Hadithi kali za king mandela

Hadithi kali za king mandela fuata na kulike page hii ili kupata hadithi kali zenye kusisimua na kuelimisha, k**a unapenda hadith

26/12/2025

Usithubutu...

HATUPO SAWA (USAWA NI NADHARIA)Mwandishi KING MANDELADunia haina usawa, hivyo binadamu hatupo sawa pia, kuna wakati naja...
13/12/2025

HATUPO SAWA (USAWA NI NADHARIA)
Mwandishi KING MANDELA

Dunia haina usawa, hivyo binadamu hatupo sawa pia, kuna wakati najaribu kuelewa nadharia mbalimbali zinazo hubiri usawa baina ya watu duniani ila kila nikiwaza kwa kina nagundua ukitoa kitu kimoja kwamba wote ni binadamu, vingine vilivyo baki vyote hakuna kinacho hubiri usawa kwa vitendo,
huwezi kunielewa ikiwa hutotuliza akili yako na kuiandaa kunielewa, labda nikuulize jambo dogo, je na wewe na kati ya wale wanao amini kwamba binadamu wate tupo sawa, k**a ndiyo je ni kwanini, nadhani ukifikiria kwa kina utakuwa na majibu yako peke ako, baada ya kufiriki kwa kina nimegundua usawa wa binadamu upo kwenye nadharia na mikutano ya umoja wa kimataifa tu lakin ukweli ni kuwa hutuwezi kuwa sawa,

"Unasemaje tupo sawa ikiwa kwenye jamii mojapppp kuna masikini na kuna matajiri, wapo walio leta nadharia za utafutaji eti atafutae hachoki, ni kweli nakubali atafutae hachoki lakin je hii ina maana gani, je ni kweli kwamba kila asiye choka kutafuta hupata, bila shaka jibu ni hapana maana wapo walio tafuta sana tena bila kuchoka, wengine nawaona tokea nikiwa mdogo sana na juhudi zao za utafutaji hazikuwahi kukoma lakin ukweli ni kuwa wengi wao hawaja pata mpaka mda huu ambao mimi nimekuwa mkubwa na natafuta pamoja nao"

"Wahamasishaji husema vile uaminivyo ndani yako ndivyo utakuwa, sipingani nao wala kuwabishia ila naamini wanao amini kuwa wao ni watu wakubwa na wamebeba vitu vikubwa ndani yao ni wengi lakin wanao fanikiwa kufikia hata nusu ya vile wajionavyo ni wachache sana "

"Kuna baadhi ya wana imani huamini ya kuwa dunia imebebwa na bahati wao husema hata ukiwa mpambani vip k**a bahati yako si nzuri basi huwezi fanikiwa, hapo najiuliza usawa uko wapi" wengine husema ni lazima usafishe nyota, wengine husema kwa kuroga,wengine husema kwa kusali sana, lakin najiuliza ikiwa wengine kufanikiwa kwa kuroga na wengine kwa kusali je usawa upo wapi ?

"Ndugu zangu wana zuoni nazani ifike mahala sasa tukalishane chini tufundishane kwa vitendo ni kwa namna gani tunaweza kujikwamuwa kutoka kwenye hili tindiga la umaskini, kupeana moyo na ujasiri peke yake haitoshi, lakini hii ni kwa hadhira pia je mpo tayari kupokea maarifa mapya ili tuweze kujitwalia hekima kubwa na maarifa mengi ya jinsi ya kujikwamua kutoka kwenye mtego huu wa kimaskini ulio fanikiwa kuk**ata wengi kuanzia enzi za waanzirishi wa koo zetu, najaribu kufikiria tu, hatuwezi kuwa sawa ikiwa hatukaribiani kwenye namna ya kujitegemea, tunaweza vip kuwa sawa ikiwa wewe ni tegemezi yeye ni tegemezwi"

