Onemoja maarifa

Onemoja maarifa History,news,entertainment and business

Hii ndio ilikuwa Bendera yetu, Na Katikati ya bendera ni Ngao ya Jamii (Coat of arms) ya Nchi yetu enzi tunaitwa Deutsch...
24/12/2024

Hii ndio ilikuwa Bendera yetu, Na Katikati ya bendera ni Ngao ya Jamii (Coat of arms) ya Nchi yetu enzi tunaitwa Deutsch-Ostafrika (Ujerumani ya Afrika Mashariki) miaka ya 1885 mpaka 1918.

Wakati huo nchi ilikuwa na Eneo la Mita Square 994,996 Km² ndani yake kuna Burundi na Rwanda, na Eneo la Nchi ya Msumbiji lililoitwa Kionga Triangle.

Je wajua Neno La Kiswahili "Shule" limetoka kwenye Neno la Kijerumani "Schule" yote yakimaanisha "School"

Maeneo Mengine yaliitwa hivi:

• Rombo iliitwa Fischerstadt
• Nyakanazi iliitwa Friedberg
•Kisarawe Iliitwa Hoffnungshöh
•Tukuyu iliitwa Langenburg
•Ushetu iliitwa Marienthal
•Shume (Huko kwa Wapare) kuliitwa •Neu-Hornow
•Mbulu Kuliitwa Neu-Trier
•Sekenke Paliitwa Sachsenwald na ilikua ni Mgodi.
•Lushoto iliitwa Wilhelmsdorf.

Kipindi hiki ndio Tulijengewa Reli iliyoitwa Usambara Railway mwaka 1891 Ilijengwa na Wajerumani na ilikua na Km 350, Ilianzia Mjini Tanga, Ikawa na Makutano Na Kenya Mji wa Kahe, Ikapita Moshi mpaka Arusha.

Wajerumani Katika Reli hii walikua na Vichwa vya Treni 18 (Locomotive) na mabehewa 199, Kipindi hicho Reli hii ilikua na Wafanyakazi 562 huku kati yao 35 tu ndio Walikua Wajerumani.

Lengo la Wajerumani kujenga Reli hii ilikua ni Kuunganisha Bandari ya Tanga na Ziwa Victoria kupitia milima ya Usambara.

Treni la Kwanza Lilipita Likiwa Tupu Tarehe 26 September 1911 ili kujaribu Safari na Kufanikiwa 100%, Likapita tena likiwa na Abiria Tarehe 4 October 1911 na kufanikiwa 100% Wajerumani wakaamini Kweli Kitu ni Konki.

Hivyo ukafanyika uzinduzi wa Reli Tarehe 7 February 1912, Na Baada ya Hapo Treni lilikua lazima lifanye safari Kila siku Kutoka Tanga mpaka Buiko na Kurudi, Safari ilichukua Muda wa masaa 14 na dakika 40.

Reli hii haikukamilika Mpaka Arusha sababu ya Vita ya Kwanza ya Dunia, Waingereza ndio Wakaiunganisha.



Ake Ronaldooh

I've received 1,000 reactions to my posts in the past 30 days. Thanks for your support. 🙏🤗🎉
14/07/2024

I've received 1,000 reactions to my posts in the past 30 days. Thanks for your support. 🙏🤗🎉

Wananchi waungana kuzuia mapinduzi ya kijeshi Bolivia.🇧🇴K**a kuna sehemu hii kitu imewahi tokea naomba mniambie,lakini h...
27/06/2024

Wananchi waungana kuzuia mapinduzi ya kijeshi Bolivia.🇧🇴

K**a kuna sehemu hii kitu imewahi tokea naomba mniambie,lakini hii inapaswa kuwa ushindi mkubwa sana wa demokrasia duniani.

Bolivia ni nchi iliyopo Amerika kusini,inapakana na nchi kadhaa k**a Brazil🇧🇷 upande wa mashariki,Peru 🇵🇫 upande wa magharibi na Paraguay 🇵🇾 upande wa kusini.

K**a ilivo kwa nchi nyingi za ukanda huu wa bara la Amerika,,nyingi zimepitia utawala wakimabavu wakijeshi kwa miaka mingi na uchungu wa aina hiyo ya utawala wanaujua.

