
03/10/2025
EPISODE 62: NUSU BINADAMU NUSU MBWA MWITU
.......ILIPOISHIA.........
Aliposema maneni hayi niliona nyewel na shuka la kimai likienda katika ule mparangani wa lile joka, huko nje kelele za wamama ng'ombe, na wazee pamoja na watoto ndio zilizonidonisha chozi hasa pale lisoyani kuniacha kanifunga............SASA ENDELEA.....
Nilitafuta jitihada za kujikwamua kile kitanzi cha mikono na miguu kwa jina lingine iliitwa (KUDU). Ni mda sio mrefu tu ndio vidonda vilitibiwa, lakini vilianza kuvuja damu tena nikiwa najizungusha na kutapa tapa pale chini ili nitoea kamba.
Nikiwa pale kwenye giza nilisikia sauti ya mtoto mchanga ikilia pembeni kidogo kwenye giza lillozidi kuliko pale nilipikuwa. Sauti yake ilifanana na k**a mtu aliyejifungua siku za karibuni au siku hiyo.
Kelele za kule nje na zile za yule mtoto mchanga zilifanya nianze kujinyanyua ata nikae kwa magoti
"Ntapata wapi panga au kisu nijifungue mimi" nilijisemea moyoni nikianganza huku na kule ili nione kitu cha kujifunga lakini sikubahatika kuona ata ncha ya upanga wala chupa, zaidi ya ngozi zilizotandikwa chini pamoja na vibuyu.
"Hapana sikubali watu wanakufa kisa ujio wetu lazima niwasaudie" niliwaza hayo nikiwa naisugua mikono ambayo mda ule ilikua ishatoa alama za michubuko kwa kuisugua kwa nguvu. Nilianza kukaza mikono k**a naitanua kwa nyuma nikajikuta napata maumivu nakubwa sana. Kichwa nimekilaza chini bado, nilpigwa na butwaa baada ya mwanga wa mwezi kumulika pale niliko k**a niko nje halafu mngurumo mkali ukiwa juu yangu, nilijiuliza swali ambalo sikuweza kujijibu mapema kwa kile nilichokiona.
Matone ya maji yalinidondokea. Wazo lilinijia kwamba ni mvua inanyesha lakini imepitaje wakati nilikua ndani pia kusingeweza kupita mvua.
Niligeuza shingo kuangalia juu kumekuaje mpaka nadondokewa na maji, macho yangu yalitwama kwenye mznuguko wa maji, huku miraba ya mtelezo ikionekana.
Lilikua ni lile joka la ajabu ambalo ni k**a kambale, yule joka alitoa paa la nyumba nililiokuwepo kisha akawa ananitazama na jicho lake lenye kiini cha kijani,, nilihisi mkojo kwa sababu mojakwamoja alikua aniangalia mimi akitaka kunimeza.
Zile kambba ndio zilinifanya nisiweze kukimbia nikajikuta nagala gala chini kwa kuona kifo mbele yangu sauti ya yule mtoto bado ilisikika kwa sana.
Nilianza kuona yule joka akianza kuleta kichwa chake akipanua mdomo uliojaa damu za watu na wanyama wa eneo lile. Bado kule nje wamasai walipiga yowe.
Lisoyani alinifunga kamba lakini hakufnikiwa kumthibiti nyoka mpaka kujua niliko, ina maana na yeye kaliwa au kashachukuliwa na kupelekwa na yule joka karudi tena kwa ajili ya kunimaliza,, nilijiuliza maswali hayo like joka likiwa lishafikisha kichwa karibu yangu kabisa yani yale maji yaliokua yanamzunguka yalinimwagikia k**a naogeshwa na ndoo na bado yeye hayakumuisha kabisa.
Sikuona msaada wowote zaidi ya kufunga macho ili nikifungua nijikute ndani ya tumbo la nyoka au ku*imu. Nilitamani ata niongee kihisia na lisoyani ila zile kelele nisingeweza kufanya vile
Nilifunga macho kisha nikamuomba mungu wangu kwa mara ya mwisho ndipo nikasubiri kifo
Ilichukua dakika k**a mbili bado sikuona tukio la kumezwa na yale maji sikuyasikia tena yananimwagikia,, ile hali ilinishtua kidigo ikanipelekea nifungue panzia la macho yangu tena.
Macho yalipokuwa wazi nilitazama juu sikumuona tena lile joka zaidi ya kuona nyota na mbalamwezi. Ilikua ni hali ya kushangaza kwangu iweje nimuoene mda ule na kwa sasa simuoni.Lakini ghafla nilisikia sauti ya lile joka nje na pia sauti k**a ya lisoyani. Kwa kuwa hisia zangu za kusikia zilikua kubwa kuliko binadamu wa aina yeyote yule hivyo ikawa naisikia ipasavyo bali kelele za watu zilinizingua.
Sauti ya lisoyani haikuwa ile ya kuongea. Ilikua ni sauti ya samaki ambayo naweza kusema ni mru*i mwembamba wa aina yake. Ambao mru*i huo huwa anaubania kuupiga au kuukatisha katisha. Sijui labda wavuvi wanaijua hiyo sauti.