"Tufundishane na kuelekezana tu iwe kwa upole au kwa ukali kuwa hatuko sawa na hatuwezi kuwa sawa hata dunia ikianza upya kesho cha msingi ni walau kila mmoja wetu aweze kutambua kusudi lake la kuumbwa ni nini na je mungu alilenga nini katika uumbaji wa kiumbe wewe na kiumbe mimi nadhani kila mmoja akijua alicho kibeba na akakifata kwa namna ya kukifanyia kazi kuna wengi wataishi maisha huru ya kujitegemea na baada ya hapo hoja ya usawa inaweza kufikia asilimia 10, na hata k**a ni utegemezi yapaswa kuwa kutegemeana I mean ile ya win win situation sio utegemezi wa parasites vs host, bado nipo ndotoni naota namna nzuri ya kuhubiri usawa nikipata njia nzuri ntaamka
"Lakini ajabu ni kwamba usingizi ni mzito na usiku ni mrefu kwa ufupi ni kuwa hakukuchi, tenda ni usiku ilio beba usingizi wenye ndoto nyingi za kutisha, kuliko ndoto za furaha na kitia moyo, je huogopi unatishwa usingizini ukiamka unakutana na uhalisia je usawa uko wapi,
"Ibakia kuwa wote ni waafrika labda, wote wakiwa waarabu, labda waote washirikiane mwenye uzungu, lakini kwenye kuhubiri usawa tunadanganyana kwa kuwa neema zate hazifanani ,biblia husema kulikuwepo na wale maskini, na matajiri, mabwana na watumwa zao, watoza ushuru na maskini watozwa ushuru je bado unaamini tupo sawa ?
"Bila shaka umesinzia ukiamka utanikuta mbele nimetangulia kutafuta kinacho nifaa na kunistahiri maana usawa ni nadharia inayo lenga kuniacha shimoni, tena gizani ikiwa mwanga umefunikwa na giza, .....
Nb ni mimi African thinker

@
06/12/2025

@

TANGAZO..................NAMTAFUTA....Na mwandishi wako..... KING MANDELA/Daudi Nelsonmfalme wa nyanda za juu kusini/ MB...
18/09/2024

TANGAZO..................NAMTAFUTA....
Na mwandishi wako..... KING MANDELA/Daudi Nelsonmfalme wa nyanda za juu kusini/ MBEYA THE GREEN CITY.

"Simjui yeye ni nani wala sielewi anatokea wapi, siwajui ndugu zake wala marafiki walio mzunguka, sijui utaifa wake hata sielewi anatokea mkoa gani, sijafikiria ukabila wake kwa maana mimi si mbaguzi wa makabila, sijawahi kumuona akipita hata akiwa amesimama kwa mbali nawaza kuhusu hili nikiwaambia mtaniona chizi,"
"Uzuri wake ni zaidi ya pambo la ulimwengu kwa jinsi anavyo vutia, mwili wake ni k**a shamba lenye rutuba kila mkulima atakae muona lazima atamani kuwa awe wa kwanza kuweka mbegu ya zao alipendalo, sijui k**a unaelewa kwa maana naongea haya nikiwa nimevurugwa , ubongo ukiwa umekosa njia kwa maana sijui wapi nitamuona"
"Rangi yake ya dhahabu kila mara inanirudia, macho yake ya mviringo mazuri yenye mng'ao na rangi ya kipekee ambayo sikuwahi kuiona duniani, akikutizama ana uwezo wa kuvuta kila kitu na kufuta kumbukumbu ya uliyo kuwa ukiyafanya ili umtizame yeye, wengine husema yule ni jini jann aina ya majini ambao dhahania husema ni majini wenye mionekano mizuri zaidi kwenye jamii ya majini yaan, umbo matata, sura ya kupendeza na macho ya kung'aa na roho ya kusaidia wengine,'

"Ananifahamu kwa majina kwa maana ndotoni huniita tena na sauti yake nzuri ni k**a sauti ya kinanda kilicho kuwa kikipigwa na mpiga kinanda maarufu kutoka nchini Argentina yaan mwanamama Martha Argerich" k**a ukipata nafasi ya kusikia sauti yake walai nakuambia utalizimaka kumfata k**a kivuli chake popote pale aendapo,

""Natamani nimpate lakin sijui ni wapi nitampata, natamani ningeweza kuigeuza taswira yake inayo ishi kichwani mwangu kuwa picha na niweke kila sehemu k**a mabango ili walimwengu wanisaidie kumwangaza huko alikuwa "
"Hunijia ndotoni lakini hajawahi kunitajia jina lake, natamani ningemjua jina pengine ningelipia hata media huko watangaze kua anatafutwa, pengine angejitokeza nami ningemuona "

