08/08/2025
*VIJANA NA DEMOKRASIA: MSINGI WA MABADILIKO YA KWELI*✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻
Demokrasia ni ngoma ya mabadiliko inayohitaji kila kijana kucheza kwa hatua ya uelewa, si kwa midundo ya ushabiki. Ni mwaliko wa kuchagua kesho, si kusindikiza leo. Katika dunia inayosonga kwa kasi, vijana ndio pumzi ya taifa, lakini k**a hawatapaza sauti yao kupitia kura, taifa litabaki likilia kwa kimya kisichosikika.
Kura si kijikaratasi – ni silaha ya amani, ni saini ya maamuzi, ni mlango wa matumaini. Kwa vijana, kura ni zaidi ya haki – ni wajibu wa kizalendo. Kupiga kura ni kutangaza kwamba unaamini katika nguvu ya mabadiliko, na kwamba unaamini kesho inaweza kuwa bora zaidi k**a utaichangia leo.
> “Mabadiliko hayaji k**a mvua ya ghafla – huandaliwa, hupangwa, na huchaguliwa.”
Vijana wana elimu, wana nguvu, wana sauti, na wana ndoto. Sasa ni wakati wa kuzitumia hizo silaha nne kwa njia ya Demokrasia. Kupiga kura ni kutekeleza ndoto zako kwa vitendo. Ni kujenga taifa unalotamani kuliona — kwa kalamu yako, kwa fikra zako, kwa sauti yako.
Kwa hiyo, kila kijana anapaswa kujiuliza: Ninaitumiaje nafasi yangu ya kidemokrasia? Ninachagua kwa sababu ya ahadi tamu au kwa sababu ya historia ya utendaji? Maamuzi ya leo ni msingi wa maisha ya kesho. Na k**a kijana utatumia kura yako k**a zawadi ya hisia au kisasi, utalazimika kuishi na majuto yaliyojengwa kwa mikono yako mwenyewe.
> “Usisubiri kesho ijengewe na wengine, chukua tofali la kura yako, jenge na wewe.”
Kila kura ya kijana ni jiwe moja la kujenga daraja la kesho bora. Uamuzi wa leo unaweza kuwa uzuri wa kesho au majuto ya miaka mingi. Tusikubali kupoteza nafasi kwa maneno ya kupumbaza au ahadi za chupa tupu. Tusome, tuhamasike, na tupige kura kwa msimamo na maarifa.
> “Ukitaka mabadiliko, usisubiri viongozi waje – kuwa mmoja wao kwa kura yako.”
Kwa hiyo, vijana wote – wa vijijini na mijini, wa vyuoni na kazini, wa mitaani na majumbani – tuichukue Demokrasia k**a fursa ya kuandika historia, si kuisoma kwa huzuni. Tusikubali kuwa watazamaji