
11/04/2025

Ahsanteni sana Wapenzi Watazamaji Mnaotufuatilia Kwenye Channel yetu ya YouTube ( MAWIO TZ) na Mitandao ya Kijamii ๐Ÿ™๐Ÿ’“๐Ÿซ‚

Familia inazidi kukua, Sasa Rasimi tumefikia Wafuatiliaji zaidi ya 60,000 Kwenye Channel yetu ya YouTube kwa jina la MAWIO TZ (Zamani Busokelo TV)

Tuwashukuru pia Watazamaji wetu Mnaotupa maoni yenu chanya kwa Maendeleo ya hiki Chombo chenu pendwa, tunaahidi kutowaangusha kwa kuwaletea Habari, Makala za Uhakika na Ukweli bila kuegemea Upande wowote.

K**a Bado Nenda Subscribe kwenye Channel yetu, nawe uwe miongoni mwa wengi wanotufuatulia ili kupata Habari na Maka

31/12/2024

TAARIFA KWA UMMA
31/12/2024

TAARIFA KWA UMMA

30/12/2024

Shamlashamla za Mkutano wa Busokelo Pamopene unaoendelea katika ukumbi wa shule ya sekondari Lwangwa katika halmashauri ...
28/12/2024

Shamlashamla za Mkutano wa Busokelo Pamopene unaoendelea katika ukumbi wa shule ya sekondari Lwangwa katika halmashauri ya Busokelo,Mkutano huo.umelenga kujadili musuala ya Maendeleo.

SERIKALI YA RAIS SAMIA KUWACHUKULIA HATUA WATAKAOBAINIKA KUCHELEWESHA UJENZI JENGO LA WAZAZI UKEREWE Serikali ya Jamhuri...
27/12/2024

SERIKALI YA RAIS SAMIA KUWACHUKULIA HATUA WATAKAOBAINIKA KUCHELEWESHA UJENZI JENGO LA WAZAZI UKEREWE



Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo kumpeleka Mkaguzi wa ndani wa Mkoa kukagua mwenendo wa utekelezaji wa ujenzi wa Jengo la wazazi katika Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe kabla hajachukua hatua kwa wazembe watakaobainika.

Hatua hiyo imekuja kufuatia Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia, kuwataka Watumushi wa Serikali kusimamia Sekta ya Afya, kutokana na jitihada za Rais kuwekeza nguvu nyingi katika kuboresha mazingira katika Sekta hiyo muhimu.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda, mapema Ijumaa 27 Disemba, 2024 alipotembelea Hospitalini hapo, kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la wazazi na kubaini kuna ucheleweshaji wa miezi sita, kinyume na mkataba na kuagiza , ujenzi huo ukamilike ndani ya siku 20.

โ€œSerikali imeleta Milioni 900 kwenye Hospitali hii kwa ajili ya kujenga wodi muhimu ya wazazi ili kuboresha huduma bora za afya kwa Wananchi na kuboresha hali ya utoaji huduma hivyo wasimamizi hampaswi kukwamisha juhudi hiziโ€. Mtanda.

Ameongeza kuwa, inashangaza kuona fedha zimeshafika tangu mwezi Machi mwaka huu na walipaswa kukamilisha ujenzi mwezi Juni lakini ni Milioni 700 pekee zimelipwa kwa mafundi ikiwa ni asilimia 85 ya fedha zote na kusababisha kuchelewesha ujenzi huo.

Aidha, ameelekeza mzabuni wa milango kwenye Hospitali hiyo ahakikishe anakabidhi mara moja ili iweze kuwekwa na kukamilisha ujenzi na kuhusu majengo yaliyoandaliwa kufanya upanuzi, ameahidi kuwasiliana na Wizara ili kuhakikisha fedha zinaletwa kukamilisha ujenzi.

* *

Address

Mbambo
Mbeya
53525

Telephone

+255676506998

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when MAWIO TZ posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to MAWIO TZ:

Share