"Ni kweli namtafuta ila sijui ni wapi nitamuona, sijui yupo wapi, sijui anaishije, lakini cha zaidi hata yeye simjui pia, sijui nifanyaje, nasema sijui nitende lipi, k**a kuna mtu anamjua tafadhari naombeni msaada wenu nifanyajeee"

Simulizi.......................Mapacha na ndoaMwandishi..........King Mandela/Daudi NelsonSehemu ya........................
01/04/2024

Simulizi.......................Mapacha na ndoa
Mwandishi..........King Mandela/Daudi Nelson
Sehemu ya..............................0️⃣1️⃣

Katika daradara moja watu walikuwa wakimiminika, waking'ang'niana kuingia watu wengi waliipenda gari hii ya abiria kutokana na usafi na ustaharabu pamoja na upendo walio kuwa nao kondakta na dereva wake, ndani ya mda mchache gari ilikuwa imejaa abiria tayari na hapo ikaanza safari yake ya kupeleka abiria wake mjini katika siti ya mbele ya dereva alionekana binti mmoja mzuri, nathubutu kusema mzuri kwani binti huyu mwenye urefu wa wastani, sura yake iliyo jiviringa vizuri utasema mungu alimuumba wikiendi akiwa hana majukumu mengi, hivyo alikuwa na kazi moja tu ya kumuumba yeye kwani mbali na kichwa kilicho pambwa na sura nzuri, shingo iliyo beba kichwa kweli iliongeza uzuri wa binti huyu shingo yake ilikuwa ndefu yenye kutengeneza maringo mithili ya twiga, kifuani binti huyu alikuwa amepambwa na machungwa flani ambayo si makubwa wala madogo yakiwa yamepambwa na chuchu zilizo simama wima kweli, nikielezea uzuri wake naweza kutengeneza hadithi nyingine lakini alikuwa na tumbo flati chini ya katikati ya mwili yaani chini ya kitovu kulikuwa na kiuno cha mviringo mithili ya round about ya letko kuelea hospital rufaa ya mbeya chini ya kiuno kulikuwa na mzigo flani ya haja nahisi kwa uzoefu wangu wa kupima nyama ule mzigo ungefika kilo ishirini ivi, ukishuka kwenye hips mapaja pamoja na miguu dah hapo k**a mwanaume rijari lazima utamtizama tu, mwanzoni dereva alijifanya kuwa bize kuendesha gari yake lakini kila alipo taka kuingiza gia alijikuta akikutanisha macho yake na mapaja ya binti yule, dereva ambaye kwa jina aliitwa Joel alijikuta akijisemea moyono, dah hii kazi bwana nimewahi kutana na wadada wengi wazuri ila huyu duh mwisho tunafanya dhambi bure, wakati akiwa kwenye mawazo yale alisikia sauti ya konda wake ambaye kwa jina anaitwa John na hawa walikuwa ndugu yani walikuwa mapacha tena wa kufanana
"sai shusha apo ilikuwa ni sauti ya John mbayo ilimfikia moja kwa moja dereva wake, na yule dada pamoja na abiria wote mule ndani,
,mmmmh huyu kaka anasauti nzuri alijisemea moyoni yule dada aliye kaa siti ya mbele kwa dereva ambaye kwa jina anaitwa Tina huku akigeuka kumuangalia konda yule, baada ya kuyatuma macho yake kwa yule konda kwa muda alijikuta, akijiuliza mmh huyu mbona amefanana dereva wake hivi, alijiuliza Tina na kugeza shingo yake na kumtizama dereva ambaye ni Joeli, alikutana na sura k**a aliyo iona kwa konda, hapo tina akijikuta ghafla ubaridi ukimwingia kwenye moyo hali ambayo haikuwahi kumtokea kabla, ivi Tina nimekuwaje mimi maskini, inamaana ndo nishapenda au, alijiuliza Tina, huku akimtizama dereva na kwa kuibia akigeuka na kumwangalia kondakta, hali ambayo Joel ambaye ni dereva aliitambua vyema na hapo hata yeye akaona ndo mwanya wa kumuongelesha binti huyu,
"dada vipi naona unatufananishaa, vip ushawah kutuona aliuliza joel swali ambalo lilimuacha tena hoi kwani sauti ya joel na John zilifanana sana hivyo ilikuwa kazi sana kuwatofautisha mapacha hawa
"mmmmh mmh ham hamna kaka yangu ili ninyi mnafanana sana, aliongea Tina
"ndiyo dada sisi ni ndugu yeye ni k***a hivyo kwangu ni kaka na mimi ni doto, aliongea Joel,
"ahaa sawa kaka ila mnaonekana mnapendana kweli, aliongea Tina
