HERO MEDIA

HERO MEDIA Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from HERO MEDIA, Media, Mbeya.

Karibuni kufollow ukurasa huu.HERO MEDIA
14/09/2025

Karibuni kufollow ukurasa huu.

HERO MEDIA

“Chama cha ACT-Wazalendo kimeendelea kuwa darasa la kudai na kupigania demokrasia Tanzania. Tulisema tunashiriki (uchagu...
13/09/2025

“Chama cha ACT-Wazalendo kimeendelea kuwa darasa la kudai na kupigania demokrasia Tanzania. Tulisema tunashiriki (uchaguzi) tukipambana na tunapambana tukishiriki.”
Dorothy Semu, Kiongozi ACT-Wazalendo

HERO MEDIA

Mgombea urais kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu ameahidi kuendeleza baadhi ya misingi ya utawa...
13/09/2025

Mgombea urais kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu ameahidi kuendeleza baadhi ya misingi ya utawala wa Hayati Rais John Magufuli, ikiwa atachaguliwa kuingia Ikulu katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

Akihutubia mamia ya Wakazi wa Nkololo Bariadi Vijini, Mkoa wa Simiyu, Mwalim amesema Serikali ya Magufuli alijitahidi kutatua changamoto za Wananchi, hasa katika sekta ya Kilimo, Miundombinu na kupambana na rushwa.

“Nichagueni niende Ikulu nikavae viatu vya Magufuli nikainyooshe hii nchi, alikuwa Mwanaume mmoja tu, alifanikisha; wengine wote wameshindwa.” amenukuliwa Salum Mwalimu

HERO MEDIA

Rais wa Marekani, Donald Trump, ametaka nchi zote za NATO kuacha kununua mafuta kutoka Urusi na pia kuweka ushuru mkubwa...
13/09/2025

Rais wa Marekani, Donald Trump, ametaka nchi zote za NATO kuacha kununua mafuta kutoka Urusi na pia kuweka ushuru mkubwa kwa bidhaa kutoka China. Trump anasema kwamba hatua hizi zinaweza kusaidia kumaliza haraka vita vya Russia na Ukraine. Alieleza kuwa yupo tayari kuweka vikwazo vikubwa dhidi ya Urusi ikiwa nchi zote za NATO zitashirikiana naye, na kwamba ushuru mkubwa dhidi ya China unaweza kudhoofisha udhibiti wa China juu ya Urusi, jambo ambalo linaweza kuharakisha kumaliza vita.

Trump ameonya kwamba k**a nchi za NATO hazitashirikiana, jitihada za Marekani zitakuwa zinapoteza muda na rasilimali, huku akisisitiza kwamba utekelezaji wa pamoja unaweza kuokoa maisha mengi na kuokoa pesa nyingi za taifa. Katika maneno yake, Trump anasisitiza haraka hatua na mshik**ano wa kimataifa k**a njia ya kumaliza mzozo huu hatari.

HERO MEDIA

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi k...
13/09/2025

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kukamilisha miradi ya umeme mkoani Kigoma ikiwemo ule wa maji katika mto Malagarasi utakaokuwa suluhisho la changamoto za nishati kwa mkoa mzima.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika wilayani Kasulu leo Jumamosi Septemba 13, 2025, Dkt. Samia amekumbusha hatua kubwa iliyofikiwa mwaka 2022 wakati Kigoma iliunganishwa kwenye gridi ya Taifa kupitia mradi wa Nyakanazi.

“Ninakumbuka tulikuwa pamoja tarehe 17 mwezi wa 10 mwaka 2022 katika ziara ya kihistoria nilikuja kuwasha umeme wa gridi ya Taifa katika wilaya ya Kasulu na kuzima mitambo ya jenereta za dizeli. Hii ilikuwa ni hatua kubwa kwani mbali na kuiunganisha Kasulu tuliunganisha pia Buhigwe kupitia wilaya za Kakonko na Kibondo,” amesema Dkt. Samia.