Mkuu wa Jeshi Juan José alimkosoa vikali rais wa nchi hiyo bw Moralés kwenye interview aliyoifanya siku kadhaa nyuma ambayo ilionyesha dhahiri mpango wake wakutaka kuipindua serikali kwa kisi gizio chakuwa anataka kurekebisha mfumo wa demokrasia nchini humo,na baada ya hapo Rais alimtaka José kutoka katika nafasi yake baada ya kumkosoa rais wa nchi lakini aligoma na ndipo kuamua kuchukua vikosi vya jeshi na kuingia mtaani na kwenda kuiteka ikulu.

Rais Moralés alilihutubia taifa akiwa ndani ya Ikulu na kuwaomba wananchi waungane kupinga mapinduzi hayo ili kuunga mkono demokrasia.

Wananchi walijitokeza kwa maelfu kisha kuandamana kuelekea ikulu ambako waliwashinda nguvu wanajeshi hao ma kupelekea bw José kuk**atwa na mapinduzi hayo kufeli.

Kabla ya sasa rais huyo alishawahi kutolewa madarakani mwaka 2019 na kukimbilia Mexico ambako Jeshi lilitoa sababu kwamba walifanya mapinduzi hayo kutokana na rais kutaka kufanya uchakajuaji wa kura kitu ambacho kilipingwa na rais huyo.

Alirejea mwaka 2020 ambako ulifanyika uchaguzi na akashinda tena ambako alihudumu hadi sasa.

Tutaendelea zaidi post inayokuja.

Follow page yetu

Nchi zinazoongoza kwa kupokea misaada ya kigeni Afrika.1. Misri - $7.7 billion2. Ethiopia - $5.3 billion3. Nigeria - $5 ...
27/06/2024

Nchi zinazoongoza kwa kupokea misaada ya kigeni Afrika.

1. Misri - $7.7 billion

2. Ethiopia - $5.3 billion

3. Nigeria - $5 billion

4. DR Congo - $3.4 billion

5. Kenya - $3.3 billion

6. Tanzania - $3 billion

7. Mozambique - $2.9 billion

8. Morocco - $2.6 billion

9. Uganda - $2.4 billion

10. Niger - $2.2 billion

Chanzo;IMF

FOLLOW PAGE YETU

Huyu jamaa anakuja Bongo kuupanda mlima Kilimanjaro.🔥🔥🔥😜😜Kashaupanda wa Mobetto 😅😅 anataka kupanda Kilimanjaro sasa😁Foll...
27/06/2024

Huyu jamaa anakuja Bongo kuupanda mlima Kilimanjaro.🔥🔥🔥

😜😜Kashaupanda wa Mobetto 😅😅 anataka kupanda Kilimanjaro sasa😁

Follow page yetu

Thanks for being a top engager and making it on to my weekly engagement list! 🎉 Ķ Mbombe, Rashidi Mbena, Furaha Mbega, A...
25/06/2024

Thanks for being a top engager and making it on to my weekly engagement list! 🎉 Ķ Mbombe, Rashidi Mbena, Furaha Mbega, Akulugula Berehani, Bob Rich, Flaviana Chileu, Dito Uliza, Ally Manyanya Manayanya, Maalim Abdul Kareem Hemed, Mwesiga Kikaka

Michael Jackson kabla yakuwa mzungu.Follow page yetu
24/06/2024

Michael Jackson kabla yakuwa mzungu.

Follow page yetu

Follow page yetu      Simba SC Tanzania Young Africans Sports Club
24/06/2024

Follow page yetu

Simba SC Tanzania Young Africans Sports Club

Mount Kilimanjaro 🇹🇿Follow page yetu
24/06/2024

Mount Kilimanjaro 🇹🇿

Follow page yetu

Korea kusini yafyatua risasi za onyo kwa wanajeshi wa Korea kasakzini.Hili limetokea mapema siku ya alhamisi ambapo kuto...
21/06/2024

Korea kusini yafyatua risasi za onyo kwa wanajeshi wa Korea kasakzini.

