26/12/2025
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Ardhi (ARU) Balozi Salome
Sijaona amewataka wahitimu wa ARU kushiriki kikamilifu katika kutatua
changamoto mbalimbali zinazokabili jamii
Akizungumza katika mahafali ya kumi na tisa (19) ya chuo hicho
ambayo yamefanyika leo tarehe 18 Disemba, 2025 Balozi Sijaona
amesema wahitimu wa ARU wana uwezo wa kushiriki kutatua
changamoto mbalimbali kwa sababu mitaala ya ARU imewandaa
kukabiliana na changamoto za jamii kinadharia na kivitendo ambazo
zinawasaidia kuwa tayari kujiajiri au kuajiriwa.
Balozi Sijaona amesema ARU itaendelea kuzingatia utekelezaji wa
mipango ya kitaifa ikiwa ni pamoja na maelekezo mbalimbali
yaliyotolewa katika dira ya maendeleo ya taifa 2050
Naye Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Evaristo Liwa amesema
bunifu mbalimbali za wanafunzi wa ARU zinazolenga kutatua
changamoto za jamii zinaendelea kutazamwa kwa umakini mkubwa na
kwamba kwa mwaka wa masomo uliopita ARU mesajili hatimiliki nane
(8) ambazo zitasaidia kutengeneza ajira kwa jamii,
Katika mahafali hayo, jumla ya wahitumu 1,571 wametunukiwa shahaba
mbalimbali ambapo wahitimu 18 wametunukiwa Shahada za Uzamivu,
wahitimu 72 wametunukiwa Shahada za Uzamili na wahitimu 1,471
wametunukiwa Shahada za awali
Kwa maelezo zaidi kuhusu program zinazotolewa na ARU tafadhali
tembelea www.aru.ac.tz
6 wizara_elimutanzania
-tz
Gormipango_uwekezaji
Earualumni
aru_architecture
Earu_ai_lab
aruso_media
📸 pic by