04/03/2024
MKUU WA WILAYA YA MBINGA ASHIRIKI KIKAO MAALUMU CHA BARAZA LA MADIWANI WA HALMASHAURI YA MJI WA MBINGA KUJADILI RASIMU YA MPANGO WA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2024/2025.
Mkuu wa Wilaya ya Mbinga *Mhe. Aziza Ally Mangosongo* amehudhuria kikao maalumu cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga kujadili rasimu ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025, Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi mdogo wa Halmashauri na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na baadhi ya wananchi.
Aidha, Akitoa salamu za serikali katika baraza hilo Mkuu wa Wilaya Mbinga, Alitumia nafasi hiyo kumshukuru Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kutoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya halmashauri ambayo inaakisi ukuaji wa sekta mbalimbali ikiwemo afya,elimu,maji,kilimo, miundombinu.
Hata hivyo Mhe.Mangosongo Mkuu wa Wilaya ya Mbinga alisisitiza kwamba ili mikakati na mipango iliyopo iweze kuwa na ufanisi mzuri na itekelezeke ni lazima bajeti hiyo iendane na kasi ya ukusanyaji wa mapato sambamba na kubuni vyanzo vipya vya mapato vyenye tija.
Alikadhalika, Dc Mangosongo alitumia nafasi hiyo kuwataka viongozi kushirikiana katika kuhakikisha wafanyabiashara wanauza sukari kwa bei elekezi na kuthibiti uingizaji holela wa sukari kinyume na sheria pamoja kuwabaini wanaofanya vitendo hivyo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa kukiuka miongozo.
Akiwasilisha rasimu ya mpango wa bajeti, ndugu Paschal Masatu, Afisa mipango wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga, Alibainisha kwamba Halmashauri imekadiria kukusanya Tzs bilioni 3.4 kutoka vyanzo vya mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2024/25, Ikiwa ni ongezeko la 39.5% kutoka makadirio ya fedha kwa mwaka uliopita wa 2023/2024.
Mwisho nao Meneja wa taasisi za RUWASA, TARURA na MBIUWASA waliwasilisha bajeti zao ili baraza hilo liliridhie zipitishwe kwa ajili ya utekelezaji, Ambapo Meneja wa TARURA Wilaya ya Mbinga Mhandisi Oscar M***a alisema TARURA inatarajia kutumia Tzs bilioni 2.4 kwa mwaka fedha 2024/25 kwa ajili ya kufungua barabara mpya, ujenzi wa madaraja, vivuko, makaravati na matengenezo mengine.
Vilevile, Nae Meneja wa RUWASA Mhandisi Mashaka Sinkala alisema RUWASA inatarajia kutumia tzs Milioni 977 kwa ajili ya miradi mipya na kuboresha miundombinu Pamoja na hilo MBIUWASA nao wanatarajia kutumia zaidi ya Tzs Bilioni 4 kwa ajili ujenzi wa miradi mipya mikubwa ili kuhakikisha mji wa Mbinga unakuwa na huduma ya uhakika ya maji ili kuendana na kasi ya uchukuaji na mahitaji.
Imetolewa na
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbinga.
March 04, 2024.