Hili limetokea mapema siku ya alhamisi ambapo kutokana na taarifa kutoka katika jeshi la Korea kusini ni kwamba wanajeshi wa Korea kaskazini walivuka eneo lisilo la kijeshi linalofahamika k**a Demilitarized zone ama (DMZ).

Eneo hili ni eneo ambalo lina urefu wa kilomita 250 na upana wa kilomita 4 ambapo haparuhusiwi shughuli yoyote ya kijeshi na hutumika k**a mpaka baina ya nchi hizo mbili tangu mwaka 1953 ambapo makubaliano ya kijeshi kati ya Marekani chini ya mwamvuli wa umoja wa mataifa na Korea Kaskazini.

Ikumbukwe kwamba Korea hizi mbili hazijawahi kusaini mkataba wa amani wala wa kusitisha vita bali ni makubaliano ya kijeshi yaliyofikiwa mwaka 1953.

Korea kusini imedai kuwa kuvuka kwa wanajeshi wa Kaskazini kwenye eneo hilo ni mara ya tatu ndani ya mwezi mmoja na mara zote imeonekana k**a walivuka kimakosa.

Tukio la hivi karibuni lilotokea alhamisi ,limetokea punde tuu baada ya ziara ya Rais wa Urusi Vladimir Putin nchini Korea Kaskazini alipokutana na Kim jong UN.

Hivi sasa nchi hizo zipo katika vita inayofahamika k**a "vita vya map**o" ambapo nchi hizo zimekua zikitumia map**o katika kutumiana vitu mbali mbali.

Korea kusini ilituma p**o likiwa na vipeperushi vya propaganda kuelekea Kaskazini na wao walijibu kwa kutuma map**o ya uchafu kuelekea kusini. Alhamisi pia ilishuhudiwa mwanaharakati wa Korea kusini akishirikian na mwananchi aliewahi kutoroka Kaskazini kutuma map**o 20 kwenda Kaskazini yaliyokuwa yamebeba vipeperushi laki tatu,flashi elfu tano zenye maudhui mbali mbali ya Korea kusini k**a nyimbo,filamu na michezo,lakini pia wakiweka na kiasi cha dola elfu tatu.

Jambo hili lilifanya dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Yo jong kutoa onyo la vitisho kwa Kusini akisema.
"Unapofanya jambo ambalo ulionywa waziwazi kutofanya, ni kawaida tu kwamba utajikuta ukishughulika na jambo ambalo hukulazimika kufanya," Shirika rasmi la Habari la Korea Kaskazini la Korea Kaskazini lilimnukuu Kim Yo Jong akisema.

Follow page yetu

✨ Platypus: mnyama wa ajabu zaidi! ✨ Huenda platypus ndiye mnyama wa ajabu zaidi kwenye sayari Dunia🌏. Ni mamalia 🐾, lak...
21/06/2024

✨ Platypus: mnyama wa ajabu zaidi!

✨ Huenda platypus ndiye mnyama wa ajabu zaidi kwenye sayari Dunia🌏.

Ni mamalia 🐾, lakini cha kushangaza hutaga mayai 🥚. Ana mdomo k**a wa bata 🦆, mkia wa beaver 🦫 , miguu ya bata na, ana sumu 🐍.

Mnyama huyu anayevutia ana vipokea umeme vya kutafuta mawindo 🦐, macho yenye koni mbili 👀, na cha kushangaza, hana tumbo. Kwa kuongeza, DNA yake ina chromosomes 10. Na ikiwa haya yote hayatoshi, platypus ni fluorescent! 🌟 yaani hung'aa chini ya mwanga wa UV, na kumfanya kuwa wa kushangaza zaidi.

Follow page yetu

Msimamo wa FIFA wa timu za taifa hivi sasaFollow page yetuKumi bora ya timu bora za taifa duniani hivi sasa.Argentina ba...
20/06/2024

Msimamo wa FIFA wa timu za taifa hivi sasa

Follow page yetu

Kumi bora ya timu bora za taifa duniani hivi sasa.

Argentina bado wanashika usukani.

Address

Mbeya

Telephone

+255654752753

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Onemoja maarifa posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Onemoja maarifa:

Share