"kawaida tu dada yangu na hata hivyo mimi na ndugu yangu hatujawahi kuishi mbalimbali aliongea Joel
"mmh hongereni kwa upendo wenu kaka maana kuna ndugu wanagombana kwani na mimi nina pacha wangu na huyo sijawahi kuishi naye namuona tu kwenye picha, aliongea Tina
"daah pole dada yangu kwani yeye yuko wapi? Aliuliza Joel
"ni stori ndefu kaka yangu, naitwa Tina hii na kadi yangu ya kibiashara ina namba zangu za simu aliongea huku anamkabizi kadi ile, sijui wewe unaitwa nani kaka yangu
"mimi naitwa Joel na ndugu yangu anaitwa John aliongea Joel huku akipokea kadi ile na kuiweka mfukoni na kwa wakati ule tayali gari ilikuwa inafika kabwe
"sawa mimi nashuka ila naomba ukipata mda usisite kunitafuta. Aliongea Tina na kwa wakati ule tayari gari ilikuwa imesimama hivyo akafanya kushuka, bas joel na John waliendelea na majukumu ya siku ile mpaka malengo ya bosi yalipo kamilika ambapo walienda kurudisha gari kwa bosi kisha safari ya kurudi gheto ambako walikuwa wakikaa ikanzaa, na uzuri ni kuwa wao walikuwa wanakaa mtaa wa itezi wakati bosi wao alikuwa anakaa mtaa wa bomba mbili mitaa ambayo ilikuwa imepakana hivyo haikuwa kazi sana kurudi mpaka nyumbani, basi wakati wanarudi Joel akawa ameanzisha hadithi kidogo kuhusu suala lile la mchana
"John unajua leo kuna mtoto mkali kinyama nimemuona yaani toka nianze kazi ya udereva leo nimekutana na mtoto mkali kinyama yaani toka niwe dereva ni leo nimeona mtoto mzuri aliongea Joel
"haaahahaa Joel bwana ina maana kuwa siku zote hukuwahi kuona mtoto mzuri yaan unamaana huyo ni mzuri kuliko shemeji yangu uliye achana naye
"John sikutanii mwanangu yan mpaka Prisca akasome bonge la mtoto, utamwona na si kanipa namba ya simu mwenyewe tu utanyosha mikono na miguu juu kaka, aliongea Joel
"Tatizo lako Joel unapenda kusifia sasa utakuta kipuri chenyewe cha ajabuuu, aliongea John
"aaaah John bwana eti kipuri cha ajabu kile sio kipuri kaka ni bonge la kinjuka kaka mtoto sura k**a hajazaliwa ilo umbo sasa huko nyuma ndo daa utajua kuna kitu kimepachikwa acha tusiandikie mate nikipimpigia nitamwomba anitumie picha whatsapp, aliongea Joel na kwa wakati ule tayari walikuwa tayari wamefika gheto,
"haya bhana nitamuona vipi sasa leo tunakula nini mzee, aliongea John akimuuliza Pacha wake
"mmmmh leo nahis tuleee tukale gengeni tu bro miye nimechoka naitaji kulala mapema, aliongea Joel.
"Tatizo lako wewe mtoto wa mama sijui huko chuo ulikuwa unaishijee mzee, aliongea John akimzihaki pacha wake yake
"acha tu kaka yaan nimesoma kwa shida afu ndo ivo ajira noo ila sawa siku moja mambo yanaweza kuwa poa labda tutaajiriwa broo ila kaka inatubidi tuwekeze sana aliongea Joel na kuendelea
"tatizo broo ulikimbilia chuo saizi tungekuwa na biashara zetu kwani toka nimeanza kufanya kazi na wewe saizi hela inaonekana, kaka unajua miaka yote mitatu nimefanya kazi na walevi hela nilikuwa siioni na kuna mda hata gari haikuwa na wateja sababu ya ukali wa makonda wangu lakini saizi tumekutana wote sio walevi tunaweza fanya jambo la maana, Aliongea Joel,
"daah kaka eti walevi dah sawa twende tukale alafu umpigie huyo mrembo, aliongea John kisha wakainuka kuanza kuutafuta mgahawa ambao ulikuwa karibu na eneo lile, alifika wakaagiza wali maharage wakala kisha wakarudi zao gheto,
"haya sasa mpigie huyo mrembo bro maana si kwa sifa ulizo mmwagia, aliongea john
"sawa kaka ila dah nimesahau kukunua vocha ila nina sms si mbaya nitamtumia meseji tu, aliongea Joel akiitoa kadi ile ya biashara aliyo pewa na Tina kisha akahamishia namba zile kwenye simu yake,
"Sms unazingua wewe sema sio mbaya nahis nina vichenji mpesa kwanza nikuhamishe uunge dakika aliongea John na hapo alilo sema alilitimiza mwisho wakaunga dakika"
""""""itaendelea,,,,,,,,,,,

