06/12/2025
Mji wa Pemba nchini Msumbiji umegeuka kitovu cha mkutano wa kiroho baada ya Mtume Mwamposa kuanza kongamano lake kubwa la injili lililovuta maelfu ya waumini.
Katika mkutano huo uliojaa shangwe, nyimbo za kusifu na mahubiri yenye nguvu, watu mbalimbali walitoa ushuhuda wa kupokea faraja, uponyaji na nguvu mpya za kiroho. Wengine waliangua kilio cha furaha, wengine wakishangilia baada ya kudai kuponywa magonjwa yaliyowasumbua kwa muda mrefu.
Mkutano huu unaokamilika leo umeiweka Pemba kwenye ramani ya matukio makubwa ya kiroho Afrika Mashariki na Kusini, huku watu wakiendelea kumiminika kutoka maeneo ya jirani.
Kwa waliohudhuria, tukio hili wanasema limekuwa “tetemeko la kiroho”—na wengi wakisema, “kesi zao zimekwisha.”