29/12/2025
MWANDAMBO ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KIJINAI
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Mwalimu wa Shule ya Awali ya Saint Clemence, Clemence Kenani Mwandambo, mkazi wa Uzunguni “A” Jijini Mbeya kwa tuhuma za kuchapisha na kusambaza taarifa za uongo pamoja na kukashfu imani za dini zingine.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Benjamin Kuzaga imeeleza kuwa Mwandambo alik**atwa Disemba 29, 2025 majira ya saa nne asubuhi maeneo ya Uzunguni akichapisha na kusambaza taarifa za uongo pamoja na kukashfu imani ya dini ya kiislamu na kikristu kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii.
Kamanda Kuzaga amesema upelelezi unakamilishwa ili hatua nyingine za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake.