13/06/2025
UCHAMBUZI WA EP YA MBOSSO "ROOM NUMBER 3"
Kwanza kabisa nimpongeze Mbosso na watu wote ambao walikua nyuma kukamilisha project hii hakika mmejua kututendea Haki mashabiki na Wadau wa burudani.
1. JINA LA EP NA COVER
K**a ambavyo yeye mwenyewe amesema kua Room Number 3 sio chumba cha guest Bali ni sehemu ya Tatu ya ukuaji wake. Sehemu ya Kwanza ilikua Yamoto Band, sehemu ya pili ni WCB wasafi na sasa ni Yeye mwenyewe. Kwahiyo kila kitu humu unategemea ukute jinsi gani amekua.
COVER.
Ningekua mwanafasihi ningesema picha inasadifu yaliyomo Ndani, Kwanza ukiangalia Picha utaona watoto wa 3 wa Mbosso, Hii ni kwamba amekua Mwanaume sasa hakwepi majuk*mu yake anayatikiza k**a Baba.
Lakini pia ukiangalia Meza imesheheni vyakula na Matunda huku Mbosso ameshika chupa ya Chai ikiwa na maana Kwamba, Hayo ni Matunda ya mziki wake mpaka kufikia hapa, lakini bado yeye anajuk*mu la kuilisha familia yake k**a Baba.
2. IDADI YA NYIMBO BILA KUSHIRIKISHA MTU.
YES! Yuko sahihi kabisa 100% nyimbo 7 (6+1 bonus Track) k**a kweli amekua basi tunahitaji atuoneshe ukubwa wake, matarajio ya wengi ilikua NI kwamba kwakua mbosso hayuko WCB ana wigo Mpana wa kufanya Collaboration na wasanii wengine ikiwemo kundi lake la Yamoto Band, lakini lazima watu wajue kua huyu ni Mbosso Mkubwa inabidi aoneshe ukubwa wake.
3. NYIMBO BORA.
Katika nyimbo 7 ukimsikiliza mbosso ametumia Melody k**a 2 kwenye ladha mbalimbali za muziki ikiwemo Afro pop, Singeli, Mchiriku nk, ukiangalia Kwa namba mpaka sasa PAWA ndio imepokelewa Kwa ukubwa, lakini Kwa upande wangu Asuman huenda ukawa wimbo Bora wa Singeli, lakini Wimbo wa Nusu saa ni wimbo Bora Sana.
Mwisho.
Hii ni Ep Bora ipeni sikio lakini utunzi na uwasilishaji Bora wa mashairi ulio fanywa humu ni Excellent 👌 👌 nad Dope
By