ALPHER TV

ALPHER TV ALPHER PODCAST MEDIA
C.E.O AND OWNER
PLATNUMZ
you can follow in social network
Instagram
YouTube

Msanii mkubwa na Mwanasimba kindakindaki, Mbosso atakiwasha katika Simba Day 2025 itakayofanyika Septemba 10, 2025 kweny...
30/08/2025

Msanii mkubwa na Mwanasimba kindakindaki, Mbosso atakiwasha katika Simba Day 2025 itakayofanyika Septemba 10, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa.

Bila chuki wala fitina wasanii wa Tanzania wenye nguvu kimataifa ni watatu tu yani Diamond, Alikiba na Rayvanny kwa saba...
20/08/2025

Bila chuki wala fitina wasanii wa Tanzania wenye nguvu kimataifa ni watatu tu yani Diamond, Alikiba na Rayvanny kwa sababu zifuatazo na nitawapanga kwa namba.

1. DIAMOND PLATNUMZ
Huyu anakaa hapa kwa rekodi zake kubwa alizoweka kuanzia shows, tuzo na nguvu ya ushawishi na mpaka sasa bado amesimama k**a mwanamuziki mwenye nguvu zaidi kimataifa kutoka Tanzania.

2. ALIKIBA
Huyu anakaa namba mbili kwa makubwa aliyofanya zikiwemo shows za kimataifa na tuzo za kimataifa ambapo mpaka leo ukimtoa Diamond hakuna tena mwanamuziki mwingine aliyefanya mambo makubwa kumzidi yeye hili halihitaji unafiki Alikiba kukaa hapa ingawa kwasasa ameshuka sana na simuoni kwenye ushindani tena.

3. RAYVANNY
Hapa ukitaka kubisha unatakiwa uniambie unabisha kwasababu gani na k**a sio Rayvanny ni nani? Kwasababu Rayvanny amepata bahati ya kupanda majukwaa makubwa na kufanya kolabo kubwa hasa kupitia wimbo wake wa Tetema kitu ambacho kinamfanya kuwa mwanamuziki wa 3 kutoka Tanzania kufanya kolabo kubwa na kutumbuiza kwenye majukwaa makubwa. Sipendi kuihesabu Tuzo yake ya B.E.T sababu kipengele alichoingia hakina heshima kwasababu ni kipengere ambacho hakijumuishi wasanii wakubwa kutoka duniani bali ni wale wanaotazamiwa kukua ndio maana alishiriki kile kipengere kipindi anachipukia na sasa amekuwa hana tena nafasi ya kushiriki B.E.T sababu panatakiwa wale wasanii wakubwa ambao sio chipukizi. Kipengere alichoshinda Rayvanny ndicho alicho shiriki Abby Chams "Views Choice" wakati kutoka Afrika kipengere wanacho shiriki wasanii wakubwa ni "Best International Act" ambacho ukishinda unahesabika k**a namba moja Afrika kwahiyo siku akiwa mkubwa hapa Afrika mtamuona kwenye kipengere cha "Best International Act".

Kwenye hii orodha ukitaka msanii mwingine nje na hao aingie kwenye anga la kimataifa unatakiwa uje na data amefanya jambo gani huko kimataifa la kufanya aingie kwenye hiyo 3 bora sababu hapo hatupo kwenye ushabiki tupo kwenye uhalisia na data, ukibisha weka data watu wazione ili wakuamini. Ukiumia na hauna data unaruhusiwa kutukana tu maana mashabiki wa Bongo wanapenda tu umsifie msanii wake hata k**a hana alichofanya...

Alpher Platnumz ✍

 : Aliyekuwa mshambuliaji wa Singida Black Stars, Seleman Mwalimu 'Gomez' amejiunga na klabu ya Simba Sc kwa mkopo wa mw...
16/08/2025

: Aliyekuwa mshambuliaji wa Singida Black Stars, Seleman Mwalimu 'Gomez' amejiunga na klabu ya Simba Sc kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea klabu ya Wydad Casablaca inayoshiriki ligi kuu Nchini Morocco.

Gomez ambaye alijiunga na Wydad mwishoni mwa msimu uliopita anarejea Tanzania kwa mkopo huku akitarajiwa kuungana na mshambuliaji mwenzake Jonathan Sowah ambaye naye alikuwa Singida Black Stars.

Mwalimu alikuwa sehemu ya kikosi cha Wydad Casablanca kilichoshiriki michuano ya kombe la Dunia la FIFA ngazi ya klabu huko Marekani ambapo alicheza mechi mbili kati ya tatu za hatua ya makundi.

Nahodha wa Bafana Bafana kwenye CHAN2024, Neo Maema amepewa mkono wa kwaheri na klabu yake ya Mamelodi Sundowns baada ya...
15/08/2025

Nahodha wa Bafana Bafana kwenye CHAN2024, Neo Maema amepewa mkono wa kwaheri na klabu yake ya Mamelodi Sundowns baada ya kuhudumu klabuni hapo kwa miaka minne na kuifungia magoli 13, akisaidia 'assists' mengine 14 kwenye mechi 120. Instagram

Maema 29, raia wa Afrika Kusini ambaye anatarajiwa kujiunga na Simba Sc baada ya kutamatika kwa michuano ya CHAN2024 ameisaidia Sundowns kushinda Mataji manne ya Ligi Kuu Afrika Kusini, taji moja la Nedbank Cup, taji moja la MTN8, na taji moja la African Football League kwa kipindi cha miaka minne cha utumishi wake klabuni hapo.

