14/11/2025
SEMINA: *NAMNA YA KUPOKEA MSAADA WA KIUNGU (HOW TO ACCESS DIVINE HELP)*
KUTOKA: FAMILIA YA MAWAKILI WA INJILI (GOSPEL STEWARDS FAMILY -GSF)
MKUFUNZI: JAPHET KATANA
KARIBU DARASANI
Tuombe
Bwana Yesu mwema Asante kwa fursa hii ya uzima. Ninakutukuza kwa wema wako Asante kwa sababu unatufundisha ili tupate faida.
Ninaomba useme nasi katika majira haya tena.
Amen
Mpendwa wangu tulianza kujufunza kuhusu namna ya kupokea msaada wa kiungu katika siku kadhaa zilizotangulia, tumejifunza kuhusu Roho mtakatifu, ulinzi wa kiungu.
Nataka tusonge mbele tutazame jambo la tatu leo.
3. KIBALI CHA KIUNGU (DIVINE FAVOR)
Hii ni namna nyingine ambayo mwamini anapokea msaada wa Kiungu ni kupitia kibali cha kiungu.
Sasa unaweza kuwa unataka kujua kibali ni nini nataka tuanze na tafsiri nyepesi kabisa ya kawaida. Tunaposema kibali inamaana kitu kinachokufanya uruhusiwe kufanya jambo fulani katika eneo fulani. K**a unataka kusafiri nje ya nchi kwanza unapaswa kuwa na kitambulisho (passport) pia Visa kwa baadhi ya nchi huwezi kuingia bila visa. Hiki ni kibali cha kukufanya ukaruhusiwa kuingia katika nchi yao na kufanya shughuli zako kwa muda fulani.
Tukizungumzia katika usafiri kibali chako ni tiketi yako.
Mpendwa wangu sasa ninaposema kibali cha kiungu maana yake unapokea kukubalika kusikotokana na sababu au vigezo vya kawaida.
Usidhanie kila mtu anapata kazi sababu tu ya vyeti vyake bali sababu ya kibali pia.
Kuna watu akizungumza na mtu au akionwa tuu watu wanaanza kumtaka awe kiongozi wao hiki ni kibali, mara nyingi kinatokana na ukiroho.
K**a mtu hajui kanuni za ukiroho basi kibali chake kinaweza kupotezwa au kuibiwa, au kikaharibiwa na tabia zako mbaya.
Kumbuka kazi ya kibali ni kukufungulia milango ya fursa lakini tabia zako ndizo zitazifanya fursa hizo kukaa au kupotea.
Tusome andiko hili pamoja..
Zaburi 5:12
Kwa maana Wewe utambariki mwenye haki; Bwana, utamzungushia radhi k**a ngao.
(For thou, LORD, wilt bless the righteous; with favour wilt thou compass him as with a shield.)
Kiswahili neno lililotafsiriwa k**a radhi kingereza kinalitafsiri k**a kibali.
Unaona ukizungushiwa kibali k**a ngao ni wazi Kila mlango utakaokuwa unausogelea basi utakuwa unakufungukia.
Kibali cha Bwana ndicho humfanya mtu kukubalika kila anapokwenda ukifuatilia maisha ya Yusufu ndipo utaona hili kuhusu kibali likiwa halisi sana kila alipokuwa anakwenda anapata nafasi ya kuaminiwa na kuwa bora.
Mwanzo 39:3-6
3. Bwana wake akaona ya kwamba Bwana yu pamoja naye, na ya kuwa Bwana anafanikisha mambo yote mkononi mwake.
4. Yusufu akaona neema machoni pake, akamtumikia. Naye akamweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na yote yaliyomo akayaweka mkononi mwake.
5. Ikawa tokea wakati alipomweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na vyote vilivyomo, Bwana akabariki nyumba ya yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu. Mbaraka wa Bwana ukawa juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba, na katika shamba.
6. Akayaacha yote aliyokuwa nayo mkononi mwa Yusufu; wala hakujua habari za kitu cho chote chake, ila hicho chakula alichokula tu.
Hiki ndicho kibali cha Mungu watu wanajiona salama wakifanya kazi nawewe.
Unaaaminika, watu wanaona mafanikio katika mambo unayoyasimamia.
Hakika Mungu akikuachilia kibali mambo ambayo wengine wanatumia nguvu nyingi na hata wasipate wewe yanakufuata yenyewe.
Kibali cha Bwana kinaweza kukufanya watu kukupa zawadi, tuzo, pongezi, fedha n.k
Natamani kila siku liwe kati ya maombi yako, kuombea kibali kwanza katika uso na mwili wako ili watu wakuonapo wapate kukukubali pasipo sababu, pili kibali katika jina lako. Ili linapotajwa liwe jina jema kwa kila anayelisikia.
Ukikosa kibali maisha yanakuwa magumu, inamaana unakuwa na roho ya Kaini u akataliwa kila unapojaribu kusogea unakataliwa.
Mpendwa wangu Yesu mwenyewe alikuwa na kibali ndio maana alimpendeza Mungu pamoja na wanadamu.
Luka 2:52
Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.
(And Jesus increased in wisdom and stature, and in favour with God and man.)
Namimi ni ombi langu kwa Mungu miaka yangu inapoongezeka yaani umri unapoongezeka hakika na kibali cha Bwana juu yangu kiongezeke.
Sijui wewe shauku yako ni ipi..
Mwanzo 39:21
Lakini Bwana akawa pamoja na Yusufu, akamfadhili, akampa kibali machoni pa mkuu wa gereza.
(But the LORD was with Joseph, and shewed him mercy, and gave him favour in the sight of the keeper of the prison.)
Unaona jambo moja kujua umepokea fadhili za Kiungu ni kupata kibali.
Kabla sijafikia mwisho yako mengi ningesema nawe kuhusu kibali.
Lakini kibali chanzo chake ni Mungu mwenyewe hivyo usiache kuomba kibali ili Mungu akufadhili nacho.
Japo la pili kibali huja kwa kutenda vyema au kutenda vema.
Mwanzo 4:7
K**a ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.
Mpendwa wangu yako mengi ningeweza kusema nawe lakini naomba kwa leo nikomee hapa.
Shauku yangu ujue kwamba unaweza kupokea msaada wa kiungu kupitia kibali.
Nakutakia tafakari njema, ni Mimi ndugu yako nikupendaye sana. Japhet Katana.
Unaweza kufuatilia semina hii moja Kwa moja kupitia WhatsApp group yetu Mawakili wa Injili, tuma jina lako na mahali ubapatikana kuja WhatsApp namba +255745746691
Barikiwa sana
🇹🇿🇰🇪🇲🇼🇲🇿🇺🇸🇺🇬🇨🇩🇳🇦🇷🇼❤️