23/10/2025
                                            JE, WAJUA KWANINI NENO MAANDAMANO KWA TANZANIA LINATUPA HOFU SISI AMBAO TUNAHITAJI AMANI ITAWALE?
    Leo nakudokeza kwa ufupi, kuwa MAANDAMANO sio tatizo na kwenye katiba kwa wataalamu wa Sheria wananielewa kuwa yanaruhusiwa.
   K**a mnavyojua kwenye maandamano kila mtu ana namna anavyowaza na kuyafanyia kazi, hivyo kuna chombo ambacho kinasimamia RAIA na Mali zao. Hiki chombo kinapaswa kupewa taarifa ili kiweze kutoa ruksa, endapo wale wenye nia Ovu watakapoinuka basi hiki chombo kiweze kulinda Raia wake na mali zao zisihalibiwe.
    Hicho chombo kina hatua moja mbele, kujua aina ya watu na aina ya maandamano yanayotakiwa kifanywa. K**a hicho chombo hakijaridhishwa na uratibu wa maandamano hayo, wahusika wa maandamano hawatapaswa kufanya maandamano.  Kwasababu chombo kinacholinda raia na mali zao, kimeona madhara yake. 
   KWA UCHACHE HUO, TUNAPASWA KULIOMBEA TAIFA KWA PAMOJA ILI KUINUA MIOYO YA WALIOVUNJIKA NA KUKATA TAMAA.
   Kwenye maisha kila mtu anaguswa kwa namna yake, naomba saana kuwa pale tunapoona hapapo sawa zipo njia nyingine za kuhakikisha panakuwa sawa.
    Mfn: 
Huu ni Mwaka wa Uchaguzi, kuna vyama havijashiriki kampezni za uchaguzi na wanachama wake inamaana hawatashiriki. Vile ambavyo vimeshiriki kampeni za Uchaguzi, wanachama wake wataenda kwenye vituo vya kupigia kura na kuwachagua viongozi wawakilishi kwenye vyama vyao.
    K**a Chama chako hakijashiriki Uchaguzi na unaona kuna kiongozi ambaye wewe unaona hafai, nenda kituo cha kupigia kura kamchague wa Chama kingine ambaye anafaa.
  Lakini usishiriki kuzuia wengine wasiende kupiga kura, hutokuwa unaikosea Serikali tu baali utakuwa unamkosea yeye kwa kumzuia kufanya jambo ambalo linampa amani. Hautakuwa unaitafuta haki yako kikatiba kwa kuinyima haki ya mwenzio, nenda kituo cha kupigia kura kwa hasira hiyo kamchague unaemtaka.
MWISHO:
    Mungu atupe wepesi wa kubebeana madhaifu, sisi mimi nimezaliwa na kukulia kwenye Familia Duni. Mpaka sasa napambana ili niwe msaada kwa Familia yangu, unadhani akaja mtu kuivuruga sehemu ninapopatia ugali. Nitaishije?
   KILA MMOJA AJIPE MUDA WA KUJITAFAKALI BINAFSI, KISHA TUSEME NJIA YA KUITAFUTA HAKI INAHITAJI UTULIVU WA AKILI NA MWILI.
   🇹🇿❤️