12/10/2025
𝗛𝗢𝗝𝗔
..Hoja ya Kwamba Mchezaji mzuri huitwa kwenye Timu ya Taifa na Mchezaji mbaya huachwa nafikiri Haina mashiko na imekosa Upembuzi wa kina kutoka Kwa wachambuzi Wetu Baadhi na hili suala limekuwa linajirudia Kila Siku Timu za taifa zinapotaja vikosi vyao, Wachambuzi Wetu wamekuwa wakituaminisha Sana mchezaji mzuri ni yule anayeitwa Timu ya Taifa tu.
Ni aibu Iliyoje Watu ambao wanaaminika na wadau wa Mpira nchini kupewa vipaza sauti na Media kubwa Kuuchambuwa mpira Bila ufafanuzi wa kina na badala yake wanajikita zaidi Kueneza uchawa na Mapenzi Yao Kwa Timu au mchezaji Binafsi Aliyeitwa Timu ya Taifa.
Watu wanawaongelea Direct "Ahoua na Pacome" ambaye ameitwa Timu ya Taifa Ivory coast Wakimsifia Sana kwamba ni mzuri kuliko Ahoua ndiomaana ameachwa. Wanasahau k**a wachezaji Hawa hawalingani umri wao hata Takwimu msimu uliyoisha na huu wa sasa Ahoua Yupo juu Ya Pacome kwa Takwimu kwa Sasa, Hilo lipo wazi namba zinaongea, lakini pia Ahoua Mdogo Kiumri Dhidi ya Pacome kiasi kwamba Ivory Coast wanaweza Kumwita katika Kikosi Chao na kumuongezea Profile wakafaidika naye Kwa Miaka Zaidi ya 4 mbele Kuliko Pacome ambaye Umri umeshaenda...
Kimsingi Pacome hawezi kuisadia Ivory coast miaka miwili mbele. Kuitwa kwake pia ni fluke tu kitu ambacho kinaweza kisitokee Tena Kwenye Kikosi Kijacho.
Wachambuzi Wanatakiwa wakumbuke Kocha "Dunga" Na Brazil yake 2010 Alimuacha Ronaldinho Gaucho Tena wakiwa wanaelekea kwenye Michuano mkubwa ya Kombe la Dunia iliyofanyika Afrika ya Kusini, Cappelo Kocha Wa Uingereza Aliwahi Kumuacha Jermaine Difoe Akiwa wamoto kabisa pale Sandarland akaondoka na Peter Croach...
Labda Nataka Kusema Nini?
Mchezaji kuachwa kwenye Timu ya Taifa au kutoitwa inategemea falsafa ya Mwalimu au aina ya Mechi Ambayo anaenda kucheza, Na siyo tafsiri ya kwamba Ahoua Hajui ndiomaana hajaitwa au Pacome anajuwa Sana ndiomaana kaitwa Ivory coast.
Ukiangalia Kikosi Kilichoanza Jana Ivory coast Dhidi ya Shelisheli Utagundua Mwalimu na F.A ya Cote D'Ivoire Hawakuuchukulia Kwa Uzito Sana Mchezo Wa Jana, Utaona kwenye Kikosi chao Wale Akina Frankie Kessie, Adingra na wengine wanaounda Kikosi Cha Kwanza Hawakuanza kabisa. Kwahiyo Pacome Ni Mchezaji wa kawaida Sana Kule Cote D'Ivoire Ambaye wanaweza kumtumia kwenye mechi ndogondogo ambazo hazina presha. Mfano hapa Kwetu Tukaamua kuwatumia akina "Hilika, Saadun, Chikola" Kwenye Mechi labda Dhidi ya Burundi au Kenya Mataifa ambayo Tunaweza kuyamudu kisoka bila Akina Msuva, Feisal, Samata".
MOUD Mtanzania ゚viralシ ゚viralシfypシ゚