Amefafanua kuwa mradi huo uliwezesha serikali kuokoa takribani shilingi bilioni 58 ambazo awali zilikuwa zikitumika kununua vipuri na mafuta kwa ajili ya mitambo ya dizeli, fedha ambazo zimeelekezwa kwenye kupeleka umeme vijijini mkoani humo.

Hata hivyo, Dkt. Samia amekiri bado kuna changamoto za upatikanaji wa nishati ya uhakika kutokana na umbali wa kuzalisha umeme na Kigoma, hivyo hatua madhubuti zimechukuliwa.

“Ndiyo maana tumeamua kuendeleza mradi wa umeme wa maji pale mto Malagarasi utakaotoa megawati 49.5. Tukizalisha umeme ule, itakuwa rahisi kuusambaza ndani ya Kigoma,” amesema.

HERO MEDIA

''Mdogo wangu  leonardo am so proud of you lakini nataka kukumbusha kitu kimoja kikubwa epuka kuharibu chain of connecti...
13/09/2025

''Mdogo wangu leonardo am so proud of you lakini nataka kukumbusha kitu kimoja kikubwa epuka kuharibu chain of connections katika maisha yako .

Hakikisha hauharibu au kudhihaki brand ya tajiri mwingine ili ku maintaina connection za leo na kesho . Ndio maana mimi ni simba lakini huwezi kunikuta nimedhihaki brand ya GSM hata siku moja sababu najua kazi zangu zinarotate huku na kule .

Umekosea saaana kuharibu brand na kudhihaki brand ya joerwegasira . Nikukumbushe Jayrutty_ ana brand nyingi saana ambazo zingine hazihusiani na mpira . Huenda ungeweza kufanya vizuri kwenye tamasha la mwananchi na akakuona kisha akakutumia kwenye bidhaa zake nyingine za Jayrutty.

Nakushauri usichekeshe kwa kudhihaki brand nyingine . Najua unajua sana kuchekesha mdogo wangu ila jana umeharibu saana kwa tajiri Joerwegasira

But fata nyayo zangu ndio maana u naona mm nafanya kazi yanga na simba kote kote naokota sababu siwadhihaki kwa kutumia Brand zao but nawakera kutumia mashabiki zao'' Ameandika Mwijaku.

Nini maoni yako?

HERO MEDIA

Baada ya msako wa siku mbili, Tyler Robinson (22), mkazi wa Utah, amek**atwa kwa tuhuma za kumuua mwanaharakati anayeung...
12/09/2025

Baada ya msako wa siku mbili, Tyler Robinson (22), mkazi wa Utah, amek**atwa kwa tuhuma za kumuua mwanaharakati anayeunga mkono Israel, Charlie Kirk.

Kwa mujibu wa ripoti ya New York Post, Robinson alikiri kwa baba yake kuwa ndiye aliyempiga risasi Kirk. Baada ya kukiri, baba yake alimkabidhi mwenyewe kwa polisi na kusalia naye hadi alipochukuliwa na mamlaka husika.

Rais wa Marekani, Donald Trump, amethibitisha kuk**atwa kwa mtuhumiwa huyo Ijumaa hii kupitia mahojiano ya televisheni, akisema vyombo vya usalama vimefanikisha operesheni hiyo baada ya msako wa karibu siku mbili.

HERO MEDIA

Rais wa zamani wa Brazil, Jair Bolsonaro, amehukumiwa kifungo cha miaka 27 jela na Mahak**a ya Juu baada ya kupatikana n...
12/09/2025

Rais wa zamani wa Brazil, Jair Bolsonaro, amehukumiwa kifungo cha miaka 27 jela na Mahak**a ya Juu baada ya kupatikana na hatia ya kupanga njama za kupindua matokeo ya uchaguzi wa 2022 na kujaribu kubaki madarakani kwa nguvu.

Bolsonaro alikutwa na hatia katika makosa matano, ikiwemo kupanga mapinduzi ya serikali, kushiriki katika genge lenye silaha na kuharibu mali za umma wakati wa uvamizi wa majengo ya serikali Januari 8, 2023.

