
14/04/2025
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imetangaza kuanzia mwezi July mwaka huu imeaandaa mpango wa usajili na utambuzi wa Watu wote wenye umri kuanzia 0 hadi miaka 18 ili kuwezesha upatikanaji wa Jamii Namba pamoja na wageni wote wanaoingia nchini na kukaa chini ya miezi sita.
Mkurugenzi Mkuu wa NIDA,James Kaji amesema hayo leo April 14,2025 Jijini Dar es salaam huku akisema dhamira yao na Seriiali kwa ujumla ni kuona kila Mtanzania anapata kujulikana na kufikiwa na huduma za msingi zikihitajika na kila kitambulisho kilichotengenezwa kinachukuliwa na Mhusika na hasa ikizingatiwa Serikali imetumia fedha nyingi kutengeneza.
Kaji amesema kuanzia May 01, 2025 NIDA itasitisha rasmi matumizi ya Namba ya Utambulisho wa Taifa (NINs ) kwa wote ambao walitumiwa ujumbe mfupi wa simu ya mkononi (sms) lakini hawakujitokeza kuchukua vitambulisho vyao na kwamba yule ambaye matumizi ya namba yake ya NIDA yatafungwa hatoweza kuitumia namba hiyo kwa ajili ya huduma yeyote.
Kaji amesema tangu kuanza kwa zoezi hilo kuanzia mwezi January hadi kufikia March mwaka huu jumla ya Wananchi 1,88060 sawa na asilimia 157 ya Wayu wote walikuwa hawajachukua vitambulisho vyao licha ya kutumiwa ujumbe mfupi (sms) “Kwa mujibu wa takwimu hizi idadi ya Wananchi waliojitokeza kuchukua vitambulisho baada ya kupokea sms ni 565,876 sawa na asilimia 30 tu ya Watu wote waliotumiwa na kupokea sms”