27/07/2025
Ukiwa Kijana, kuwa Mfano wa Kuigwa!
K**a kijana wa taifa hili, unapaswa kuwa mfano bora kwa vijana wenzako—kuwapa sababu ya kuamini kuwa mafanikio yanawezekana, hatua kubwa zinaweza kupigwa, na ndoto zinaweza kutimia.
Klabu ya Yanga SC imempata kijana wa mfano—Hersi Said. Kiongozi kijana ambaye amekuwa chachu ya mabadiliko makubwa katika tasnia ya soka nchini Tanzania. Ameonyesha kuwa vijana wakipewa nafasi, wakaaminiwa, na kuungwa mkono, wanaweza kupeleka taifa hili mbali katika sekta mbalimbali.
Hersi, wewe ni shujaa. Wewe ni kielelezo cha uthubutu, maono, na mapenzi ya kweli kwa taasisi unayoiongoza. Endelea kuupiga mwingi—Tanzania inakuona, na Yanga SC inaendelea kufaidika na uongozi wako wa mfano.
Leo unatimiza miaka kadhaa tangu kuzaliwa kwako. Tunamuomba Mwenyezi Mungu azidi kukulinda, kukuongoza na kukutunza katika safari yako ya maisha. Wananchi wa Yanga SC na Watanzania kwa ujumla, tunajivunia kuwa na kiongozi kijana k**a wewe.
Leo dunia inaitazama Tanzania kwa namna tofauti. Dunia inaitazama Yanga SC k**a klabu kubwa, imara na yenye maono—na yote haya ni matokeo ya uongozi wako makini na thabiti.
Enjoy Your Birthday Rais Wa Kabumbu 🎂🎂
Endelea kuwa mwanga kwa kizazi cha sasa na kijacho.