Ingawa muziki umemletea mafanikio makubwa na kumfanya kuwa mmoja wa wasanii matajiri Afrika, Diamond Platnumz amesema wa...
01/08/2025

Ingawa muziki umemletea mafanikio makubwa na kumfanya kuwa mmoja wa wasanii matajiri Afrika, Diamond Platnumz amesema wazi kuwa haamini muziki k**a biashara ya muda mrefu. Kwa nini?

Kwa mujibu wa Diamond, muziki unahitaji uwekezaji mkubwa sana, hasa kwa wasanii wa kiwango cha kimataifa. Kutengeneza video moja ya kimataifa kunaweza kugharimu hadi milioni 490 za Kitanzania, lakini mapato sio kila wakati huendana na uwekezaji huo. Aidha, wasanii hulazimika kushindana kimataifa kwa ubora wa sauti, video, na masoko; jambo linaloongeza gharama zaidi.

Diamond anaamini muziki ni jukwaa la kuanzisha biashara nyingine, sio chanzo cha kutegemewa kwa muda mrefu. Anasema kuna hatari kubwa ya kufilisika k**a msanii au lebo haina usimamizi imara na mzunguko wa mapato wa kueleweka.

Kwa sasa, anatumia jina lake kuendesha biashara k**a Wasafi Media, Wasafi Bet, na miradi mingine. Anaamini Tanzania inahitaji wawekezaji wenye mitaji mikubwa ili kulifanya soko la muziki kuwa la kimataifa na lenye faida kwa wasanii wengi zaidi.

Kwa kifupi, muziki ni biashara ya mabilionea, lakini sio kila msanii anaweza kustahimili gharama zake, hasa bila mfumo madhubuti wa kifedha na kisheria.
Powered By: | ✍️: au Alpher Platnumz

Mheshimiwa .jmagufuli , ambaye ni miongoni mwa wagombea wa nafasi ya Ubunge kupitia Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), amew...
01/08/2025

Mheshimiwa .jmagufuli , ambaye ni miongoni mwa wagombea wa nafasi ya Ubunge kupitia Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), ameweka historia kwa kuwa mgombea wa kwanza kujitokeza rasmi kuomba kura kwa Wajumbe.

Kwa ujasiri, unyenyekevu na dhamira ya kweli ya kuwatumikia vijana na Taifa kwa ujumla, Mh. Jesca ana maono makubwa ya maendeleo ya vijana na Watanzania kwa ujumla

πŸ—³οΈ Wajumbe wa UVCCM,
Hii ni nafasi ya kuchagua kiongozi mwenye maono, uthubutu na rekodi safi ya utumishi.

βœ… Kura zenu kwa Mh. Jesca J. Magufuli ni kura ya kuamini uwezo wa kijana na mwanamke mchapakazi!
βœ… Ni kura kwa mabadiliko chanya ndani ya UVCCM!
βœ… Ni kura kwa uwakilishi wa kweli na sauti ya vijana!

πŸ“Œ Tuchague kiongozi anayetuona, anatuelewa, na yuko tayari kutupigania. Sauti ya Jesca ni sauti ya kizazi kipya!


  Huyu hapa beki mpya wa Simba SC; Anaitwa Rushine De Reuck kutoka Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa mkataba wa mwa...
30/07/2025

Huyu hapa beki mpya wa Simba SC; Anaitwa Rushine De Reuck kutoka Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa mkataba wa mwaka mmoja….

Je, wamepata au wamepatikana???

🚨 πŽπ…π…πˆπ‚πˆπ€π‹: Mohammed Bajaber joins Simba SC on a two-year deal! ✍️🦁  ALPHER TV  The talented midfielder/winger has signe...
30/07/2025

🚨 πŽπ…π…πˆπ‚πˆπ€π‹: Mohammed Bajaber joins Simba SC on a two-year deal! ✍️🦁
ALPHER TV
The talented midfielder/winger has signed his contract and is now officially a Simba player.

As a result, he will not be eligible to feature in the upcoming CHAN tournament.

Thoughts on this signing, Simba fans? πŸ’­



πŸ’ͺwenyenchi

Simba sc watikisa Jiji kwa sajiri TATU zamoto
24/07/2025

Simba sc watikisa Jiji kwa sajiri TATU zamoto

Aliyekuwa nahodha wa klabu ya Simba Sc Mohamed Hussein (Zimbwe Jr) ameaga rasmi klabu hiyo baada ya mkataba wake kumaliz...
19/07/2025

Aliyekuwa nahodha wa klabu ya Simba Sc Mohamed Hussein (Zimbwe Jr) ameaga rasmi klabu hiyo baada ya mkataba wake kumalizika na kutokuongezwa ambapo Kupitia ujumbe aliouandika katika ukurasa wake Mohamed ameushukuru uongozi, benchi la ufundi, Wafanyakazi wa klabu na Mashabiki wa Simba Sc kwa sapoti waliompa kwa kipindi chote alichoitumikia timu hiyo kwa takribani miaka 11.

Katika ujumbe wake Mohamed Hussein alieleza kuwa maamuzi ya kuondoka Simba SC yamelenga maendeleo na maslahi yake binafsi pamoja na kukuza weledi wake wa soka ambapo amesisitiza kuwa kuipigania nembo ya Simba Sc kulikuwa ni heshima kubwa kwake.

Huku akiaga rasmi tetesi zimeanza kuzagaa kwamba beki huyo mahiri yupo mbioni kujiunga na Yanga SC, wapinzani wakubwa wa jadi wa Simba ingawa bado hakuna taarifa rasmi kutoka klabu husika, Mashabiki na Wachambuzi wa soka wanaendelea kufuatilia kwa karibu mustakabali wa nyota huyo.

Address

Mjini
Morogoro

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00

Telephone

+255625788632

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ALPHER TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to ALPHER TV:

Share

Category