Ingawa alikanusha mash*taka hayo, ushahidi ulionesha alihusika moja kwa moja katika mpango wa kudhoofisha demokrasia na kushinikiza jeshi kuingilia kati baada ya kushindwa kwenye uchaguzi.

HERO MEDIA

Mahak**a ya Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, imemhukumu kifungo cha miaka mitano jela au kulipa faini ya shilingi 300,00...
11/09/2025

Mahak**a ya Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, imemhukumu kifungo cha miaka mitano jela au kulipa faini ya shilingi 300,000/= Adela Ndela Zakaria (25), mkazi wa Viwawa, Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya, baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kutupa mtoto jalalani mwanzoni mwa mwezi Septemba 2025.

Hukumu hiyo imetolewa na Mheshimiwa Hakimu Ngeka, aliyesema kitendo hicho ni cha kinyama na hakikubaliki katika jamii yoyote.

Kwa mujibu wa maelezo ya kesi, mshtakiwa alifika Dar es Salaam mwezi Aprili 2025 kwa lengo la kufanya kazi za ndani. Alipokelewa na mwenyeji wake eneo la Keko, bila kufahamika kuwa alikuwa mjamzito. Baada ya kujifungua, alificha ujauzito huo na kisha kumtupa mtoto wake wa k**e jalalani, akidhani hatagundulika na hivyo kuendelea na kazi aliyoifuata.

Tukio hilo lilifichuliwa baada ya majirani kuona kichanga kikiwa kimetupwa, ndipo uchunguzi ulipofanyika na kubaini kuwa mtuhumiwa ndiye aliyefanya kitendo hicho. Alipok**atwa na kuhojiwa, alikiri kuhusika moja kwa moja.

HERO MEDIA

Mahak**a ya Wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, imetoa adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa Grayson Muze Msemo (55), mui...
11/09/2025

Mahak**a ya Wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, imetoa adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa Grayson Muze Msemo (55), muinjilisti na mkazi wa Raskazoni – Tanga, baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa k**e mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi minne.

Hukumu hiyo ilisomwa jana, Septemba 10, 2025, majira ya saa saba mchana na Hakimu Mkazi, Mheshimiwa Husna Mwiula, ambaye alibainisha kuwa ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka ulikuwa wa kutosha kumtia hatiani. Amesema kifungo hicho kinalenga kutoa fundisho kwa jamii na kulinda haki za watoto.

Kesi hiyo ilihusisha tukio la Septemba 1, 2025, katika eneo la Funguni Street, Pangani, ambapo mtuhumiwa alidaiwa kutekeleza unyama huo.

HERO MEDIA

Chief God Love amefichua kuwa aliwahi kumpa Chid Benz kiatu chenye thamani ya shilingi milioni mbili, k**a ishara ya upe...
11/09/2025

Chief God Love amefichua kuwa aliwahi kumpa Chid Benz kiatu chenye thamani ya shilingi milioni mbili, k**a ishara ya upendo na heshima kwake.

"Nilimwambia, usinunue nguo. Njoo kwangu, kuna nguo nimezinunua lakini sijawahi kuzivaa. Nilikuwa nimepanga kuzivaa kwa heshima, lakini leo nataka wewe uzivae, kwa sababu mimi mwenyewe naenda kwenye tukio la Tunda. Kwa heshima, sitaki nizivae mimi. Kuna kiatu nilichonunua kwa dola elfu moja, njoo ukichukue," alisema Chief God Love.

Tamasha la Simba Day limefanyika jana tarehe 10 Septemba 2025 ambapo pamoja na burudani toka kwa wasanii mbalimbali, pia...
11/09/2025

Tamasha la Simba Day limefanyika jana tarehe 10 Septemba 2025 ambapo pamoja na burudani toka kwa wasanii mbalimbali, pia kulikuwa na mchezo wa kirafiki kati ya Simba na Gor Mahia.

HERO MEDIA

Address

Mbeya

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when HERO MEDIA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category