Matarajio ya urejeo ...Je upo tayari kupokea kazi mpya
01/04/2024

Matarajio ya urejeo ...
Je upo tayari kupokea kazi mpya

Top 10 ideas from the book "Start with Why - How Great Leaders Inspire Everyone to Take Action" by Simon Sinek"Start wit...
26/08/2023

Top 10 ideas from the book "Start with Why - How Great Leaders Inspire Everyone to Take Action" by Simon Sinek

"Start with Why" by Simon Sinek is an engaging discussion about the power that 'why' holds in influencing our actions. Here are the top 10 ideas from the book:

1️⃣Understand Your 'Why': The principle of 'why' being more important than 'what' or 'how' is central to the book. Sinek argues that understanding why you do what you do is the key to inspiring others. This includes understanding your passion, purpose, or belief.

2️⃣Golden Circle Concept: The Golden Circle consists of Why (the purpose), How (the process), and What (the product). Sinek states that most companies work from 'what' to 'why,' but the inspiring leaders and companies work in the opposite direction, from 'why' to 'what.'

3️⃣Authenticity in Leadership: For a leader or a company to inspire, they must be authentic. The 'why,' 'how,' and 'what' must align; this is called a 'WHY Statement' in Sinek's terms.

4️⃣Inspiration Over Manipulation: While manipulative techniques can drive sales and spur action, they do not foster loyalty and trust the way inspiration does.

5️⃣Trust and Loyalty: If a company or leader's 'why' resonates with people, they can build deeper relationships based on trust and loyalty because people understand, believe in, and want to support what they're doing.

6️⃣People Over Profit: Companies that prioritize profit over people, risk losing the connection with their clients or employees, thus, decreasing loyalty and morale. Sinek stresses that people and 'why' should be a priority.

7️⃣Effective Communication: The key to successful communication starts with saying 'why' you are doing what you are doing, followed by 'how' you will do it, and then 'what' you are doing.

8️⃣Successful Hiring: Leaders should hire people who align with the company's 'why.' By doing so, they will have a team working for a common purpose, not just a paycheck.

9️⃣Leadership Responsibility: Leaders have a responsibility to protect their team. Sinek suggests having individuals who feel safe, and are willing to take risks, can foster creative solutions.

1️⃣0️⃣Clarity, Discipline, Consistency: These are the principles upon which trust is built. Sinek says that understanding the 'why,' being disciplined in the 'how,' and being consistent in the 'what' leads to a robust, trustworthy business or organization.

This revolutionary book shows leaders and organizations how to inspire others by focusing less on what they do and more on why they do it!

Have a great weekend💕

Address

Mbeya

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Hadithi kali za king mandela posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Hadithi kali za king mandela:

Share

Category