MUST FM Radio - Mbeya

MUST FM Radio - Mbeya Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from MUST FM Radio - Mbeya, Media/News Company, Box 131, Mbeya.

04/09/2025
Unadhani ni lazima mtoto kuwasaidia wazazi wake kila kitu mara baada ya kusomesha?Live kupitia Live Ladha ya leo ya 104....
21/02/2024

Unadhani ni lazima mtoto kuwasaidia wazazi wake kila kitu mara baada ya kusomesha?

Live kupitia Live Ladha ya leo ya 104.5 Must Fm.

01/06/2023

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amewataka Wakuu wa Shule pamoja na Wakurugenzi kuzingatia utaratibu uliotolewa na Kamishna wa Elimu kuhusu muongozo wa kufunga na kufungua shule ili kuwapatia nafasi wanafunzi kupumzika katika kipindi cha likizo.

"na mbaya zaidi kuna baadhi ya malalamiko tumeanza kupokea kwamba kuna shule zinazuia wanafunzi kwenda likizo bila hata kushauriana na wazazi na wengine wazazi wanatakiwa walipe kuwaweka wanafunzi mashuleni" alisema Prof. Mkenda.

Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kinapenda kukukumbusha uwepo wa Dawati la Malalamiko linalolenga kubor...
23/03/2023

Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kinapenda kukukumbusha uwepo wa Dawati la Malalamiko linalolenga kuboresha ubora wa huduma zake kwa kamili.
Hivyo katika kuhakikisha inafikia malengo ya kushughulikia malalamiko Afisa anayehusika na Dawati hili pia anakualika kufika ofisi nambari 18 Administrative Basement ili kutoa maoni yako.
"Kwa pamoja tunaweza kuimairisha ubora wa huduma zinazotolewa na Taasisi yetu"
104.5 MUST FM

08/03/2023

"Wanawake ni CHACHU ya mabadiliko"
Ujumbe kutoka kwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), Utawala, Fedha na Mipango Dr. John P. John katika Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani Mwaka 2023.

Dr. John pamoja na kuwapongeza Wafanyakazi Wanawake wa MUST, amewahimiza kuendelea kufanya kazi kwa juhudi na maarifa katika kulitumikia TAIFA lao.

01/08/2022

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dkt. Rashid Chuachua amesema msimu wa mavuno wa mwaka 2021 Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ilizalisha jumla ya tani takribani milioni 10 za mazao ya chakula na tani 636,000 ya mazao ya biashara.

Dkt. Chuachua ametoa kauli hiyo leo wakati akitoa salamu akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera kwenye ufunguzi wa Maonyesho ya Wakulima (Nanenane) Kitaifa, ambapo pia ameeleza kuwa katika kuhakikisha kuna usalama wa chakula, mikoa hiyo mwaka 2022, inatarajia kuzalisha mazao ya chakula kwa ziada ya tani 5,900,000.

01/08/2022

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Phillip Mpango amevitaka Vyombo vya Habari kuelimisha na kuhamasisha jamii masuala yanayohusu kilimo na ufugaji kwa ajili ya kuchochea maendeleo na uchumi nchini.

Dkt. Mpango ametoa wito huo leo wakati akitembelea mabanda katika ufunguzi wa Maonyesho ya Wakulima (Nanenane) Kitaifa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini viwanja vya John Mwakangale, ambapo amesema lazima kuwepo na vipindi vya elimu kwa ajili ya wakulima pamoja na ufugaji wa aina zote ili kuwawezesha wananchi kufahamu kuhusu faida za sekta hizo.

28/05/2022

Leo ni Siku ya Hedhi Salama Duniani.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi amesema ‘’hedhi salama ni afya na ni baraka za uumbaji wa Mwenyezi Mungu’’ hivyo ameitaka jamii kuachana na mila na desturi potofu kuhusu hedhi.

Unashiriki vipi kuhakikisha jamii yako inakuwa na mazingira ya Hedhi Salama? Pia unaweza kutuandikia maswali yako kuhusu mada hii, ndani ya kipindi chetu AFYA NA MAZINGIRA kuanzia saa 5 asubuhi mpaka saa 6 Adhuhuri hapa 104.5 MUST FM Dira ya Sayansi na Teknolojia.

06/05/2022

Address

Box 131
Mbeya

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when MUST FM Radio - Mbeya posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to MUST FM Radio - Mbeya:

Share