Niliposikia ile sauti nilijua moja kwa moja kwamba ndio maana lile joka liliondoka maana ile sauti ya samaki ya Lisoyani ilimsaidia kumjua alipo.
"Lisoyani, ndio anaenda kuchukuliwa?!!!!!!" nilijiuliza kwa mshangao.
Nilijijua kwamba mimi ni mbwa mwitu na pia ba nguvu kuliko bindamu wa kawaida ata k**a nisipo badilika. Zile kamba alizonifunga Lisoyani zisingeweza kunizuia mpaka mtu aje kunifungua. Ni bora nijiumize nibadilike kuwa Mbwa mwitu kuliko nibaki vile vile watu na yule mtoto mchanga pale chini wakiwa wanalia.
Nilijikusanya nyama, misuli mifupa yani namaanisha nilijivuta nguvu kwa kutoa pumzi kubwa mara mbili.
Baada ya kufanya vile nilianza kujitanua ile mikono niliyofunga ambayo ndio kiungio cha kamba ya miguu. Japo maumivu yalizidi ila wakati uke nilijitolea.
Nilijitanua mishipa ya damu ikawa inatokeza kuanzia ya kichwa mpaka mwilini. Joto kali likinijia huku nikihisi mwili unatanuka. Zile zilikua dalili tosha za mimi kukaribia kuwa mbwa mwitu. Sikutaka kubadilika mwili mzima lakini wakati nakata zile kamba nilihisi macho yanabadilika ila nilijizuia kwa kuivuta taswira ya sura ya Lisoyani.
Ilichukua dakika mbili kucha za mikono zikatokeza na mda ule ule zile kamba zilikatika mfano wa u*i wa kushinoa nguo. Nilichuchumaa chini hali ikitaka kuendelea kubadilika. Kucha zangu nilizizamisha kwenye udongo,huku maumivu ya kubadlika yakinizidi na mimi nikizidi kujizui nisiendelee kubadilika.
Kiukweli ilikua ni mara yangu ya kwanza kujizuia kuendelea kubadiluka katika umbo la kimbwa mwitu, kwani haikuchukua ata dakika tano nilishangaa kuona kucha zikirudi zenyewe. Ile hali ata mimi niliifurahia sana kuona kwamba sasa naweza nikajizuia na ninaweza kujiweka mbwa mwitu.
Baada ya kuona kwamba nimerudi kawaida nilinyanyuka haraka kwenda kwa yule mtoto mchanga anayelia.
Nilifika katika lile eneo alilokua cha Ajabu nilikumta katika k**a kabeseni fulani. Mawazo yangu nilijua lina maji ila nilipo tumbukizqla mikono nilikuta ni mafuta meng sana yalijazwa k**a maji na yule mtoto akiwa ndani.
Nilijiuliza kwanini yupo mule na ukicheki ata kitovu chake hakijakatika vizuri.
Sikuwa na muda wa kupoteza kumjadili yule mtoto japo mpaka leo hii huwa inanitatiza.
Nilichoamua nilimbeba vile vile na mafuta yake kisha kulikua na shuka nyingine ya kimasai maeneo yale niliichukua ni kumviringishia kwa usalama zaidi maana mama na ndugu zake wamekimbia kwa ajili ya lile joka.
Nilipomaliza kufanya vile nilianza kutoka nje ambapo nilipokelewa na moshi mzito wa baadhi ya nyumba kuungua huku baadh ya wamasai wanakimbia. Ilikua ni k**a vita eneo lile kwani ata wale walio aminiwa ni walinzi nao walijikuta wakiliwa na lile joka kambale.
Nilizisikia sauti ya mngurumo wa lile koka mbele kidogo,, ambapo sikuweza kuliona kwa juu kwa ajili wa moshi wa pale.
Mtoto akiwa mkononi bila kujali nilipiga hatua za farasi kukimbia kuelekea kule kwenye uwanja wa mapambano. Njiani kila niliyekutana nae alikllia sana huku wengine wakililia ng'ombe zao, na wengine wakilia vibanda vyao, nafsi iliniuma sana ni bora ata nnbgekua kwetu kuliko unafika ugenini walipoishi kwa amani ila unaleta maaafa makubwa kwa muda mfupi,
Nilipita vibanda kadhaa nikikitiza maz**i ya ng'ombe ambayo hayakuwa na ng'ombe..
Mbio zangu ziliishia ukingoni baada ya mbele yangu kukutana na lile joka halafu chinu kulikua na baadhi ya wamasai wakilipiga na mikuki na sime japo hawakumuambulia ata kumgusa zaidi ya wao ndio walikua wanailiwa. Lakini yule joka alionesha hapambani tena bali alikua anaelekea kwenye ile njia ya ziwa tulikotoka na LISOYANI. Nilijitahidi kumuangalia sana k**a nitamuona LISOYANI lakini sikuweza kumuona ata kwenye lile kundi.
Nilizidi kuendelea kwenda katika ile vita nikijipenyeza hivyo hivyo..........ITAENDELEA......
NAPENDA KUWAOMBA RADHI KWA KUCHELEWA KWA SIMULIZI ZA HUMU NDANI,,
Ahsanteni NAWAPENDA WOTE.....